Usindikaji wa viazi vitamu

By, Melkisedeck Shine.

familia-mapenzi-na-mahusiano.png

Usindikaji wa viazi vitamu

Ingawaje viazi vitamu vinatumiwa kama kiazi kilicho chemshwa, katika maeneo mengine ya Afrika mashariki vinatumika kutengeneza chipsi na unga kwa ajili ya kuhifandi chakula na kwa ajili ya kuuza katika masoko madogo madogo vijijini na hata mijini.

Pamoja na faida ya kuhifadhi, utengenezaji wa chipsi na unga wa kuanika una faida zifuatazo:

1. Husaidia utunzaji na usafirishaji
2. Kupunguza ukubwa wa viazi na upotevu wa viazi kwa sababu viazi uharibika haraka na kama viazi vikiachwa ardhini wadudu (fukuzi) huweza kushambulia
3. Huongeza muda wa kuhifadhika
4. Unga na chipsi vina virutubisho vingi kwa vile kiwango kikubwa cha maji kwenye kiazi kinakuwa kimetolewa kwa hiyo kiwango cha protini, wanga, pectini, mafuta na chumvichumvi huongezeka
5. Huongeza chanzo cha mapato kwa wakulima kama vile upatikanaji wa masoko na chanzo kipya cha kipato 6. Husaidia kusambaza taarifa kwamba viazi vitamu huweza kuwa zao la biashara lenye matumizi mbalimbali na watumiaji wengi

Njia mbalimbali za utengenezaji wa kienyeji kama vile kuanika juani viazi vilivyomenywa, na kuanika viazi vilivyokatwa katwa juani uweza kusababisha:

1. Njia hizi hutegemea sana hali ya hewa (kama mvua ikinyesha inabidi kuanua na kwenda kuhifadhi sehemu kavu)
2. Zinahitaji watenda kazi wengi kwa ajili ya kumenya, kukatakata, kuanika juani, kugeuza geuza unga wakati wa kuanika, kulinda unga ili usiliwe na mifugo, kuanua unga kama mvua ikinyesha nk
3. Kuto kuwa na udhibiti wa vimeng’enyo wakati wa kuanika husababisha kuwa na unga unaotoa harufu na wenye rangi ya kizambarau
4. Ukubwa wa chipsi hutofautiana
5. Ukosefu wa uwiano katika ukubwa wa vipande vyake
6. Kutokuwa na usawa na kiwango cha rangi
7. Uharibifu wa ngozi ya viazi
8. Kuwepo kwa mchanganyiko usiotakiwa.

Ni muhimu kujua kuwa chipsi na unga kutokana na aina mbalimbali ya viazi utofautiana katika tabia kama vile vionjo na rangi. Hivyo, ni muhimu kuonja, kutambua na kutenganisha aina mbalimbali ya viazi wakati wakutengeneza chipsi kavu , unga na mlamba ili kupata unga wa viazi wenye rangi, harufu nzuri na virutubisho bora. Kwa vile inahusisha gharama ni bora teknolojia hii ikatumiwa na vikundi vya wakulima. Njia bora za utengenezaji wa viazi zinalenga kuboresha zile za kienyeji.

Hatua za kufuata ili kutengeneza chipsi na unga bora wa viazi vitamu ni kama zifuatazo:

Uchaguzi wa mali ghafi

Chagua viazi vizuri kwa ajili ya utayarishaji

Kuosha/ kusafisha kiazi

Kiazi kisafishwe kwa maji na kuhakikisha udongo wote umeondolewa na sehemu zilizoharibika zitolewe ili kupata kiazi safi Pipa lakuoshea limetengenezwa kwa ajili ya kusaidia uoshaji. Pipa hilo lina dramu la lita 200 lililofungwa kwenye mpingo wa sambamba. Pipa hilo limekatwa kwa urefu ili kutoa mlango ambao unaweza kufungwa na kufunguliwa wakati wa uwekaji na utoaji viazi wakati wa kuosha. Ndani ya pipa hilo kuna brashi zilizofungwa kwa mkabala. Pembeni imefungwa kuwezesha kuzungusha pipa hilo na kuosha viazi hivyo. Upande mmoja wa pipa unaweza kufunguliwa ili kutoa maji machafu baada ya uoshaji. Pipa hilo linaweza kutumika kuosha hadi kilo 40 za viazi vitamu kwa dakika 10-20 kwa kutumia lita 30 za maji masafi. Kama mapipa hayapatikani, mabeseni makubwa yanaweza kutumika. Baada ya kuosha pitisha viazi kwenye maji masafi.

