Elimu Kuhusu Madawa ya Kulevya, Mambo ya Msingi kujua Kuhusu dawa za Kulevya

By, Melkisedeck Shine.

MADAWA YA KULEVYA NI NINI?? NINI ATHARI ZA MADAWA YA KULEVYA KWA VIJANA NA TAIFA KWA UJUMLA?_

Madawa ya kulevya ni aina ya madawa au vilevi ambapo mtumiaji akishatumia mfumo wa mwili na akili yake hubadilika. Mtumiaji huweza kudhoofika kimwili au kupata madhara ya kiakili na baadhi huweza hata KUFA.

Yapo aina nyingi ya madawa ya kulevya kama vile bhang/marijuana, mirungi/miraa, Cocaine, Valium, Ugoro, heroine, petrol, spirit, mafuta ya taa, glue power etc..

Kwa ujumla aina hizi za madawa ya kulevya hutoa aina tofauti tofauti ya hisia (stimu) kwa mtumiaji. Mfano: Cocaine na bangi mtumizi hupata hisia kali na kuwa _Coolant_ huku mtumizi akipata stimu ya kuwa yuko Mamtoni (kwa maana nje ya Nchi hasa Ulaya, Jamaica na Marekani).

Kwangu mie madawa ya kulevya sio kitu kizuri kwa JAMII na TAIFA kwa ujumla. Vijana wetu wanateketea. NGUVU kazi ya TAIFA nayo inapungua.

MIKOA mahususi kwa utumizi uliokithiri wa madawa haya ni Dar Es Salaam, Tanga, Arusha, Mwanza, Morogoro na Mbeya. (Big cities).

Lakini pia ipo MIKOA mingine ambayo nayo ni wazalishaji wakubwa wa madawa haya ya kulevya hasa bangi na mirungi nayo ni Kilimanjaro, Manyara, Singida, Njombe, Iringa, Mara na Kigoma.

MIKOA mingine ya Tanzania nayo pia hupokea madawa ya kulevya kutoka ktk maeneo tajwa na kama inalima bangi na mirungi basi sio ktk kiwango cha juu ukilinganisha na MIKOA tajwa hapo juu.

Kwanini Vijana hujiingiza ktk matumizi ya madawa ya kulevya_??

1. Kufuata MIKUMBO; Baadhi ya Vijana hujiingiza ktk matumizi ya madawa ya kulevya kutokana na kufuata mikumbo ya marafiki na watu waliowazunguka ktk JAMII.

2. Kuukimbia Ukweli wa tatizo ulilonalo (To escape from realities of life) like quarrels, poverty, to be divorced etc.. Hali hii hupelekea Mtu ajiingize ktk utumizi wa madawa ya kulevya ili kuukimbia ukweli wa tatizo.. Mathalani umeachwa na mke/mpenzi, umasikini, ugonjwa n.k

3. Udadisi (Just for curiosity); Baadhi ya vijana hutumia madawa ya kulevya ili kujaribu kuonja tu ladha ya madawa husika.. Aone ladha au stimu zikoje n.k

4. Wengine hutumia madawa ya kulevya bila ya kujua kwanini wanatumia; Katika kundi hili mathalani mpenzio ni mtumizi wa madawa basi nawe kidogo kidogo hushawishiwa na kuanza kutumia madawa pia. Hali hii ilimtokea dada YETU Rehema Chalamila (Ray C) kipindi fulani mpaka baadae akapata msaada kutoka kwa Mh Rais Mstaafu Jakaya Kikwete.

5. Msongo wa mawazo; Hali hii huweza kumpelekea MTU husika akaamua kutumia madawa ili aondokane na stress. Japo utumizi wa madawa ya kulevya sio njia sahihi ya kupunguza stress.

6. For sociability and wish to have fun (Ili kuleta mjamiano nzuri ktk JAMII); Kwa sasa vijana wengi hujiingiza ktk utumizi wa madawa ya kulevya ili kuweza kufit ktk JAMII husika. Mfano kwa sasa Uvutaji wa bangi na ugoro haswa ktk maeneo mengi Nchini yamekuwa ni kama fasheni kwa Vijana na KIJANA asiyetumia huonekana mshamba au lofa. Hali hii hupelekea vijana kutokukubali kuwa washamba hivyo hujiingiza ktk utumizi wa haya madawa.

