PN.gif MASOMO YA MISA, OKTOBA 13, JUMAPILI, 2019 DOMINIKA YA 28 YA MWAKA C WA KANISA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Naamani alishuka, akajichovya mara saba katika Yordani, sawasawa na neno lake yule mtu wa Mungu; nayo nyama ya mwili wake ikarudi ikawa kama nyama ya mwili wa mtoto mchanga, akawa safi. Akamrudia yule mtu wa Mungu, yeye na mafuatano yake yote. Akaja, akasimama mbele yake; akasema, Sasa tazama, najua ya kwamba hakuna Mungu duniani mwote, ila katika Israeli; basi nakuomba upokee mbaraka kwa mtumwa wako. Lakini akasema, Kama Bwana aishivyo, ambaye nimesimama mbele yake, sipokei kitu. Akamshurutisha apokee; lakini akakataa. Naamani akasema; Kama sivyo, lakini mtumwa wako na apewe mzigo wa udongo wa baghala wawili; kwa maana mtumwa wako hatatoa tena sadaka ya kuteketezwa wala dhabihu kwa miungu mingine, ila kwa Bwana.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, OCTOBER 12, 2019 JUMAMOSI JUMA LA 27 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Bwana asema hivi: Mataifa na wajihimize, wakapande juu katika bonde la Yehoshafati; maana huko ndiko nitakakoketi niwahukumu mataifa yote yaliyo pande zote. Haya! Utieni mundu, maana mavuno yameiva; njoni, kanyageni; kwa maana shinikizo limejaa, mapipa nayo yanafurika; kwani uovu wao ni mwingi sana.
Makutano makubwa, makutano makubwa, wamo katika bonde la kukata maneno! Kwa maana siku ya Bwana I karibu, katika bonde la kukata maneno.
Jua na mwezi vimetiwa giza, na nyota zimeacha kuangaza. Naye Bwana atanguruma toka Sayuni, atatoa sauti yake toka Yerusalemu; na mbingu nan chi zitatetemeka; lakini Bwana atakuwa kimbilio la watu wake, na ngome ya wana wa Israeli. Hivyo ndivyo mtakavyojua ya kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu, kikaaye Sayuni, mlima wangu mtakatifu; ndipo Yerusalemu utakapokuwa mtakatifu, wala wageni hawatapita tena ndani yake kamwe.
Tena itakuwa siku ile, ya kwamba milima itadondoza divai tamu, na vilima vitatiririka maziwa, na vijito vyote vya Yuda vitatoa maji tele; na chemchemi itatokea katika nyumba ya Bwana, na kulinywesha bonde la Shitimu. Misri itakuwa ukiwa, na Edomu itakuwa jangwa tupu, kwa sababu ya dhuluma waliowatenda wana wa Yuda; kwa sababu wamemwaga damu isiyo na hatia katika nchi yao. Bali Yuda atadumu milele, na Yerusalemu tangu kizazi hata kizazi. Nami nitaitakasa damu yao ambayo sijaitakasa; kwa maana Bwana ndiye akaaye Sayuni.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, OCTOBER 11, 2019, IJUMAA, JUMA LA 27 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njoni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu. Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa Bwana, Mungu wenu, na kumlilia Bwana, Ole wake siku hii!
Kwa maana siku ya Bwana inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; wenyeji wote wa nchi na watetemeke; kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia.
Siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, OCTOBER 10, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 27 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Maneno yenu yamekuwa magumu juu yangu, asema Bwana. Lakini ninyi mwasema, Tumesema maneno juu yako kwa namna gani? Mmesema, Kumtumikia Mungu hakuna faida; na, Tumepata faida gani kwa kuyashika maagizo yake, na kwa kwenda kwa huzuni mbele za Bwana wa majeshi? Na sasa twasema ya kwamba wenye kiburi ndio walio heri; naam, watendao uovu ndio wajengwao; naam, wamjaribuo Mungu ndio waponywao. Ndipo wale waliomcha Bwana waliposemezana wao kwa wao. Naye Bwana akasikiliza, akasikia; na kitabu cha ukumbusho kikaandikwa mbele zake, kwa ajili ya hao waliomcha Bwana, na kulitafakari jina lake. Nao watakuwa wangu, asema Bwana wa majeshi, katika siku ile niifanyayo; naam, watakuwa hazina yangu hasa; nami nitawaachilia, kama vile mtu amwachiliavyo mwanawe mwenyewe amtumikiaye. Ndipo mtakaporudi, nanyi mtapambanua kati ya wenye haki na waovu, na kati yay eye amtumikiaye Mungu nay eye asiyemtumikia.
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi. Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawazukia, lenye kuponya katika mbawa zake.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, OKTOBA 9, 2019 JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Yona alikasirika sana. Akamwomba Bwana, akasema, Nakuomba, Ee Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya. Basi, sasa, Ee Bwana, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Naye Bwana akasema, Je! Unatenda vema kukasirika? Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule utakuwaje. Na Bwana Mungu aliweka tayari mtango, akaufanya ukue juu ya Yona, ili uwe kivuli juu ya kichwa chake, na kumponya katika hali yake mbaya. Basi Yona akafurahi sana kwa sababu ya ule mtango. Lakini siku ya pili kulipopambazuka, Mungu akaweka tayari buu, nalo likautafuna ule mtango, ukakauka.
Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi. Mungu akamwmbaia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili yam tango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa.
Bwana akamwmbia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuutesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tenda wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, OCTOBER 8, 2019 JUMANNE, JUMA LA 27 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Neno la Bwana likamjia Yona mara ya pili, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukaihubiri habari nitakayokuamuru. Basi Yona akaondoka, akaenda Ninawi, kama Bwana alivyonena. Basi Ninawi ulikuwa mji mkubwa mno, ukubwa wake mwendo wa siku tatu. Yona akaanza kuuingia mji mwendo wa siku moja, akapaza sauti yake, akasema, Baada ya siku arobaini Ninawi utaangamizwa.
Basi watu wa Ninawi wakamsadiki, Mungu; wakatangaza kufunga, wakajivika nguo za magunia, tangu yeye aliye mkubwa hata aliye mdogo. Habari ikamfikia mfalme wa Ninawi, naye akaondoka katika kiti chake cha enzi, akavua vazi lake, akajivika nguo za magunia, na kuketi katika majivu. Naye akapiga mbiu, akatangaza habari katika mji wa Ninawi, kwa amri ya mfalme na wakuu wake; kusema, Mwanadamu aisonje kitu, wala mnyama wala makundi ya ngโ€™ombe, wala makundi ya kondoo; wasile, wala wasinywe maji; bali na wafunikwe nguo za magunia, mwanadamu na mnyama pia, nao wakamlilie Mungu kwa nguvu, naam, na wageuke, kila mtu akaache njia yake mbaya, na udhalimu ulio mikononi mwake. Ni nani ajuaye kwamba Mungu hatageuka na kughairi, na kuiacha hasira yake kali, ili tusiangamizwe? Mungu akaona matendo yao, ya kuwa wameiacha njia yao mbaya.
Basi Mungu akalighairi neno lile baya, ambalo alisema atawatenda; asilitende.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA OCTOBER 7, 2019 JUMATATU, JUMA LA 27 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu. Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana. Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.
Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.
Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na tupige kura, tupate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Akawaambia, Mimi ni Mwebrania, nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeviumba bahari nan chi kavu.
Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itutulilie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itawatulilia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata. Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana.
Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda. Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri.
Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku. Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA JUMAPILI, OKTOBA 6, 2019 DOMINIKA YA 27 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Ee Bwana, nilie hata lini, wewe usitake kusikia? Nakulilia kwa sababu ya udhalimu, ila hutaki kuokoa. Mbona wanionyesha uovu, na kunitazamisha ukaidi? Maana uharibifu na udhalimu u mbele yangu; kuna ugomvi, na mashindano yatokea. Bwana akanijibu, akasema, Iandike njozi ukaifanye iwe wazi asana katika vibao, ili aisomaye apate kuisoma kama maji. Maana njozi hii bado ni kwa wakati ulioamriwa, inafanya haraka ili kuufikilia mwisho wake, wala haitasema uongo; ijapokawia; ingojee; kwa kuwa haina bidi kuja, haitakawia. Tazama, roho yake hujivunia, haina unyofu ndani yake; lakini mwenye haki ataishi kwa Imani yake.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA JUMANNE, OCTOBA 1, 2019 JUMA LA 26 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
20Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: โ€œWatu wengi wa mataifa ya kigeni na wakazi wa miji mingi watamiminika mjini Yerusalemu. 21Wakazi wa mji mmoja watawaendea wakazi wa mji mwingine na kuwaambia, โ€˜Twendeni pamoja kumwabudu Mwenyezi-Mungu wa majeshi na kumwomba baraka!โ€™ 22Naam, mataifa yenye nguvu na watu wengi watakuja Yerusalemu kuniabudu mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi na kuniomba baraka. 23Wakati huo, nasema mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi, watu kumi kutoka mataifa ya kila lugha watamng'ang'ania Myahudi mmoja na kushika nguo yake na kumwambia, โ€˜Tunataka kwenda pamoja nanyi, kwa sababu tumesikia kwamba Mungu yu pamoja nanyi.โ€™โ€. find more
PN.gif MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 29, 2019 DOMINIKA YA 26 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Ole wao wanaostarehe katika Sayuni, na hao wanaokaa salama katika mlima wa Samaria; ninyi mnaolala juu ya vitanda vya pembe, na kujinyosha juu ya masemadari yenu; ninyi mnaokula wanakondoo wa kundi, na ndama waliomo zizini; ninyi mnaoimba nyimbo za upuzi mnaokunywa divai katika mabakuli, na kujipaka marhamu iliyo nzuri; lakini hawahuzuniki kwa sababu ya mateso ya Yusufu. Basi kwa ajili ya hayo sasa watakwenda utumwani, na kelele za machezo za hao waliojinyosha zitakoma.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 28, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 25 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Niliinua macho yangu, nikaona, na tazama, mtu mwenye kamba ya kupimia mkononi mwake. Ndipo nikasema, unakwenda wapi? Akaniambia, Ninakwenda kuupima Yerusalemu, nione upana wake ulivyo na urefu wake ulivyo. Na tazama, yule malaika aliyesema nami akasimama karibu, na malaika mwingine akatoka ili kuonana naye; naye akamwambia, Piga mbio, kamwambie kijana huyu, na kusema, Yerusalemu utakaliwa na watu, kama vijiji visivyo na kuta, kwa sababu ya wingi wa watu na mifugo iliyomo ndani yake. Kwa maana mimi, asema Bwana, nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakuwa ukuta wa moto kuuzunguka pande zote, nami nitakaa, kati yako, asema Bwana. Na mataifa mengi watajiunga na Bwana katika siku ile, nao watakuwa watu wangu.. find more
PN.gif Bwana Afya wa Porini
Category ๐Ÿ‘‰methali-na-vitendawili, Tags ๐Ÿ‘‰kitendawili,
JIBU:Fisi. find more
PN.gif Amekufa lakini anasaidia mgonjwa
Category ๐Ÿ‘‰methali-na-vitendawili, Tags ๐Ÿ‘‰kitendawili,
JIBU: mti wa kushikilia mgomba. find more
PN.gif Unanitizama nimekupiga?
