Sala ya Malaika w Bwana

Blog Kwa Wakatoliki
HOME | MAKALA | TAFAKARI | SALA | MAFUNDISHO | MIUJIZA | WATAKATIFU | NYIMBO | PICHA | MAKTABA/LIBRARY | BIKIRA MARIA | KUHUSU SANAMU | KUHUSU KANISA
Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>
.
Sala ya Malaika w Bwana
Malaika wa Bwana alimpasha habari Maria, naye akapata mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. Salamu Maria,…. Ndimi Mtumishi wa Bwana, nitendewe ulivyonena. Salamu Maria, …… Neno wa Bwana akatwaa Mwili, akakaa kwetu. Salamu Maria, ….. Utuombee, ee Mzazi Mtakatifu wa Mungu, tujaliwe ahadi za Kristo. Tuombe: Tunakuomba ee Bwana, utie neema yako mioyoni mwetu, ili sisi tuliojua kwa maelezo ya Malaika, kwamba, Kristo Mwanao amejifanya mtu: kwa mateso na Msalaba wake, utufikishe kwenye utukufu wa ufufuko. Tunaomba hayo kwa njia ya Kristo Bwana wetu, Amina.
Ujumbe wangu kwako kuhusu sala
Hakuna Maisha ya Kikristo bila Kusali. Kama kuna Mkristo anaishi bila kusali huyo siyo Mkristo bali Mkristo mfu. Sala ndiyo uhai wa Mkristo. Hakuna Njia nyingine yoyote ya kumfikia Mungu isipokua sala.
Sala pasipo Imani thabiti, ya nia ya kweli, upendo wa kweli, unyenyekevu wa ndani na tumaini la kweli katika Amani ya rohoni; Haijakamilika na haifai kitu.
.
.
SALA KWA BIKIRA MARIA
.
.
.
.
.
.
SALA ZA SHUKRANI
.
.
SALA ZA HURUMA, REHEMA, TOBA NA MSAMAHA
.