YESU%20MFALME%20WA%20HURUMA.gif

Blog kwa Wakatoliki

Mpangilio wa kurasa Kwa Wakatoliki ndani ya AckySHINE

|| HOME || MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

.

images-7.jpeg

Sala Za Asubuhi

images-15.jpeg

Kwa njia ya sala Binadamu anampa Mungu Utukufu, Mungu anampa Binadamu Wokovu na Neema.

images-13.jpeg

Baada ya kusali: SALA YA KUWAOMBEA MAPADRE,

sasa tusali, Sala Za Asubuhi

Sala Za Asubuhi

SALA YA ASUBUHI.
Kwajina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

Ee Baba yetu Mungu mkuu,
Umenilinda usiku huu.
Nakushukuru kwa moyo,
Ee Baba, Mwana na Roho.
Nilinde tena siku hii,
Niache dhambi, nikutii.
Naomba sana Baba wee,
Baraka zako nipokee.
Bikira safi, Ee Maria
Nisipotee nisimamie.
Mlinzi mkuu malaika wee,
Kwa Mungu wetu niombee
Nitake nitende mema tu,
Na mwisho nije kwako juu. Amina.

NIA NJEMA.
Kumheshimu Mungu wangu
Namtolea roho yangu,
Nifanye kazi nipumzike
Amri zake tu nishike
Wazo, neno, tendo lote
Namtolea Mungu pote
Roho, mwili chote changu,
Pendo na uzima wangu
Mungu wangu nitampenda,
Wala dhambi sitatenda.
Jina lako nasifia,
Utakalo hutimia.
Kwa utii navumilia
Teso na matata pia.
Nipe, Bwana, neema zako
Niongeze sifa yako. Amina.

SALA YA MATOLEO.
Ee Yesu, kwa mikono ya Bikira Maria, na kwa maungano na sadaka yako kuu, ninakutolea sala, matendo, masumbuko na furaha zangu zote za leo. Ee Yesu, ufalme wako utufikie.

BABA YETU.
Baba yetu uliye mbinguni, jina lako litukuzwe. Ufalme wako ufike. Utakalo lifanyike duniani kama mbinguni. Utupe leo mkate wetu wa kila siku. Utusamehe makosa yetu, kama tunavyowasamehe na sisi waliotukosea. Usitutie katika kishawishi, lakini utuopoe maovuni. Amina.

SALAMU MARIA.
Salamu, Maria, umejaa neema; Bwana yu nawe. Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na Yesu mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Maria Mtakatifu mama wa Mungu, utuombee sisi wakosefu. Sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

KANUNI YA IMANI.
Nasadiki kwa Mungu Baba mwenyezi. Muumba wa Mbingu na dunia. Na kwa Yesu Kristo Mwanae wa pekee, Bwana wetu. Aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu, akazaliwa na Bikira Maria. Akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato. Akasulibiwa, akafa, akazikwa. Siku ya tatu akafufuka katika wafu. Akapaa mbinguni, amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi. Toka huko atakuja tena kuwahukumu wazima na wafu. Nasadiki kwa Roho Mtakatifu, kanisa takatifu katoliki, ushirika wa watakatifu, maondoleo ya dhambi, ufufuko wa miili na uzima wa milele ijayo. Amina.

AMRI ZA MUNGU.
1. Ndimi Bwana Mungu wako, usiabudu Miungu wengine.
2. Usilitaje bure jina la Mungu wako.
3. Shika kitakatifu siku ya Mungu.
4. Waheshimu Baba na Mama upate miaka mingi na heri duniani.
5. Usiue.
6. Usizini.
7. Usiibe.
8. Usiseme uongo.
9. Usitamani mwanamke asiye mke wako.
10. Usitamani mali ya mtu mwingine.

AMRI ZA KANISA.
1. Hudhuria misa takatifu, dominika na sikukuu zilizoamriwa.
2. Funga siku ya jumatano ya majivu; usile nyama siku ya ijumaa kuu.
3. Ungama dhambi zako walau mara moja kila mwaka.
4. Pokea Ekaristi takatifu hasa wakati wa Paska.
5. Saidia kanisa katoliki kwa zaka.
6. Shika sheria katoliki za ndoa.

