MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 24, 2019 JUMANNE, JUMA LA 25 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 24, 2019 JUMANNE, JUMA LA 25 LA MWAKA

SOMO 1

Ezr. 6:7-8, 12, 14-20

Mfalme Dario alimwandikia liwali wa ng’ambo wa mto, na wenzake; Waacheni liwali wa Wayahudi na wazee wa Wayahudi, waijenge nyumba hii ya Mungu mahali pake. Tena, natoa amri kuwaagiza ninyi mtakayowatendea wazee hao wa Wayahudi kwa kazi hii ya kuijenga nyumba ya Mungu; katika mali ya mfalme, yaani, katika kodi za nchi iliyo ng’ambo ya Mto, watu hao wapewe gharama zote kwa bidii, ili wasizuiliwe. Na Mungu huyu, aliyelifanya jina lake likae pale, na aangamize wafalme wote, na watu wote, watakonyosha mikono yao kulibadili neno hili, na kuiharibu nyumba hii ya Mungu, iliyoko Yerusalemu. Mimi, Dario, nimetoa amri; na ifanyike kwa bidii nyingi. Nao wazee wa Wayahudi wakajenga, wakafanikiwa, kwa masaada wa kuhubiri kwao Hagai nabii, na Zekaria mwana wa Ido.

Wakajenga, wakaimaliza kazi yao, kwa maagizo ya Mungu wa Israeli, na kwa amri ya Koreshi, na Dario, na Artashasta mfalme wa Uajemi. Nyumba hiyo ikamalizika siku ya tatu ya mwezi Adari, katika mwaka wa sita wa kutawala kwake mfalme Dario. Na wana wa Israeli, na makuhani, na walawi na watu wengine katika hao waliohamishwa, wakaiweka wakfru nyumba ya Mungu kwa furaha. Na katika kuiweka wakfu nyumba ya Mungu, wakatoa sadaka, ng’ombe mia, na kondoo waume mia mbili, na wanakondoo mia nne; tena wakatoa mbuzi waume kumi na wawili, kuwa sadaka ya dhambi kwa ajili ya Israeli wote, kwa hesabu ya kabila za Israeli. Wakawaweka makuhani katika kura zao, wakawaweka na Walawi vilivyoandikwa katika chuo cha Musa. Kisha, wana wa uhamisho wakaifanya Pasaka, mwezi wa kwanza, siku ya kumi nan ne ya mwezi. Kwa maana makuhani na Walawi walikuwa wamejitakasa wote pamoja; wote walikuwa hali ya tohara; wakachinja pasaka kwa ajili ya wana wote wa uhamisho, na kwa ajili ya ndugu zao makuhani, na kwa ajili ya nafsi zao.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 122:1-5 (K) 1

(K) Nalifurahi waliponiambia, na twende nyumbani kwa Bwana.

Nalifurahi waliponiambia,
Na twende nyumbani kwa Bwana. (K)

Miguu yetu imesimama
Ndani ya malango yako, ee Yerusalemu!
Ee Yerusalemu uliyejengwa
Kama mji ulioshikamana. (K)

Huko ndiko walikopanda kabila,
Kabila za Bwana;
Ushuhuda wa Israeli,
Walishukuru jina la Bwana.
Maana huko viliwekwa viti vya hukumu,
Viti vya enzi vya mbari ya Daudi. (K)

SHANGILIO

1Pet. 1:25

Aleluya, aleluya,
Neno la Bwana hudumu hata milele, na neno hilo ni neno lile jema lililohubiriwa kwenu.
Aleluya.

INJILI

Lk. 8:19 – 21

Walimwendea Yesu mama yake na ndugu zake, wasiweze kumkaribia kwa sababu ya mkutano. Akaletewa habari akiambiwa, Mama yako na ndugu zako wamesimama nje wakitaka kuonana nawe. Akawajibu akasema, Mama yangu na ndugu zangu ndio hao walisikiao neno la Mungu na kulifanya.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Je, Mungu amejitambulisha pia kwa jina?

Ndiyo, Mungu amejitambulisha pia kwa majina mbalimbali. Katika Agano la Kale jina muhimu kuliko yote liliandikwa “YHWH” yaani, “Mimi Ndimi”. Tangu zamani Wayahudi hawalitamki, hivyo wakilifikia wanasoma kwa kutafsiri, “Bwana”… soma zaidi

a.gif Ni fadhila gani inayoondoa majivuno?

Fadhila inayoondoa majivuno ni fadhila ya Unyenyekevu.. soma zaidi

a.gif Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?

Ndiyo, nilazima kwa wokovu kwa wale ambao wametangaziwa injili na wanasifa ya kuomba Sakramenti hiyo.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 24, 2019 JUMANNE, JUMA LA 25 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 24, 2019 JUMANNE, JUMA LA 25 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala kwa Malaika Mlinzi

[Tafakari ya Sasa] 👉Siri ya Imani kwa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu John Bosco

UJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Abramu Katika Nchi ya Misri

10 Basi kulikuwa njaa katika nchi ile; Abramu akashuka Misri, akae huko kwa muda maana njaa ilikuwa nzito katika nchi… soma zaidi

a.gif Mungu wako wangapi?

Mungu yupo mmoja tuu Mkubwa wa wote na Baba wa wote. (Is: 44:6).. soma zaidi

a.gif MPANGILIO WA KURASA ZA POSTI NA MAKALA

Makala kuu za Wakatoliki;.. soma zaidi

a.gif Jifunze kitu kupitia mkasa huu wa kusisimua

Kulikua na bwana👤mmoja masikini sana😳😳Kutokana na dhiki kumwandama ilifikia wakati alitamani kufa😮kuliko kuendelea kuishi sehemu alipokuwa anaishi kulikuwa na
msitu🌵🌱🌿🌴🌲mkubwa ambao ndani yake linaishi zimwi👹👹👹lenye kula watu na katika msitu huo hajawahi kuingia binadamu👴 akarudi salama✌wote waliliwa na zimwi👹👹.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ni nini?

Sakramenti ni ishara wazi ionekanayo ya neema isiyoonekana, iliyofanyizwa kwanza na Yesu Kristu mwenyewe; ilete neema au izidishe neema moyoni mwetu… soma zaidi

a.gif Chagua kunyamaza: Huu ni ushauri kwa Leo

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza… soma zaidi

a.gif Uzima wa milele

Maswali na majibu kuhusu uzima wa milele;.. soma zaidi

a.gif Mwenyezi Mungu yukoje basi?

Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote… soma zaidi

a.gif Kwa kusudi gani Yesu alianzisha Kanisa?

Yesu alianzisha Kanisa kwa nia ya Kuutangaza na kuueneza Ufalme wa Mungu (Mt 28:19-20).. soma zaidi

a.gif Zawadi ya Kipekee kwa mtu

Kuna Zawadi moja ya Kipekee ya kumpa mtu ambayo ni.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.