Tuangazie madhara ya madawa ya kulevya kwa JAMII na mtumizi husika_.

1. Kupungua kwa NGUVU kazi ya TAIFA. Hapa namaanisha NGUVU kazi ya TAIFA kwa maana ya vijana wakijiingiza ktk utumizi uliopitiliza wa madawa ya kulevya hushindwa kujiingiza au kujishughulisha ktk shughuli za uzalishaji hivyo huleta matatizo na ufanisi hupungua ktk kazi. Mtumiaji wa Cocaine akishatumia hapendi bughudha. Na hutaka kutulia sehemu moja kwa muda mrefu. Muda wa kazi yeye anakuwa anaisikilizia stimu.

2. Huongeza utegemezi kwa TAIFA na familia husika; Utumiaji uliopitiliza wa madawa ya kulevya hupelekea utegemezi mkubwa kwa TAIFA na JAMII husika kwa vile watumizi hawa hushindwa kujishughulisha. Chukulia mfano wa Msanii Abdallah Makwiro (Chid Benz) kwa sasa na jinsi alivyo kuhusiana na madhara ya madawa ya kulevya. Muda mwingi yupo _idle_.

3. Kutokea kwa Vifo kwa watumiaji wa madawa ya kulevya. Tumeshuhudia baadhi ya Wasanii wa nje hasa Marekani wakipoteza maisha. Mfano ni Msanii Mwana mama Whitney Houston ambae alikutwa bafuni akiwa amefariki baada ya kuzidiwa na haya madawa ya kulevya.

4. Mtumizi wa madawa ya kulevya hasa _Cocaine hupoteza sauti yake halisi na wakati fulani kifua hubana sana. Mathalani kwa Wasanii zile sauti zao nyororo hupotea kabisaa. Hali hii ikitokea ni hatari sana kwa Mtumizi husika. Rejea kipindi Chid Benz akiwa on fire kutokana na sauti yake nzuri kila Msanii alimshirikisha Chid Benz ktk wimbo wake. Huenda Chid Benz amemsaidia sana Diamond kutoka kisanii kwa vile Diamond alienda kumpigia magoti Chid Benz na hatimaye wakatoa single_ moja iliyobamba sana. Kwa sasa sauti ya Chid Benz IMEPOTEA. Na wala haina MVUTO tena.

5. Huweza Kuongeza maambukizi ya VVU yaani HIV/AIDS hasa kwa watumiaji wa Cocaine ambao hutumia bomba moja la SINDANO kujidunga miongoni mwao. Hali hii ni hatari sana kwa JAMII kwa vile tatizo moja hupelekea tatizo lingine.

6. Hupelekea magonjwa ya akili kwa Watumiaji husika wa madawa ya kulevya. Mtumizi huweza kuwa na _mental disorder_ kutokana na matumizi ya haya madawa ya kulevya. Idadi kubwa ya Vijana haswa wavutao bangi, mirungi, cocaine au huvutaji uliopitiliza wa ugoro huangukia huku na kuwa _VICHAA WA AKILI_.

NINI KIFANYIKE KUKABILIANA NA HALI HII YA MADAWA YA KULEVYA NCHINI_??

1. Vijana waelimishwe zaidi kuhusu madhara ya madawa ya kulevya na ikiwezekana hapa wadau kama WALIMU mashuleni, vyombo vya habari na watu mashuhuri ktk JAMII washirikishwe ktk utoaji wa Elimu hii ya madhara ya madawa ya kulevya kwa Vijana.

2. Serikali pamoja kwa kushirikiana na Vyombo vingine kama vile Bunge na Mahakama zitunge Sheria pamoja na kutoa adhabu kali sana ikiwezekana hata vifungo vya maisha kwa wote watakaopatikana na HATIA ya kujihusisha na madawa ya kulevya Nchini.

3. Ulinzi huimarishwe ktk Viwanja vya ndege, bandari zote (Bandari bubu nazo zizibitiwe) pamoja na mipakani kote. Hali hii itasaidia kupunguza na ikiwezekana kutokomeza kabisa Uingizwaji wa madawa ya kulevya Nchini.

