MASOMO YA MISA, OKTOBA 9, 2019 JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, OKTOBA 9, 2019 JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA

SOMO 1

Yon. 4:1-11

Yona alikasirika sana. Akamwomba Bwana, akasema, Nakuomba, Ee Bwana; sivyo hivyo nilivyosema, hapo nilipokuwa katika nchi yangu? Hii ndiyo sababu nalifanya haraka kukimbilia Tarshishi; kwa maana nalijua ya kuwa wewe u Mungu mwenye neema, umejaa huruma, si mwepesi wa hasira, u mwingi wa rehema, nawe waghairi mabaya. Basi, sasa, Ee Bwana, nakuomba, uniondolee uhai wangu; maana ni afadhali nife mimi kuliko kuishi.
Naye Bwana akasema, Je! Unatenda vema kukasirika? Ndipo Yona akatoka mjini, akaketi upande wa mashariki wa mji, akajifanyia kibanda huko, akakaa chini yake uvulini, hata aone mji ule utakuwaje. Na Bwana Mungu aliweka tayari mtango, akaufanya ukue juu ya Yona, ili uwe kivuli juu ya kichwa chake, na kumponya katika hali yake mbaya. Basi Yona akafurahi sana kwa sababu ya ule mtango. Lakini siku ya pili kulipopambazuka, Mungu akaweka tayari buu, nalo likautafuna ule mtango, ukakauka.
Basi ikawa, jua lilipopanda juu, Mungu akaweka tayari upepo wa mashariki, wenye hari nyingi; jua likampiga Yona kichwani, hata akazimia, naye akajitakia kufa akajitakia kufa, akasema, Ni afadhali nife mimi kuliko kuishi. Mungu akamwmbaia Yona, Je! Unatenda vema kukasirika kwa ajili yam tango? Naye akasema, Ndiyo, natenda vema kukasirika hata kufa.
Bwana akamwmbia, Wewe umeuhurumia mtango, ambao hukuufanyia kazi, wala kuutesha; uliomea katika usiku mmoja, na kuangamia katika usiku mmoja; na mimi, je! Haikunipasa kuuhurumia Ninawi, mji ule mkubwa; ambao ndani yake wamo watu zaidi ya mia na ishirini elfu, wasioweza kupambanua katika mkono wao wa kulia na mkono wao wa kushoto; tenda wamo wanyama wa kufugwa wengi sana?

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 86:3-6, 9-10 (K) 15

(K) Wewe Bwana, u Mungu wa rehema na neema.

Wewe, Bwana, unifadhili,
Maana nakulilia Wewe mchana kutwa.
Uifurahishe nafsi ya mtumishi wako,
Maana nafsi yangu nakuinulia Wewe, Bwana. (K)

Kwa maana Wewe, Bwana, U mwema,
Umekuwa tayari kusamehe.
Na mwingi wa fadhili,
Kwa watu wote wakuitao.
Ee Bwana, uyasikie maombi yangu;
Uisikilize sauti ya dua zangu. (K)

Mataifa yote uliwafanya watakuja;
Watakusujudia Wewe, Bwana.
Watalitukuza jina lako;
Kwa kuwa ndiwe uliye mkuu.
Wewe ndiwe mfanya miujiza,
Ndiwe Mungu peke yako. (K)

SHANGILIO

Ebr. 4:12

Aleluya, aleluya,
Neno la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.

INJILI

Lk. 11:1 – 4

Yesu alipokuwa mahali fulani akiomba, alipokwisha, mmoja katika wanafunzi wake alimwambia, Bwana, tufundishe sisi kusali, kama vile Yohane alivyowafundisha wanafunzi wake. Akawaambia, Msalipo, semeni: Baba, Jina lako litakaswe, Ufalme wako uje, Utupe siku kwa siku riziki yetu. Utusamehe dhambi zetu, kwa kuwa sisi nasi tunamsamehe kila tumwiaye. Na usitutie majaribuni.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Aliyevumbua utaratibu wa kuweka mistari na sura katika Biblia