Category ๐Ÿ‘‰methali-na-vitendawili, Tags ๐Ÿ‘‰kitendawili,
JIBU: Kujikwaa. find more
PN.gif Namkata lakini hakatiki
Category ๐Ÿ‘‰methali-na-vitendawili, Tags ๐Ÿ‘‰kitendawili,
JIBU: Maji. find more
PN.gif Mwavuli wa nyikani haukingi mvua
Category ๐Ÿ‘‰methali-na-vitendawili, Tags ๐Ÿ‘‰kitendawili,
JIBU: uyoga. find more
PN.gif Anatembea Huku anapika
Category ๐Ÿ‘‰methali-na-vitendawili, Tags ๐Ÿ‘‰kitendawili,
JIBU: muuza kahawa. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 26, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 25 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Katika mwaka wa pili wa Dario mfalme, mwezi wa sita, siku ya kwanza ya mwezi, neno la Bwana lilimjia Zerubabeli, mwana wa Shealtieli, liwali wa Yuda na Yoshua, mwana wa Yeosadaki, kuhani mkuu, kwa kinywa chake Hagai nabii, kusema, Bwana wa majeshi asema hivi, ya kwamba, watu hawa husema, hu sio wakati utupasao kuja, huu sio wakati wa kujengwa nyumba ya Bwana. Ndipo neno la Bwana lilikuja kwa kinywa cha nabii Hagai, kusema, Je! Huu ndio wakati wa ninyi kukaa katika nyumba zenye mapambo ya mbao, iwapo nyumba hii inakaa hali ya kuharibika? Basi sasa. Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Mmepanda mbegu nyingi mkavuna kidogo; mnakula lakini hamshibi; mnakunywa lakini hamkujazwa na vinywaji; mnajivika nguo lakini hapana aonaye moto; nay eye apataye mshahara apata mshahara ili kuutia katika mfuko uliotoboka. Bwana wa majeshi asema hivi, Zitafakarini njia zenu. Pandeni milimani, mkalete miti, mkaijenge nyumba; nami nitaifurahia, nami nitatukuzwa, asema Bwana.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 25, 2019 JUMATANO, JUMA LA 25 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Wakati wa sadaka ya jioni, mimi Ezra niliinuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za Bwana, Mungu wangu; nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni. Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyangโ€™anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo. Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na Bwana, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu. Maana sisi tu watumwa; lakini Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikilizia rehema zake, mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutuburudisha, tuisimamishe nyumba ya Mungu wetu, na kuitengeneza palipobomoka, atupe ukuta katika Yuda na Yerusalemu.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 24, 2019 JUMANNE, JUMA LA 25 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Mfalme Dario alimwandikia liwali wa ngโ€™ambo wa mto, na wenzake; Waacheni liwali wa Wayahudi na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake. Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ngโ€™ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe. Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi. Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa masaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 23, 2019 JUMATATU, JUMA LA 25 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Ilikuwa katika mwaka wa kwanza wa Koreshi, mfalame wa Uajemi, ili kwamba neno la Bwana alilolisema kwa kinywa cha Yeremia lipate kutimizwa, Bwana akamwambia roho yake Koreshi, mfalme wa Uajemi, hata akapiga mbiu katika ufalme wake wote, akaiandika pia akisema,
Koreshi, mfalme wa Uajemi asema hivi: Bwana Mungu wa mbinguni amenipa falme zote za dunia; naye ameniagiza nimjengee nyumba katika Yerusalemu, ulioko Yuda. Basi kila mtu katika ninyi nyote mlio watu wake, Mungu wake na awe pamoja naye, na akwee mpaka Yerusalemu, ulioko Yuda, akaijenge nyumba ya Bwana, Mungu wa Israeli, (yeye ndiye Mungu), iliyoko Yerusalemu. Na mtu awaye yote aliyesalia mahali popote akaapo hali ya ugeni, na asaidiwe na watu wa mahali pake, kwa fedha, na dhahabu, na mali, na wanyama, zaidi ya vitu vitolewavyo kwa hiari ya mtu, kwa ajili ya nyumba ya Mungu, iliyoko Yerusalemu.
