MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 25, 2019 JUMATANO, JUMA LA 25 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 25, 2019 JUMATANO, JUMA LA 25 LA MWAKA

KUMBUKUMBU YA MT. VINSENTI WA PAULO

SOMO 1

Ezr. 9:5-9

Wakati wa sadaka ya jioni, mimi Ezra niliinuka baada ya kunyenyekea kwangu, nguo yangu na joho yangu zimeraruliwa, nikaanguka magotini nikakunjua mikono yangu mbele za Bwana, Mungu wangu; nikasema, Ee Mungu wangu, nimetahayari, naona haya kuinua uso wangu mbele zako, Mungu wangu; kwa maana maovu yetu ni mengi, hata yamefika juu ya vichwa vyetu, na hatia yetu imeongezeka na kufika mbinguni. Tangu siku za baba zetu tumekuwa na hatia kupita kiasi hata leo; na kwa sababu ya maovu yetu sisi, na wafalme wetu, na makuhani wetu, tumetiwa katika mikono ya wafalme wa nchi hizi, tumepigwa kwa upanga, tumechukuliwa mateka, tumenyang’anywa mali zetu, tumetiwa haya nyuso zetu, kama hivi leo. Na sasa kwa muda kidogo tumeneemeshwa na Bwana, Mungu wetu, hata akatuachia mabaki yaokoke, akatupa msumari katika mahali pake patakatifu. Mungu wetu atutie nuru machoni mwetu, tuburudike kidogo katika kufungwa kwetu. Maana sisi tu watumwa; lakini Mungu wetu hakutuacha katika utumwa wetu, bali ametufikilizia rehema zake, mbele ya wafalme wa Uajemi, ili kutuburudisha, tuisimamishe nyumba ya Mungu wetu, na kuitengeneza palipobomoka, atupe ukuta katika Yuda na Yerusalemu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Tob. 13:2-4, 6 (K) 1

(K) Amehimidiwa Mungu aishiye milele.

Kwa maana hurudi, na kurehemu tena;
Hushusha hata kuzimu, na kuinua tena;
Wala hakuna awezaye kujiepusha na mkono wake. (K)

Enyi bani Israeli, mshukuruni mbele ya mataifa
Yeye ambaye ametutawanya katikati yao. (K)

Kuko huko utangazeni ukuu wake,
Mwadhimisheni mbele ya wote walio hai;
Kwa kuwa Yeye ndiye Bwana wetu,
Naye Mungu yu Baba wetu,
Naye Mungu yu Baba yetu milele. (K)

SHANGILIO

Aleluya, aleluya,
Ee Mungu, tunakusifu, tunakukiri kuwa Bwana. Jamii tukufu ya Mitume inakusifu.
Aleluya.

INJILI

Lk. 9:1-6

Yesu aliwaita wale Thenashara, akawapa uwezo na mamlaka juu ya pepo wote na kuponya maradhi. Akawatuma wautangaze ufalme wa Mungu, na kupoza wagonjwa. Akawaambia, Msichukue kitu kwa safari yenu, fimbo, wala mkoba, wala mkate, wala fedha, wala mmoja wenu asiwe na kanzu mbili. Na nyumba yoyote mtakayoingia kaeni humo, tokeni humo. Na wale wasiowakaribisha, mtokakpo katika mji huo yakung’uteni hata mavumbi ya miguuni mwenu, kuwa ushuhuda juu yao. Wakaenda, wakazunguka katika vijiji, wakihubiri Injili, na kupoza watu kila mahali.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10).. soma zaidi

a.gif Katika amri ya kwanza ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa kumdharau Mungu na kuweka imani yetu katika viumbe badala ya Mungu… soma zaidi

a.gif Dhambi ya mauti ni nini?

Dhambi ya Mauti ni kosa la kuvunja Amri ya Mungu au ya Kanisa, katika jambo kubwa, kwa fahamu na kusudi. (1 Yoh 5:16).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 25, 2019 JUMATANO, JUMA LA 25 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 25, 2019 JUMATANO, JUMA LA 25 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Nimeonja pendo lako

[Tafakari ya Sasa] 👉Mnyororo wa Baraka za Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Anna

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

KADI-SALAMU-JIONI-MZAZI.JPG

a.gif Fadhila inayoondoa uvivu ni ipi?

Fadhila inayoondoa uvivu ni utendaji.. soma zaidi

a.gif Je, wanawake wanaweza kupewa daraja?, Mwanamke anaweza kuwa padri?

Hapana, wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua wanaume tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa Maria, mtakatifu kuliko wote… soma zaidi

a.gif Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na nani?

Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na Yesu, kama sakramenti zote. Maandiko yanasimulia huruma yake iliyomfanya awaponye wengi kwa namna mbalimbali na kuwapa Mitume uwezo wa kufanya vilevile kwa “kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina” (Math 10:1). Nao

“wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza” (Mk 6:13)… soma zaidi

a.gif Ni kwa nini Sadaka ya Misa Takatifu ni Sadaka ile ile ya Msalaba?

Sadaka ya Misa Takatifu ni ile ile ya Msalaba kwa sababu ni sadaka moja tu, kuhani na kafara ni yule yule… soma zaidi

a.gif Yesu aliweka sadaka ya Misa Takatifu kwa makusudi gani?

Yesu aliweka sadaka ya Misa Takatifu ili;.. soma zaidi

a.gif Bikira Maria Katika dini ya Kiislamu

Kurani inamtaja mwanamke mmoja tu, tena mara 34: ni Mariamu, mama wa nabii Isa. Akichanganywa na dada wa Haruni na Musa, aliyekuwa na jina hilohilo, anatajwa kama binti Imrani. Pia habari nyingine kadhaa zinapishana na zile za Injili… soma zaidi

a.gif Ujumbe wa leo

*UJUMBE WA LEO*
Ndege anapokuwa hai huwa anakula sana funza, lakini atakapokufa nae huliwa na funza.. Maisha yanabadilika kila wakati, usimdharau wala kumuumiza mtu yeyote katika maisha…Unaweza ukawa imara sana leo lakini kumbuka maisha ni imara kuliko wewe.., Mti mmoja unaweza ukatengeneza mamilioni ya njiti za kiberiti, lakini muda ukifika njiti moja tu ya kiberiti inaweza ikachoma msitu mzima….. soma zaidi

a.gif Je, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi?

Ndiyo, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi tulizotenda baada ya ubatizo, kwa kuwa hatuwezi kupokea msamaha tukikataa masharti yake, na Mungu ametupangia watu ambao watuondolee kwa niaba yake… soma zaidi

a.gif Nani analazima kuhudhuria Misa Takatifu, Dominika na Sikukuu zilizoamriwa?

Kila Mkatoliki aliyetimiza umri wa Miaka saba na kuendelea ana lazima kuhudhuria Misa Takatifu, Dominika na Sikukuu zilizoamriwa… soma zaidi

a.gif Tuwaheshimu Baba na Mama kwa matendo gani?

Tuwaheshimu Baba na Mama kwa matendo ya adabu, heshima, utii na mapendo (Ayu 3:12).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.