MASOMO YA MISA OKTOBA 21, 2019 JUMATATU, JUMA LA 29 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA OKTOBA 21, 2019 JUMATATU, JUMA LA 29 LA MWAKA

SOMO 1

Rum. 4: 20-25

Ibrahimu akiiona ahadi ya Mungu hakusita kwa kutokuamini, bali alitiwa nguvu kwa Imani, akimtukuza Mungu; huku akijua hakika ya kuwa Mungu aweza kufanya yale aliyoadhidi. Kwa hiyo ilihesabiwa kwake kuwa ni haki. Walakini haikuandikwa kwa ajili yake tu kwamba ilihesabiwa kwake; bali na kwa ajili yetu sisi tuatakaohesabiwa vivyo hivyo, sisi tunaomwamini yeye aliyemfufua Yesu Bwana wetu katika wafu; ambaye alitolewa kwa ajili ya makossa yetu, na kufufuliwa ili tupate kuhesabiwa haki.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Lk. 1:69-75 (K)

(K) Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli.

Ametusimamishia pembe ya wokovu.
Katika mlango wa Daudi, mtumishi wake.
Kama alivyosema tangu mwanzo
Kwa kinywa cha manabii wake watakatifu. (K)

Tuokolewe na adui zetu,
Na mikononi mwao wote wanaotuchukia;
Ili kuwatendea rehema baba zetu,
Na kulikumbuka agano lake takatifu. (K)

Uapo aliomwapia Ibrahimu, baba yetu,
Ya kwamba atatujalia sisi,
Tuokoke mikononi mwa adui zetu,
Na kumwabudu pasipo hofu,
Kwa utakatifu na kwa haki,
Mbele zake siku zetu zote. (K)

SHANGILIO

Lk. 8:15

Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.

INJILI

Lk. 12;13-21

Mtu mmoja katika mkutano alimwambia Yesu, Mwalimu, mwambie ndugu yangu anigawie urithi wetu. Akamwambia, Mtu wewe, ni nani aliyeniweka mimi kuwa mwamuzi au mgawanyi juu yenu? Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo.
Akawaambia mithali, akisema, Shamba la mtu mmoja tajiri lilikuwa limezaa sana; akaanza kuwaza moyoni mwake, akisema, Nifanyeje? Maana sina pa kuyaweka akiba mavuno yangu. Akasema, Nitafanya hivi; nitazivunja ghala zangu, nijenge nyingine kubwa zaidi, na humo nitaweka nafaka yangu yote na vitu vyangu. Kisha, nitajiambia, Ee nafsi yangu, una vitu vyema vingi ulivyojiwekea akiba kwa miaka mingi; pumzika basi, ule, unywe, ufurahi. Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani? Ndivyo alivyo mtu ajiwekeaye nafsi yake akiba, asijitajirishe kwa Mungu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Tumekatazwa nini ili tulinde usafi wa moyo?

Tumekatazwa haya;.. soma zaidi

a.gif Kanisa limepewa na Yesu muundo gani?

Kanisa limepewa na Yesu wahudumu wenye daraja takatifu wanaoitwa makleri; waamini wengine wanaitwa walei. Kutoka pande hizo mbili wanapatikana watawa waliowekwa wakfu kwa namna ya pekee kwa kushika mashauri ya Kiinjili… soma zaidi

a.gif Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na nani?

Mpako wa Wagonjwa ulianzishwa na Yesu, kama sakramenti zote. Maandiko yanasimulia huruma yake iliyomfanya awaponye wengi kwa namna mbalimbali na kuwapa Mitume uwezo wa kufanya vilevile kwa “kupoza magonjwa yote na udhaifu wa kila aina” (Math 10:1). Nao

“wakatoa pepo wengi, wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa, wakawapoza” (Mk 6:13)… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA OKTOBA 21, 2019 JUMATATU, JUMA LA 29 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA OKTOBA 21, 2019 JUMATATU, JUMA LA 29 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉LITANIA YA BIKIRA MARIA

[Tafakari ya Sasa] 👉Uwe na maono

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Aloisi Gonzaga

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

a.gif Je, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu?

Ndiyo, kazi zote za Roho Mtakatifu zinahusiana na Yesu na kulenga hasa kuandaa watu wampokee, wamfuate na kumshuhudia katika umoja wa kundi lake, Kanisa… soma zaidi

a.gif Mambo manne ya mwisho katika maisha

Mambo manne ambayo ni ya mwisho katika maisha ni;.. soma zaidi

a.gif Tunapaswa kusadiki hasa nini?

Tunapaswa kusadiki hasa Utatu wa Mungu pekee, kwamba ni Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Milele yote Baba kwa jinsi alivyo ndani mwake anamzaa Mwana na kumvuvia Roho Mtakatifu, kama vile jua linavyotoa mwanga na joto lisitenganike navyo… soma zaidi

a.gif Makala mpya kwa sasa

Makala Mpya ni kama ifuatavyo,.. soma zaidi

a.gif Je, Yesu alirudia maisha ya duniani?

Hapana, Yesu hakurudia maisha ya duniani: tofauti na watu aliowafufua warudie maisha haya, Yesu mfufuka ameshaingia utukufu wa milele:.. soma zaidi

a.gif Jinsi ya kuishi maisha ya Kikristo katika dunia ya leo

1- Ishi Kwa Kufuata Mfano Wa Mwokozi Yesu Kristo
Kwa Kuishika Amri Yake Kuu Ambayo ni Upendo. Mpende Bwana MUNGU wako kwa Moyo wako Wote, Mwili na Nafsi yako yote.. soma zaidi

a.gif MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA

Sisi Wakatoliki nyakati hizi zilizojaa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayotumia Biblia na kuitafsiri kadiri ya
imani yao ama wenyewe wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya
kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu,
tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu
wote pamoja na Yohane Mbatizaji, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27). Hivyo yale yote
tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia kwa
hiari fumbo la mpango wake… soma zaidi

a.gif Majaribu na Aina zake

Majaribu ni nini?
-Majaribu ni kushawishi kutenda kinyume na mapenzi ya MUNGU
-Ni kipimo kwa mtu yaani yuko imara na anafaa?
‘’Heri mtu anastahimilie majaribu kwa sababu akiisha kukubariwa ataipokea taji ya uzima BWANA aliowaahidi wampendao {1 petro 6;7}.. soma zaidi

a.gif MTAKATIFU VICENT WA RELENI

Maisha ya Mtakatifu Vicent wa Releni kwa ufupi;.. soma zaidi

a.gif Ili Askofu atoe ruhusa ya kufungisha ndoa ya mchanganyiko au dini tofauti kuna Masharti gani?

Ndiyo, Askofu atatoa ruhusa baada ya Mkristo Mkatoliki kuahidi kwamba;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.