Ndipo wakaondoka wakuu wa mbari za mababa, wa Yuda na Benyamini, na makuhani, na Walawi, naam, watu wote ambao Mungu amewaamsha roho zao kukwea, ili kuijenga nyumba ya Bwana, iliyoko Yerusalemu. Na watu wote, waliokaa karibu nao pande zote wakawatia nguvu mikono yao, kwa vyombo vya fedha, kwa dhahabu, kwa mali, na kwa wanyama, na vitu vya thamani, zaidi ya vile vilivyotolewa kwa hiari ya mtu.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 22, 2019 DOMINIKA YA 25 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Lisikieni hili, enyi mnaopenda kuwameza wahitaji, na kuwakomesha maskini wa nchi, mkisema, Mwezi mpya utaondoka lini, tupate kuuza nafaka? Na sabato nayo, tupate kuandika ngano? Mkiipunguza efa na kuiongeza shekel, mkidanganya watu kwa mizani ya udanganyifu, tupate kuwanunua maskini kwa fedha, na wahitaji kwa jozi ya viatu; na kuziuza takataka za ngano. Bwana ameapa kwa fahari ya Yakobo, Hakika sitazisahau kamwe kazi zao hata mojawapo.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 20, 2019 IJUMAA, JUMA LA 24 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Mambo hayo uyafundishe na kuonya. Mtu awaye yote akifundisha elimu nyingine, wala hayakubali maneno yenye uzima ya Bwana wetu Yesu Kristo, wala mafundisho yapatanayo na utauwa, amejivuna; wala hafahamu neno lolote; bali ana wazimu wa kuwazia habari za maswali, na mashindano ya maneno, ambayo katika hayo hutoka husuda, na ugomvi, na matukano, na shuku mbaya; na majadiliano ya watu walioharibika akili zao, walioikosa kweli, huku wakidhani ya kuwa utauwa ni njia ya kupata faida. Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa. Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu; ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.
Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu. Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.
Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, Imani, upendo, saburi, upole. Piga vita vile vizuri vya Imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMATANO, SEPTEMBA 18, 2019 JUMA LA 24 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Nakuandikia hayo, nikitaraji kuja kwako hivi karibu. Lakini nikikawia, upate kujua jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba Mungu, iliyo kanisa la Mungu aliye hai, nguzo na msingi wa kweli. Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu:. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMATATU, SEPTEMBA 16, 2019 JUMA LA 24 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote; kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu. Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu, ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli. Kwa sababu, Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na mwanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu, ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake. Nami kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli. Basi, nataka wanaume wasalishe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMANNE, SEPTEMBA 17, 2019 JUMA LA 24 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Ni neno la kuaminiwa; mtu akitaka kazi ya askofu, atamani kazi njema. Basi imempasa askofu awe mtu asiyelaumika, mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtu wa utaratibu, mkaribishaji, ajuaye kufundisha; si mtu wa kuzoelea ulevi, si mpiga watu; bali awe mpole; si mtu wa kujadiliana, wala asiwe mwenye kupenda fedha; mwenye kuisimamia nyumba yake vema, ajuaye kutiisha watoto katika ustahivu; (yaani, mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje Kanisa la Mungu?) Wala asiwe mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna akaanguka katika hukumu ya Ibilisi. Tena imempasa kushuhudiwa mema na watu walio nje; ili asianguke katika lawama na mtego wa Ibilisi.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 15, 2019 DOMINIKA YA 24 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Bwana alimwambia Musa, Haya! Shuka; kwa maana watu wako uliowatoa katika nchi ya Misri wamejiharibu nafsi zao, wamepotoka upesi kuiacha ile njia niliyowaamuru, wamejifanyizia ndama ya kuyeyusha, wakaiabudu na kuitolea dhabihu, wakasema, Hiyo ndiyo miungu yako, Ee Israeli, iliyokuwa katika nchi ya Misri. Tena Bwana akamwambia Musa, Mimi nimewaona watu hawa, na tazama, ni watu wenye shingo nguvu; basi sasa niache, ili hasira zangu ziwake juu yao, niwaangamize; nami nitakufanya wewe uwe taifa kuu.