4. Utayari na Uaminifu wa JESHI LA POLISI ktk KUSHIRIKI vita hii; Jeshi la Polisi liwe tayari ktk KUSHIRIKI vita hii kiukamilifu kabisa. Tumeshuhudia hapa majuzi Mkuu wa Mkoa wa DSM, Paul Makonda akiwataja baadhi ya askari Polisi wanaojihusisha na madawa ya kulevya. Hali hii ikiwepo ni NGUMU kufanikiwa vita hii kwa vile mipango yote itakayopangwa askari hawa wataivujisha.

5. Viongozi wa dini zote nao wawe tayari KUSHIRIKI vita hii kwa kutumia muda wao ktk majukwaa ya kiibada kukemea utumizi wa madawa ya kulevya. Lakini pia hata kama wao wanawajua wahusika basi wawe tayari kutoa ushirikiano kwa JESHI letu la Polisi ili kuidhibiti hali hiyo. Viongozi hawa wa dini wana nafasi kubwa sana ktk kukemea tatizo hili la Madawa ya kulevya kwa vile wao ni mababa wa kiroho.

6. Kutoa taarifa POLISI pale unapohisi kuwa Mtu, watu au kikundi FULANI kinajihusisha na madawa ya kulevya hasa ktk mazingira ya mtaani tunakoishi. Hii itasaidia sana kuwafichua kwa urahisi wale wote wanaojihusisha kwa namna moja ama nyingine na madawa ya kulevya. Kikubwa hapa ni kwa JESHI LA POLISI kuwalinda wale wote watakaowapatia taarifa hizi ili waendelee kuwa salama.

_Kwa ujumla vita ya madawa ya kulevya sio vita ya Kitoto hata kidogo_. Ni vita ya TAIFA zima. Ni vita ya kila mwana JAMII kwa vile madhara ya madawa ya kulevya huangukia ndani ya JAMII YETU. Hivyo kila mmoja wetu anabudi KUSHIRIKI, hivyo tusimuachie Kiongozi FULANI pekee. Abadani hatofanikiwa.

Hivyo ni mwito wangu kwa Viongozi wote Nchini kuwa tayari KUSHIRIKI ktk Vita hii, kuanzia ngazi ya chini kabisa hasa Wenyeviti wa Serikali za mitaa/Vijiji, Wajumbe wao wa Serikali za Mitaa/Vijiji, Madiwani, Maafsa Watendaji wa Mitaa/Vijiji, Makamanda wa migambo wa Vijiji/Mtaa na Maafsa Watendaji Kata nao pia ni chachu kubwa sana ya kufanikisha vita hii.

Viongozi hawa niliowataja endapo wakiwa waaminifu wanaweza kutoa msaada mkubwa sana kwa JESHI LA POLISI na Vyombo vingine vya Ulinzi na usalama ktk kudhibiti madawa ya kulevya kuanzia ktk hatua ya Uzalishaji, husafirishaji na hata hutumiaji. Viongozi hawa wapo karibu sana na JAMII kuliko Viongozi wengine na wao mengi huyafahamu kinagaubaga kabisa.

Mwisho Mh Makonda, RC DSM amethubutu kwa nafasi yake kuianza vita hii kubwa na endelevu. Nawe kwa nafasi yako ukiwa kama Kiongozi wa Serikali, Bunge, Mbunge, Idara ya Mahakama, Chama (Chama cha kisiasa au Chama cha ushirika), ASASI, Taasisi na RAIA mwema wa Nchi hii muunge mkono Mh Makonda ili mwisho wa siku tatizo la madawa ya kulevya libaki kuwa ni historia Nchini mwetu.

Na kutokea Dar Es Salaam Vita hii isambae ktk maeneo mengine ya Tanzania, kwa vile Vijana wa Tanzania hawapo tu DSM.

Kwa sasa inakadiriwa vijana takribani milioni mbili wameathiriwa na madawa ya kulevya Nchini. Ni idadi kubwa sana ukilinganisha hata na Watz wanaoishi na VVU Nchini. Ni Watanzania 1,585,385 tu ndio huishi na VVU Nchini Tanzania kwa sasa (kwa mujibu wa WHO).

Kumbe ndiyo KUSEMA kwa sasa madawa ya kulevya yana athari kubwa sana kuliko hata UKIMWI.

_Kwa pamoja tutokomeze madawa ya kulevya. Tanzania isiyo na madawa ya kulevya INAWEZEKANA_.

