MASOMO YA MISA OKTOBA 25, 2019 IJUMAA, JUMA LA 29 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA OKTOBA 25, 2019 IJUMAA, JUMA LA 29 LA MWAKA

SOMO 1

Rum. 7:18-25

Najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu.
Basi, nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani; lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu.
Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
_

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 119:66,76-77,93-94 (K) 68

(K) Unifundishe akili na maarifa, Ee Bwana.

Unifundishe akili na maarifa,
Maana nimeyaamini maagizo yako.
Weew U mwema na mtenda mema,
Unifundishe amri zako. (K)

Nakuomba, fadhili zako ziwe faraja kwangu,
Sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
Rehema sheria yako ni furaha yangu. (K)

Hata milele sitayasahau maagizo yako,
Maana kwa hayo umenihuisha.
Mimi ni wako, uniokoe,
Kwa maana nimejifunza mausia yako. (K)
_

SHANGILIO

2 Kor. 5:19

Aleluya, aleluya,
Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, ametia ndani yetu neno la upatanisho.
Aleluya.
_

INJILI

Lk. 12:54-59

Yesu aliwaambia makutano pia, kila mwonapo wingu likizuka pande za magharibi mara husema, Mvua inakuja; ikawa hivyo. Na kila ivumapo kaskazi, husema, Kutakuwa na joto; na ndivyo ilivyo. Enyi wanafiki, mwajua kuutambua uso wan chi na mbingu; imekuwaje, basi, kuwa hamjui kutambua majira haya?
Na mbona ninyi wenyewe kwa nafsi zenu hamwamui yaliyo haki? Maana, unapofuatana na mshitaki wako kwenda kwa mwamuzi, hapo njiani fanya bidi kupatanishwa naye, asije akakuburuta mpaka mbele ya kadhi; yule kadhi akakutia mikononi mwake mwenye kulipiza, na yule mwenye kulipiza akakutupa gerezani. Nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo katika dunia ya leo

1- Ishi Kwa Kufuata Mfano Wa Mwokozi Yesu Kristo
Kwa Kuishika Amri Yake Kuu Ambayo ni Upendo. Mpende Bwana MUNGU wako kwa Moyo wako Wote, Mwili na Nafsi yako yote.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Utatu Mtakatifu

Haya hapa Maswali na majibu kuhusu Utatu Mtakatifu;.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Neema na Rehema

Mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu Neema na Rehema.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA OKTOBA 25, 2019 IJUMAA, JUMA LA 29 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA OKTOBA 25, 2019 IJUMAA, JUMA LA 29 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala kwa Malaika Mlinzi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Salamu Salamu Malkia

[Tafakari ya Sasa] 👉Mawazo ya Mungu tunapokua na shida na mateso

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Ambrosi

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

a.gif Utafuteje dhambi wakati wa kujiandaa kuungama?

Tafuta dhambi kwa njia hizi.. soma zaidi

a.gif Baada ya Mitume kufa ni nani wanafanya Sakramenti ya Ekaristi

Badaa ya Mitume kufa Maaskofu na Mapadri wanaendelea kuadhimisha Sakramenti ya Ekaristi Takatifu.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Uaminifu

Uaminifu ni kipimo na kigezo cha Ukamilifu na Utakatifu… soma zaidi

a.gif Kwa sababu gani yatupasa kuwaheshimu Baba na Mama?

Yatupasa kuwaheshimu Baba na Mama kwa sababu;.. soma zaidi

a.gif Je, ekaristi ni kafara (sadaka)?

Ndiyo, ekaristi ni kafara ambayo Yesu alimtolea Baba msalabani na anaendelea kumtolea kwa wokovu wetu… soma zaidi

a.gif Tabernakulo ni nini?

Tabernakulo ni mahali Patakatifu anapokaa Yesu wa Ekaristi siku zote.. soma zaidi

a.gif Tuchukue tahadhari gani tunapotumia visakramenti?

Tunapotumia Visakramenti tuchukue tahadhari hizi.. soma zaidi

a.gif Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni vipi?

Kati ya vitabu vya Biblia, vilivyo bora ni Injili 4 zilizoandikwa na Mathayo, Marko, Luka na Yohane… soma zaidi

a.gif Abramu na Loti Watengana

1 Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini… soma zaidi

a.gif Je, mwili wetu ni muhimu?

Ndiyo, mwili wetu ni muhimu, kwa sababu umeumbwa na Mungu, umetwaliwa na Mwanae ili atuokoe, umehuishwa na Roho Mtakatifu atakayeutukuza siku ya ufufuo kwa mfano wa Yesu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.