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, SEPTEMBA 14, 2019 JUMA LA 23 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Siku zile jangwani, watu walimnungโ€™unikia Mungu, na Musa, mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa. Watu wakamwendea Musa, wakasema, tumefanya dambi kwa sababu tumemnungโ€™unukia Mungu, na wewe, utuombee kwa Bwana, atuondolee nyoka hawa. Basi, Musa akawaombea watu. Bwana akawaambia Musa, Jifanyie nyoka ya shaba, ukaiweke juu ya mti, na itakuwa kila mtu aliyeumwa, aitazamapo, ataishi. Musa akafanya nyoka ya shaba, akaiweka juu ya mti, hata ikiwa nyoka amemwuma mtu, alipoitazama ile nyoka ya shaba, akaishi.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 8, 2019 DOMINIKA YA 23 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Ni mtu yupi awezaye kulijua shauri la Mungu? Au ni nani atakayeelewa na mapenzi yake? Kwa kuwa mawazo ya wanadamu yana woga, na makusudi yetu yanaelekea kushindwa; na mwili wenye uharibifu huigandamiza roho, na kiwiliwili cha kidunia huzilemea akili zilizosongwa na masumbuko. Kwa shida tu twayapambanua yaliyoko duniani, na yaliyo karibu nasi ni kazi kuyaona; lakini yaliyoko mbinguni ni nani aliyeyagundua? Naye ni yupi aliyeyavumbua mashauri yako, isipokuwa ulimpa Hekima na kumpelekea Roho yako takatifu kutoka juu? Ndivyo miendo yao wakaao duniani ilivyosafishwa, na wanadamu walivyofundishwa yakupendezayo; hata na kwa Hekima wao wenyewe waliponywa.. find more
PN.gif A MASOMO YA MISA JUMAPILI, SEPTEMBA 1, 2019: DOMINIKA YA 22 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Mwanangu, wakati wa kufanikiwa uendelee katika unyenyekevu; hivyo utapendwa kuliko mwenye ukarimu. Kadiri ulivyo mkuu uzidi kujinyenyekesha, nawe utapata kibali machoni pa Bwana; kwa maana rehema zake Bwana zi kuu, na siri yake ni kwa wanyenyekevu.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA JUMAPILI, AGOSTI 18, 2018 DOMINIKA YA 20 YA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Ndipo wakuu walimwambia mfalme, Twakuomba, mtu huyu auawe, kwa kuwa aidhoofisha mikono ya watu wa vita, waliobaki katika mji huu, na mikono ya watu wote, kwa kuwaambia maneno kama hayo; maana mtu huyu hawatafutii watu hawa heri, bali shari. Naye mfalme Sedekia akasema, Tazama, yu mikononi mwenu; maana mfalme siye awezaye kufanya neno lolote kinyume chenu. Basi wakamtwaa Yeremia, wakamtupa katika shimo la Malkiya, mwana wa mfalme, lililo katika uwanda wa walinzi; wakamshusha kwa kamba. Na mle shimoni hamkuwa na maji, ila matope tu; naye Yeremia akazama katika matope hayo. Ebedmeleki akatoka nyumbani mwa mfalme, akamwambia mfalme, akisema, Ee Bwana wangu, mfalme, watu hawa wametenda mabaya katika mambo yote waliyomtenda Yeremia, nabii, ambaye wamemtupa shimoni; naye hakosi atakufa pale alipo, kwa sababu ya njaa; kwa kuwa hapana mkate kabisa katika mji. Ndipo mfalme akamwamuru Ebedmeleki, Mkushi, akisema, chukua pamoja nawe watu thelathini; toka hapa, ukamtoe Yeremia shimoni, kabla hajafa.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMAPILI, AGOSTI 11, 2019: DOMINIKA YA 19 YA MWAKA C
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Usiku ule baba zetu walitangulia kuonywa, ili wakiwa na ufahamu hakika, wafurahishwe na viapo walivyovitegemea; kwa hiyo watu wako waliutazamia wokovu wa wenye haki na uharibifu wa adui. Madhali uliwalipia kisasi watesi wale, na kwa njia ile ile uliwatukuza ukituita ili tukujie. Zaidi ya hayo watoto watakatifu wa watu wema walitoa dhabihu kwa siri, na kwa moyo mmoja walijitwalia agano la torati ya dini, ya kwamba watashirikiana katika mambo mema na vile vile katika hatari; pindi walipoimbisha nyimbo takatifu za mababu katika kumhimidi Mungu.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMAMOSI, AGOSTI 10, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Apandaye haba atavuna haba; apandaye kwa ukarimu atavuna kwa ukarimu. Kila mtu na atende kama alivyokusudia moyoni mwake, si kwa huzuni, wala si kwa lazima; maana Mungu humpenda yeye atoaye kwa moyo wa ukunjufu. Na Mungu aweza kuwajaza kila neema kwa wingi, ili ninyi, mkiwa na riziki za kila namna sikuzote, mpate kuzidi sana katika kila tendo jema; kama ilivyoandikwa, Ametapanya, amewapa maskini, Haki yake yakaa milele.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, IJUMAA, AGOSTI 9, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Musa aliwaambia makutano: Uliza sasa siku zilizopita, zilizokuwa kabla yako, tangu siku ile Mungu aliyoumba mwanadamu juu ya nchi, na toka pembe hii ya mbingu hata pemhe hii, kwamba kumetukia neno lo lote kama neno hili kubwa, au kwamba kumesikiwa habari ya neno kama hili? Je! watu wakati wo wote wameisikia sauti ya Mungu ikinena toka kati ya moto, kama wewe ulivyosikia, wasife? Au Mungu amekwenda wakati gani akajitwalia taifa toka kati ya taifa lingine, kwa majaribu, na kwa ishara, na kwa maajabu, na kwa vita, na kwa mkono hodari, na kwa mkono ulionyoshwa, na kwa maogofya makuu, kama vile Bwana, Mungu wenu, alivyowatendea ninvi katika Misri, mbele ya macho yenu?. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, ALHAMISI, AGOSTI 8, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia bara ya Sini, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko. Na hapo hapakuwa na maji kwa ule mkutano; wakajikusanya juu ya Musa na juu ya Haruni. Watu wakashindana na Musa, wakanena, wakisema, Ingalikuwa heri kama tungalikufa wakati ule ndugu zetu walipokufa mbele za Bwana! Mbona mmewaleta kusanyiko la Bwana hata jangwa hili ili tufe huku, sisi na wanyama wetu? Na mbona mmetupandisha kutoka Misri ili kutuleta hata mahali hapa pabaya? Si mahali pa mbegu, wala tini, wala mizabibu, wala makomamanga; wala hapana maji ya kunywa. Musa na Haruni wakatoka pale palipokuwa mkutano, wakaenda hata mlangoni pa hema ya kukutania, wakaanguka kifudifudi; utukufu wa Bwana ukawatokea. Bwana akasema na Musa, akinena, Twaa ile fimbo, ukawakusanye mkutano, wewe na Haruni ndugu yako, ukauambie mwamba mbele ya macho yao utoe maji yake, nawe utawatokezea maji katika mwamba, na hivyo utawanywesha maji mkutano na wanyama wao. Musa akaitwaa hiyo fimbo kutoka mbele za Bwana kama alivyomwamuru. Musa na Haruni wakawakusanya kusanyiko mbele ya mwamba, akawaambia, Sikieni sasa, enyi waasi; je! Tuwatokezee maji katika mwamba huu? Musa akainua mkono wake akaupiga ule mwamba kwa fimbo yake mara mbili; maji yakatoka mengi, mkutano wakanywa na wanyama wao pia. Bwana akamwambia Musa na Haruni, Kwa kuwa hamkuniamini mimi, ili kunistahi mbele ya macho ya wana wa Israeli, basi kwa sababu hiyo, hamtawaingiza kusanyiko hili katika ile nchi niliyowapa. Maji haya ni maji ya Meriba; kwa sababu wana wa Israeli waliteta na Bwana, naye alijionyesha kuwa mtakatifu kati yao.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMATANO, AGOSTI 7, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Bwana alinena na Musa, akamwambia, Tuma watu, ili waende wakaipeleleze nchi ya Kanaani, niwapayo wana wa Israeli; katika kila kabila ya baba zao mtamtuma mtu mmoja, kila mtu na awe mkuu kati yao. Wakarejea baada ya kuipeleleza nchi, mwisho wa siku arobaini. Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonyesha matunda ya nchi. Wakamwambia wakasema, Tulifika nchi ile ulivotutuma, na hakika yake, ni nchi yenye wingi wa maziwa na asali, na haya ndiyo matunda yake. Lakini watu wanaokaa katika nchi ile ni hodari, na miji yao ina maboma, nayo ni makubwa sana; na pamoja na havo tuliwaona wana wa Anaki huko. Amaleki anakaa katika nchi ya Negebu; na Mhiti, na Myebusi, na Mwamori wanakaa katika milima, na Mkanaani anakaa karibu na bahari; na kando ya ukingo wa Yordani. Kalebu akawatuliza watu mbele ya Musa, akasema, Na tupande mara, tukaitamalaki; maana twaweza kushinda bila shaka. Bali wale watu waliopanda pamoja naye wakasema, Hatuwezi kupanda tupigane na watu hawa; kwa maana wana nguvu kuliko sisi. Wakawaletea wana wa Israeli habari mbaya ya ile nehi waliyoipeleleza, wakasema, lie nchi tuliyopita kati yake ili kuipeleleza, ni nehi inayowala watu wanaoikaa; na watu wote tuliowaona ndani yake ni watu warefu mno. Kisha, huko tuliwaona Wanefili, wana wa Anaki, waliotoka kwa hao Wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa kama mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi. Mkutano wote wakapaza sauti zao wakalia; watu wakatoka machozi usiku ule. Kisha Bwana akanena na Musa na Haruni, na kuwaambia, Je! nichukuane na mkutano mwovu huu uninungโ€™unikiao hata lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo. Waambieni, Kama niishivyo, asema Bwana, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi; mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi; hao walioninungโ€™unikia. Kwa hesabu ya hizo siku mlizoipeleleza ile nchi, yaani, siku arobaini, kila siku kuhesabiwa mwaka, mtayachukua maovu yenu ndiyo miaka arobaini, nanyi mtakujua kufarikana kwangu. Mimi Bwana nimekwisha nena, hakika yangu ndilo nitakaloutenda mkutano mwovu huu wote, waliokusanyika juu yangu; wmtaangamia katika nyika hii, nako ndiko watakakokufa.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMANNE, AGOSTI 6, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Mimi nilitazama hata viti vya enzi vikawekwa, na mmoja aliye mzee wa siku ameketi; mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji, na nywele za kichwa chake kama sufu safi; kiti chake cha enzi kilikuwa miali ya moto, na gurudumu zake moto uwakao. Mto kama wa moto ukatoka ukapita mbele zake; maelfu elfu wakamtumikia, na elfu kumi mara elfu kumi wakasimama mbele zake; hukumu ikawekwa, na vitabu vikafunuliwa.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMATATU, AGOSTI 5, 2019 JUMA LA 18 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Wana wa Israeli walilia wakasema, Nโ€™nani atakayetupa nyama tule? Twakumbuka samaki tuliokula huko Misri bure; na yale matango, na matikiti, na mboga, na vitunguu, na vitunguu saumu; lakini sasa roho zetu zimekauka; hapana kitu cho chote; hatuna kitu cha kutumaini isipokuwa hi; mana tu.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, AUOSTI 4, 2019 DOMINIKA YA 18 YA MWAKA C