SALA YA IMANI.
Mungu wangu, nasadiki maneno yote. Linayosadiki na linayofundisha Kanisa Katoliki la Roma. Kwani ndiwe uliyetufumbulia hayo. Wala hudanganyiki, wala hudanganyi. Amina.

SALA YA MATUMAINI.
Mungu wangu, natumaini kwako, nitapewa kwa njia ya Yesu Kristo. Neema zako hapa duniani, na utukufu mbinguni. Kwani ndiwe uliye agana hayo nasi, nawe mwamini. Amina.

SALA YA MAPENDO.
Mungu wangu, nakupenda zaidi ya chochote. Kwani ndiwe mwema, ndiwe mwenye kupendeza. Nampenda na jirani yangu, kama nafsi yangu, kwa ajili yako. Amina.

SALA YA KUTUBU.
Mungu wangu, nimetubu sana dhambi zangu. Kwani ndiwe mwema, ndiwe nwenye kupendeza. Wachukizwa na dhambi, basi sitaki kukosa tena. Nitafanya kitubio, naomba neema yako, nipate kurudi. Amina.

SALA KWA MALAIKA MLINZI.
Malaika mlinzi wangu, unilinde katika hatari zote, za roho na za mwili. Amina.

MALKIA WA BWANA
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria,naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.
Salama Maria………

Ndimi mtumishi wa Bwana nitendewe ulivyonena.
Salamu Maria………..

Neno la Bwana akatwaa mwili,akakaa kwetu
Salamu Maria……….

Utuombee ee mzazi Mtakatifu wa Mungu,tujalie ahadi za Kristo

Tuombe
Tunakuomba ee Bwana utie neema yako moyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika kwamba mwana amejifanya mtu kwa mateso na msalaba wake utufikishe kwenye utukufu na ufufuko tunaomba hayo kwa njia ya Yesu kristo Bwana wetu.
Amina.

Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu. Amina.

images-7.jpeg

Sala iliyopita: SALA YA KUWAOMBEA MAPADRE

HAPPY-MOMENTS.jpg

Sala inayofuata: Novena ya Noeli

Ujumbe wangu wa leo kwako kuhusu sala

images-24.jpeg
FURAHA-SHINE.jpg

Kama mtu anasali kila siku katika maisha yake hakuna kitu kitakachokuwa kigumu. Sala ni njia ya kujipatia neema za kuendesha maisha yetu. Usiache kusali kila siku hata kama upo katika hali gani.

Hakuna Maisha ya Kikristo bila Kusali. Kama kuna Mkristo anaishi bila kusali huyo siyo Mkristo bali Mkristo mfu. Sala ndiyo uhai wa Mkristo. Hakuna Njia nyingine yoyote ya kumfikia Mungu isipokua sala.

Mungu akujalie udumu daima katika sala

.

.

images-15.jpeg

Tumsifu Yesu Kristu…. Hakuna sala yeyote itolewayo kwa unyenyekevu wa kweli katika imani, matumaini na mapendo inayopita bure mbele ya Mungu. Mungu hamtupi mwenye unyoofu wa moyo.

Jina langu ni Melkisedeck L. Shine. Mimi ni Mkristu Mkatoliki

images-16.jpeg

Karibu Katika Blog yangu ya Kikatoliki mahali pa kusoma makala mbalimbali za Kikatoliki, sala, Tafakari, Picha za Katoliki pamoja na nyimbo za Kikatoliki

images-9.jpeg

Mungu ni rahisi sana kupatikana. Ugumu ni njia ya Kumtafuta Mungu na namna ya kumuishi Mungu. Hapa ndipo watu wengi wanashindwa. Endelea kutembelea Blog hii kila siku tuzidi kutafakari mafumbo ya Mungu.

images-21.jpeg

Chagua unachotaka hapa…
|| MAKALA || TAFAKARI || SALA || MAFUNDISHO || MIUJIZA || WATAKATIFU || NYIMBO || PICHA ||

images-10.jpeg

Usisite kuniandikia maoni,mapendekezo au maswali hapa

Jina
Dini/dhehebu
Mfano Mwislamu, Katoliki, Lutherani, Mlokole n.k
Email
Itatumika kukujibu
Maoni yako
SOKOINE-UNIVERCITY-OF-AGRICULTURE.jpg

Karibu tena na Mungu Akubariki

ABOUT ME | MY PERSONAL BLOG