Na; Adinan LIVAMBA.

_Mwandishi ni mchambuzi na mfuatiliaji wa masuala mbalimbali ya Kijamii na Kisiasa. Kitaaluma ni Mhitimu wa SHAHADA ya Sanaa (Sayansi ya SIASA na Lugha) na Elimu wa CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM - Mwl Julius Nyerere Main Campus_.UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG

Endelea kusoma makala hizi zinazofanana na hii ya, Elimu Kuhusu Madawa ya Kulevya, Mambo ya Msingi kujua Kuhusu dawa za Kulevya;

a.gif JINSI YA KUJIOKOA IKITOKEA DHARURA YA MOTO NDANI

Inapotokea dharura ya moto ndani ya nyumba:
1 - Kitu cha muhimu ni kutoka nje salama haraka iwezekanavyo (as soon as possible)… endelea kusoma

a.gif Usiyoyajua kuhusu nyangumi

JE WAJUA?????…….
Nyangumi ni aina ya samaki Na ndie mnyama mkubwa kuliko
wanyama wote wanaoishi majini…….
Sifa za NYANGUMI hizi hapa…..
1»> moyo Wa nyangumi unakadiriwa kuwa Na kilo 600
2»> mtoto Wa Nyangumi anauwezo Wa kunywa Maji Lita
400 kwa Sikh.. endelea kusoma

a.gif Madhara ya kuitumia simu kwenye giza

Daktari justice Authur, ambae ni daktari kule africa kusini ameniomba kuwagawia hii na nyie pia. Amesema ni muhimu sana… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kutumia plastiki kuwekea chakula

Kuna hawa ndg zangu wanachemsha mihogo kisha wanaifunikia nailon ili ilainike vzr. Wengine huhifadhi ugali ktk mifuko ya plastic na kuitumbukiza kwenye maji moto ili ugali usipoe, wengine huchemsha supu ya kichwa cha ng'ombe ule ubongo wanautia ktk mifuko ya plastic na kuuchemsha ktk supu hiyo hiyo hadi unaiva ukiwa ndani ya plastic na plastic ndani ya supu. Je, hizi plastic madhara yake kitaalamu yakoje?.. endelea kusoma

[Kitendawili Kwako] 👉Natembea usiku na mchana

MPENZI-MLO-MWEMA-34NG.JPG

a.gif Jinsi Ya Kulima Soya

Maharagwe ya soya ni moja ya mazao muhimu katika jamii ya mikunde katika nyanja za uzalishaji wa kibiashara kutokana na kuwa na kiasi kikubwa cha protini (35-40%). Soya inatumika katika kuandaa vyakula vinavyoliwa vikiwa vibichi, vinavyovundikwa na vyakula nikavu, mfano maziwa, tofu, mchuzi pamoja na kimea… endelea kusoma

a.gif Madhara ya kutumia plastiki kuwekea chakula

Kuna hawa ndg zangu wanachemsha mihogo kisha wanaifunikia nailon ili ilainike vzr. Wengine huhifadhi ugali ktk mifuko ya plastic na kuitumbukiza kwenye maji moto ili ugali usipoe, wengine huchemsha supu ya kichwa cha ng'ombe ule ubongo wanautia ktk mifuko ya plastic na kuuchemsha ktk supu hiyo hiyo hadi unaiva ukiwa ndani ya plastic na plastic ndani ya supu. Je, hizi plastic madhara yake kitaalamu yakoje?.. endelea kusoma

a.gif Kampeni ya utunzaji wa wanyama pori

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kutunza wanyama pori kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa wanyama pori wakitunzwa vizuri wanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… endelea kusoma

a.gif Shairi la "Karudi baba mmoja.." KAMA MNATAKA MALI MTAYAPATA SHAMBANI

1. Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali,
Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili,
Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali,
Wakataka na kauli iwafe maishani… endelea kusoma

[Picha Nzuri] 👉Cheki huyu! Kweli mwanzo mgumu

[Msemo wa Leo] 👉Jaribu Mambo Kadiri uwezavyo

[Jarida la Bure] 👉Kijitabu cha Kilimo Bora cha Bamia

Usipitwe na Nafasi za kazi kwa leo

<<Bofya HAPA kujua zaidi>>

.

utotoni.gif
ml.gif

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.