Je, WAJUA?
Aliyevumbua utaratibu wa kuweka SURA na MISTARI katika BIBLIA.
Ni kasisi (Padri) Mwingereza,.. soma zaidi

a.gif Ukweli kuhusu tofauti na usawa wa X-MASS na CHRISTMAS

Na Fr. Titus Amigu
Lakini kwa leo nina jambo moja la kuweka sawa. Vijana kadhaa wameniomba nitoe maelezo kuhusiana na maneno “CHRISTMAS” na “X-MAS” maana wanachanganywa na wenzao. Kifupi, maelezo yanayosambazwa kwenye mitandao yetu ni kwamba “Christmas” ni sahihi na “X-mas” siyo sahihi. Maelezo haya yanayosambazwa si sahihi, ni ya uongo… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Kipaimara inaleta manufaa gani rohoni mwa Mbatizwa?

Manufaa ya Kipaimara ni;.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, OKTOBA 9, 2019 JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, OKTOBA 9, 2019 JUMATANO, JUMA LA 27 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Kuomba na Kushukuru

KADI-MZAZI-ASUBUHI.JPG

a.gif Kuumbwa kwa Dunia

Mungu aliumba Dunia kwa siku sita hatua kwa hatua kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Maana ya MAPOKEO kwenye Kanisa Katoliki

Maswali na Majibu kuhusu Mapokeo;.. soma zaidi

a.gif Ajabu la ukombozi wa Yesu ni nini?

Ajabu la ukombozi wa namna hiyo ni kwamba, “tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake” (Rom 5:10)… soma zaidi

a.gif Kampeni ya kutetea wajane

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni hii ni kuhamasisha watu wote kusaidia na kutetea wajane kwenye mahitaji yao ya kimwili, kiroho na kijamii hasa wale wasioweza kusimama wenyewe baada ya kuondokewa wenzi wao.
Wajane wote wanahitaji msaada hasa kipindi cha mwanzo cha ujane. Kuna wanaohitaji msaada wa kiuchumi na faraja na kuna ambao wapo vizuri kiuchumi wanahitaji msaada wa kifaraja tuu… soma zaidi

a.gif Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?

Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo.. soma zaidi

a.gif Aliyevumbua utaratibu wa kuweka mistari na sura katika Biblia

Je, WAJUA?
Aliyevumbua utaratibu wa kuweka SURA na MISTARI katika BIBLIA.
Ni kasisi (Padri) Mwingereza,.. soma zaidi

a.gif Sifa kuu za Kanisa ni zipi na zinapatikana wapi?

Sifa kuu za Kanisa ni kuwa moja, takatifu, katoliki na la Mitume. Sifa hizo zinalitambulisha kati ya madhehebu mengi Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu kumpitia Mtume aliyembadilishia jina aitwe Petro, yaani Mwamba wa Kanisa lake lisilokoma wala kupotoka kamwe:.. soma zaidi

a.gif Kisa cha Noa na Wanawe

18 Wana wa Nuhu waliotoka katika safina, ni Shemu, na Hamu, na Yafethi; na Hamu ndiye baba wa Kanaani… soma zaidi

a.gif Je, tunaweza kuhakikisha neema ya utakaso?

Hapana, hatuwezi kuhakikisha neema ya utakaso kwa kuwa ni tukio ambalo linapita maumbile na kufanyika rohoni, hivyo halifikiwi na hisi zetu. Pengine Mungu anatokeza dalili fulani za badiliko hilo kama vile furaha ya ndani au karama ya nje, lakini hizo hazihitajiki wala hazitoshi kuthibitishia mtu amepata neema hiyo… soma zaidi

a.gif Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, mbona katika viumbe vyake kuna ubaya? Kwa nini Mungu anaruhusu mabaya na maovu?

Mungu akiwa wema mkuu na mwenye uwezo wote, hakuumba ubaya wowote. Tena kila anapovumilia ule uliosababishwa na viumbe vyenye hiari anaufanya uzae mema makubwa zaidi kwa njia tusizoweza kuzifahamu vizuri hapa duniani… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.