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Mhubiri asema, Ubatili mtupu ubatili mtupu, mambo yote ni ubatili. Maana kuna mtu ambaye kazi yake ni kwa hekima, na kwa maarifa, na kwa ustadi; naye atamwachia mtu asiyeshughulika nayo kuwa sehemu yake. Hayo tena ni ubatili, nayo ni baa kuu. Kwa maana mtu hupata nini kwa kazi yake yote, na kwa juhudi ya moyo wake alivyojitahidi chini ya jua? Kwa kuwa siku zake zote ni masikitiko, na kazi yake ni huzuni; naam, hata usiku moyoni mwake hamna raha. Hayo ni ubatili.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, AGOSTI 3, 2019 JUMAMOSI, JUMA LA 17 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Bwana alinena na Musa katika mlima wa Sinai, na kumwambia: Utajihesabia sabato za miaka, maana, miaka saba mara saba; zitakuwa ni siku za sabato saba za miaka kwenu, maana miaka arobaini na kenda. Ndipo utakapoipeleka pande zote hiyo baragumu yenye sauti kuu, siku ya kumi ya mwezi wa saba; katika siku hiyo ya upatanisho mtaipeleka baragumu katika nchi yenu yote. Na mwaka wa hamsini mtautakasa, na kupiga mbiu ya kuachwa mahuru katika nchi yote kwa watu wote waiketio; itakuwa ni yubile kwenu; nanyi kila mtu atairudia milki yake mwenyewe, nanyi mtarejea kila mtu kwa jamaa yake. Mwaka huo wa hamsini utakuwa ni yubile kwenu; msipande mbegu, wala msivune kitu hicho kimeacho chenyewe, wala msizitunde zabihu za mizabibu isiyopelewa. Kwa kuwa ni yubile; utakuwa mwaka mtakatifu kwenu; mtakula maongeo yake yatokayo shambani.
Mwaka huo wa yubile mtairudia kila mtu milki yake. Tena kama ukimwuzia jirani yako chochote, au kununua chochote mkononi mwa jirani yako, msidanganyane wenyewe kwa wenyewe; kwa hesabu ya miaka iliyo baada ya yubile ndivyo utakavyonunua kwa jirani yako, na kama hesabu ya miaka ya mavuno ndivyo atakavyokuuzia wewe. Kama hesabu ya miaka ilivyo ni nyingi ndivyo utakavyoongeza bei yake, na kama hesabu ya miaka ilivyo ni chache ndivyo utakavyopunguza bei yake; kwani yeye akuuzia mavuno kama hesabu yake ilivyo. Wala msidanganyane; lakini utamcha Mungu wako; kwa kuwa mimi ndimi Bwana, Mungu wenu.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, AGOSTI 2, 2019 IJUMAA, JUMA LA 17 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Bwana akanena na Musa, na kumwambia: Sikukuu za Bwana ni hizi, ni makusanyiko matakatifu, ambayo mtayapigia mbiu kwa nyakati zake.
Mwezi wa kwanza, siku ya kumi na nne ya mwezi wakati wa jioni, ni pasaka ya Bwana. Na siku ya kumi na tano ya mwezi ule ule ni sikukuu kwa Bwana ya mkate usiotiwa chachu; mtaila mikate isiyochachwa muda wa siku saba.
Siku ya kwanza mtakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi. Lakini mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto siku saba; siku ya saba ni kusanyikko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.
Kisha Bwana akanena na Musa, na kumwambia, Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Hapo mtakapokuwa mmekwisha ingia hiyo nchi niwapayo, na kuyavuna mavuno yake, ndipo mtapomletea kuhani mganda wa malimbuko ya mavuno yenu; naye atautikisa mganda mbele za Bwana ili kwamba ukubaliwe kwa ajili yenu; siku ya pili baada ya sabato kuhani atautikisa.
Nanyi mtajihesabia tangu siku ya pili baada ya sabato, tangu siku hiyo mliyouleta mganda wa sadaka ya kutikiswa; zitatimia sabato saba; hata siku ya pili ya hiyo sabatos ya saba mtahesabu siku hamsini; nanyi mtamsongezea Bwana sadaka ya unga mpya.
Lakini siku ya kumi ya mwezi huo wa saba ni siku ya upatanisho; itakuwa kusanyiko takatifu kwenu, nanyi mtazitesa nafsi zenu; nanyi mtasongeza sadaka kwa Bwana kwa njia ya moto.
Nena na wana wa Israeli, uwaambie, Siku ya kumi na tano ya mwezi huo wa saba ni sikukuu ya vibanda muda wa siku saba kwa Bwana.
Siku ya kwanza kutakuwa na kusanyiko takatifu; msifanye kazi yoyote ya utumishi. Mtamsongezea Bwana sadaka kwa moto siku saba; siku ya nane kutakuwa na kusanyiko takatifu kwenu; ni mkutano wa makini huu; msifanye kazi yoyote ya utumishi.