Ukataji

Baada ya kusafishwa viazi vitamu inabidi vianikwe kwa muda kwenye sehemu safi juani kwa dakika 10 kuondoa maji kwenye gozi. Mashine ya mkono au motor inaweza kutumika kukata viazi vitamu katika vipande vinavyolingana ukubwa.

Kuweka majini

Vipande vilivyokatwa vya viazi vyeupe viwekwe ndani ya maji kwa dakika 90 ili kuzuia upotevu wa rangi. Kiasi cha maji kiwe ni mara mbili ya uwingi wa vipande vya viazi na yawe ni ya kutosha tu fufunika vipande hivyo. Viazi-karoti visiwekwe kwenye maji kuzuia upotevu wa vitamini A.

Uanikaji

Vipande vya viazi kisha huanikwa juani kwenye kitalu kilichoinuliwa kwa muda wa masaa 4-6 kama hali ya hewa ni nzuri au kwenye vyombo vya kuanikia kutumia kuni au mkaa kama chanzo cha joto. Matrei ya kuanikia yawe yameinuliwa juu ya udongo kuzuia vumbi na uchafu wingine. Kama uanikaji sio wa kutosha, chipsi zitakuwa na hatari ya kupata ukungu wakati wa kuhifadhi. Muda wa kuanika utategemea ukubwa wa vipande vya viazi, kugeuzwa geuzwa wakati wa kuanika, na kiasi cha chipsi kilichowekwa ndani ya trei. Ni vizuri kuanza uanikaji wakati wa asubuhi.

Uchambuaji

Viazi vitamu vilivyoanikwa vifanyiwe uchambuzi ili kupata vyenye ukubwa sawa kabla ya kufunga kwenye maboksi au kufanyiwa utengenezaji mwingine, kwa vile inaweza kuharibu ubora au matumizi yaliyokusudiwa au bei yake.

Kusaga

Viazi vilivyoanikwa vinaweza kusagwa ili kupata unga.

Ufungaji

Unga wa viazi vitamu unaweza kufungwa kwenye mifuko ya nailoni, ndoo au makopo. Chipsi zinaweza kutunzwa kwenye magunia safi ya katani au magunia ya visalfeti au mifuko ya nailoni. Uwekaji wa nailoni nyeusi ndani ya mifuko ya kuhifadhia husaidia kupunguza upotevu wa vitamini A (ambayo huweza kuharibiwa na jua) wakati wa kuhifadhi.

Kuhifadhi

1. Viazi hivyo viwekwe kwenye sehemu nyenye ubaridi na kavu
2. Yenye hewa ya kutosha.
3. Mabanzi ya mbao yanaweza kutumika kubania mifuko yenye viazi ili kuzuia unyevu usiingie toka sakafuni.
4. Ukaguzi wa mara kwa mara ufanywe ili kubaini muda wa kuhifadhi viazi kabla ya kuharibika kwenye vyombo vya kuhifadhia vya aina mbalimbali na kuzuia wadudu na panya waharibifu.
5. Mifuko ni lazima iandikwe majina ya:
6. Mkulima aliyezalisha na mtengenezaji, tarehe ya kutengenezwa, jina la kiazi; na muda wa mwisho kutumika.