Sikukuu za Bwana ni hizi, ambazo mtazipigia mbiu ya kuwa ni makusanyiko matakatifu, ili mmsongezee Bwana sadaka kwa moto, sadaka ya kuteketezwa, na sadaka ya unga, na dhabihu na sadaka za kinywaji, kila sadaka kwa siku yake.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, AGOSTI 1, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 17 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Musa alifanya hayo yote; kama yote Bwana aliyoagiza ndivyo alivyofanya. Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi, ile maskani ilisimamishwa. Musa akaisimamisha maskani, akayaweka matako yake, akazisimamisha nguzo zake. Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama Bwana alivyomwamuru Musa. Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku, kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama Bwana alivyomwamuru Musa.
Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani. Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa Bwana ukaijaza maskani.
Hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote, bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hata siku ile lilipoinuliwa tena. Kwa maana lile wingu la Bwana lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMATANO, JULAI 31, 2019: JUMA LA 17 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Hata ikawa, Musa aliposhuka katika mlima Sinai, na ztie mbao mbili za ushuhuda zilikuwa mkononi mwa Musa, hapo aliposhuka katika mlima, Musa hakujua ya kuwa ngozi ya uso wake ilingโ€™aa kwa sababu amesema na Bwana. Basi Haruni na wana wote wa Israeli walipomwona Musa, tazama, ngozi ya uso wake ilingโ€™aa; nao wakaogopa kumkaribia. Musa akawaita; Haruni na wakuu wote wa kusanyiko wakarudi kwake; Musa akasema nao.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMANNE JULAI 30, 2019 JUMA LA 17 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Desturi ya Musa, ilikuwa kuitwaa ile hema, na kuikita nje ya marago mbali na hayo marago; akaiita, Hema ya kukutania. Hata kila mtu aliyekuwa akitaka neno kwa Bwana, akatoka, akaenda hata hema ya kukutania, iliyokuwa nje ya marago. Hata Musa alipotoka kuiendea ile hema, watu wote waliondoka wakasimama, kila mtu mlangoni pa hema yake, akamtazama Musa, hata alipokwisha kuingia hemani. Ikawa Musa alipoingia humo hemani, ile nguzo ya wingu ikashuka, ikasimama mlangoni pa ile hema; naye Bwana akasema na Musa. Watu wote wakaiona nguzo ya wingu ikisimama penye mlango wa hema; watu wote wakaondoka wakasujudu, kila mtu mlangoni pa hema yake. Naye Bwana akasema na Musa uso kwa uso. kama vile mtu asemavyo na rafiki yake. Kisha akageuka akarejea hata maragoni; bali mtumish wake Yoshua, mwana wa Nuni, naye ni kijana hakutoka mle hemani. Bwana akashuka ndani ya lile wingu, akasimam; pamoja naye huko, akalitangaza jina la Bwana Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu. Mwenye kusamehe uovu na makosa na dhambi; wala si mwenye kumhesabia mtu mwovu kuwa hana hatia kamwe; mwenye kuwapatiliza watoto uovu wa baba zao, na wana wa wana wao pia, hata kizazi cha tatu na cha nne. Musa akafanya haraka, akainamisha kichwa chake hata nchi, akasujudu. Akasema, Ikiwa sasa nimepata neema mbele zako, Bwana, nakuomba, Bwana, uende kati yetu, maana ni watu wenye shingo ngumu; ukasamehe uovu wetu na dhambi yetu, ukatutwae tuwe urithi wako. Naye alikuwa pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano. hizo amri kumi.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JUMATTU JULAI 29, 2019 JUMA LA 17 LA MWAKA
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Musa aliwaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda. Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ngโ€™ombe.. find more
PN.gif MASOMO YA MISA, JULAI 28 2019: DOMINIKA YA 17 YA MWAKA C
Category ๐Ÿ‘‰masomo-ya-misa, Tags ๐Ÿ‘‰masomo_ya_misa,
Bwana alisema, Kwa kuwa kilio cha Sodoma na Gomora kimezidi. na dhambi zao zimeongezeka sana. basi, nitashuka sasa nione kama wanayotenda ni kiasi cha kilio kilichonijia; na kama sivyo, nitajua. Basi wale watu wakatoka huko wakaelekea Sodoma; lakini Ibrahimu alikuwa akali akisimama mbele za Bwana. Ibrahimu akakaribia, akasema, Je! utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hu- tauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? Hasha, usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha; Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? Bwana akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao. Ibrahimu akajibu, akasema, Basi, nimeshika kusema na Bwana, nami ni mavumbi na majivu tu. Huenda wakapunguka watano katika wale hamsini wenye haki, Je! utaharibu mji wote kwa kupungua watano? Akasema, Sitauharibu, nikiona humo arobaini na watano. Akazidi tena kusema naye, akinena, Huenda wakaonekana humo arobaini? Akasema, Sitafanya kwa ajili ya hao arobaini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema, Huenda wakaonekana huko thelathini? Akasema, Sitafanya, nikiona humo thelathini. Akasema, Tazama, nimeshika kusema na Bwana, huenda wakaonekana huko ishirini? Akasema. Sitaharibu kwa ajili ya hao ishirini. Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu. Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi.. find more
page 1 of 250123...249250next »

Pages pages: 3212485 in total