Utambulisho

Muda wa matumizi hutofautiana kutegemea aina ya viazi kwa hiyo jaribio lifanywe ili kupata muda kwa kila aina. Kama aina ya virutubisho inahitajika kuonyeshwa kwenye mifuko basi sampuli zichukuliwe kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Kumbuka: Ili kulinda ubora wa chipsi kavu zilizohifadhiwa, unapaswa kufanya ufuatiliaji wa: kiwango cha unyevu (kiwe chini ya asilimia 10-15). Kupima unyevu, uma kipande kwenye meno mpaka usikie kiinapasuka bila kunata mdomoni. Au saga kipande kwa chupa mpaka unga mkavu usionata kwenye paba la chupa upatikane. Vitu vingine vya kufuatilia ni rangi na mwonekano; kutokuwepo kwa harufu mbaya; usafi wa chipsi; kutokuwepo kwa uchafu mbalimbali kama vile udongo; nywele na maumbo yanayolingana.


Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Usindikaji wa viazi vitamu;

a.gif Kompyuta

Kompyuta ni mashine ya elektroniki inayotumika au kushughulika na taarifa, kama unavyotumia kisu na
patasi kwa kuchongea vinyago vya miti, unatumia kompyuta kuandaa nyaraka, barua, michoro n.k. Kimsingi
unaweza kutumia kompyuta kwa kazi mbalimbali.. endelea kusoma

a.gif Virusi vya kompyuta (computer virus)

Ni programu haramu yenye uwezo wa kujisambaa ndani ya kompyuta na kujiingiza ndani ya programu halali zinazotakiwa kufanya kazi mle. Ikisambaa inaathiri programu halali na kusababisha hasara. Virusi zinasambaa kwa njia ya intaneti lakini pia kwa njia ya sidii au diski yoyote ya kubebea data kati ya kompyuta. Virusi vinaweza kuharibu mafaili na kupunguza uwezo wa ufanyaji kazi wa kompyuta… endelea kusoma

a.gif Leo tujifunze lugha yetu ya Kiswahili

Leo tujifunze lugha teule ya Kiswahili.
1. password- Nywila.
2. juice - sharubati.
3. chips - vibanzi.
4. PhD - uzamifu.
5. Masters - uzamili… endelea kusoma

a.gif Kampeni ya Kudumisha Amani na Upendo

Kampeni hii ilianzishwa Rasmi Mwaka 2014 na Melkisedeck Leon Shine.
Lengo la kampeni Hii ni kudumisha Amani na Upendo bila kuangalia tofauti zetu.
Kampeni hii inaamini kuwa katika upendo kuna amani.
Kampeni hii inafundisha kwamba upendo wa kweli ni wa kuwafanyia wengine vile ungependa kufanyiwa nao. Kila mtu amfanyie mwenzake vile anavyopenda afanyiwe… endelea kusoma

a.gif Mambo muhimu kuyajua kuhusu nchi ya Tanzania

Haya ndio mambo ninayoyafahamu kuhusu TANZANIA.. endelea kusoma

a.gif Usindikaji wa viazi vitamu

1. Husaidia utunzaji na usafirishaji
2. Kupunguza ukubwa wa viazi na upotevu wa viazi kwa sababu viazi uharibika haraka na kama viazi vikiachwa ardhini wadudu (fukuzi) huweza kushambulia
3. Huongeza muda wa kuhifadhika
4. Unga na chipsi vina virutubisho vingi kwa vile kiwango kikubwa cha maji kwenye kiazi kinakuwa kimetolewa kwa hiyo kiwango cha protini, wanga, pectini, mafuta na chumvichumvi huongezeka
5. Huongeza chanzo cha mapato kwa wakulima kama vile upatikanaji wa masoko na chanzo kipya cha kipato 6. Husaidia kusambaza taarifa kwamba viazi vitamu huweza kuwa zao la biashara lenye matumizi mbalimbali na watumiaji wengi.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya kutetea watoto

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kuwakuza watoto kwa maendeleo bora ya kimwili, kiroho na kijamii kwa manufaa ya watoto na kwa manufaa ya watu wote kwa sasa na kwa baadae.
Kampeni hii inaamini kuwa watoto ni kama mali ambayo inawekezwa sasa kwa matumizi na maendeleo ya baadae… endelea kusoma

vichekesho-bomba-vya-siku.png

.

picha-kali.png
KADI-SALAMU-MCHANA-JION.JPG
vichekesho-bomba-vya-siku.png

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.