MASOMO YA MISA, OKTOBA 18, 2019 IJUMAA JUMA LA 28 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA, OKTOBA 18, 2019 IJUMAA JUMA LA 28 LA MWAKA

SIKUKUU YA MT. LUKA, MWINJILI

SOMO 1

2Tim. 4:10 – 17

Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu huu wa sasa, akasafiri kwenda Thesalonike; Kreske amekwenda Galatia; Tito amekwenda Dalmatia. Luka peke yake yupo hapa pamoja nami. Umtwae Marko, umlete pamoja nawe, maana anifaa kwa utumishi. Lakini Tikiko nalimpeleka Efeso. Lile joho nililoliacha kwa Karpo huko Troa, ujapo ulilete, na vile vitabu, hasa vile vya ngozi. Iskanda, mfua shaba, alionyesha ubaya mwingi kwangu; Bwana atamlipa sawasawa na matendo yake. Nawe ujihadhari na huyo, kwa sababu aliyapinga sana maneno yetu.
Katika jawabu langu la kwanza hakuna mtu aliyesimama upande wangu, bali wote waliniacha; naomba wasihesabiwe hatia kwa jambo hilo. Lakini Bwana alisimama pamoja nami akanitia nguvu, ili kwa kazi yangu ule ujumbe utangazwe kwa utimilifu, hata wasikie Mataifa yote.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 145:10 – 13, 17 – 18 (K) 12

(K) Wacha wako, Ee Bwana, wajulisha matendo yako makuu na utukufu wa fahari ya ufalme wako.

Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi,
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako. (K)

Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyaote. (K)

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
Bwana yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu. (K)

SHANGILIO

Yn. 15:1 – 9

Aleluya, aleluya,
Ni mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka mwende mkazae matunda, matunda yenu yapate kukaa.
Aleluya.

INJILI

Lk. 10:1 – 9

Bwana aliweka wengine, sabini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda kila mji na kila mahali alipokusudia kwenda mwenyewe. Akawaambia, Mavuno ni mengi, lakini watenda kazi ni wachache; basi mwombeni Bwana wa mavuno apeleke watenda kazi katika mavuno yake. Enendeni; angalieni, nawatuma kama wanakondoo kati ya mbwa mwitu. Msichukue mfuko, wala mkoba, wala viatu; wala msimwamkie mtu njiani. Na nyumba yoyote mtakayoingia, semeni kwanza, Amani iwemo nyumbani humu; na akiwamo mwana wa amani, amani yenu itamkalia; la, hayumo, amani yenu itarudi kwenu. Basi, kaeni katika nyumba iyo hiyo, mkila na kunywa vya kwao; maana, mtenda kazi amestahili kupewa ujira wake. Msihamehame kutoka nyumba hii kwenda nyumba hii. Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu; wapozeni wagonjwa waliomo, waambieni Ufalme wa Mungu umewakaribia.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Ni nani anayetoa Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?

Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa hutolewa na kuhani tuu yaani Askofu au Padri.. soma zaidi

a.gif Mtume Thoma

Thoma au Didimo, yaani Pacha alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu anayeheshimiwa kama mtakatifu, kwa namna ya pekee na Wakristo wa maeneo yaliyokuwa mashariki kwa Dola la Roma, kuanzia Iraq hadi India… soma zaidi

a.gif Kuna Rehema za namna ngapi?

Rehema za namna mbili.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, OKTOBA 18, 2019 IJUMAA JUMA LA 28 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, OKTOBA 18, 2019 IJUMAA JUMA LA 28 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

a.gif Ni nani hupanga Taratibu za Liturujia?

Mama Kanisa ndiye mwenye kupanga taratibu zote za Liturujia Katika mwaka mzima… soma zaidi

a.gif Kwa kugusa paji la uso tuna maana gani?

Kwa kugusa paji la uso tuna maana ya kukubali kwa akili.. soma zaidi

a.gif Jina Yesu lina maana gani?

Jina Yesu lina maana kuwa "Mungu Anaokoa". (Mdo 4:12).. soma zaidi

a.gif Siku ya Mungu kwa Mkristo ni lini?

Siku ya Mungu kwa Mkristo ni siku ya Dominika, ndio siku aliyofufuka Bwana na huitwa pia Siku ya Bwana.. soma zaidi

a.gif Mtu aweza kupokea Sakramenti ya ndoa zaidi ya mara moja?

Ndiyo, mwenzi akifa yule aliyebaki yupo huru kufunga ndoa tena (1Kor 7:39).. soma zaidi

a.gif Kanisa Katoliki laweza kudanganya katika mafundisho yake?

Hapana. Kanisa Katoliki haliwezi kudanganya katika mafundisho yake kwa sababu Roho Mtakatifu analilinda daima lisikosee na analiongoza. (Yoh 14:26)… soma zaidi

a.gif Mtakatifu Petro Mtume

Petro alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mfuasi wa Yesu Kristo, tena kati ya wandani wake… soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Mawazo na Mipango ya Mungu kwa mtu

Mungu daima anawaza Mema na Anampangia Mtu Mambo mema… soma zaidi

a.gif Mambo ya kufahamu katika kipindi cha kwaresima

Kwa kipindi cha Kwaresma haya ndiyo mambo muhimu unayopaswa kuyajua… soma zaidi

a.gif Matokeo ya Sakramenti ya Daraja ni yapi?

1. Inaleta mmiminiko wa kipekee wa Roho Mtakatifuambao unamlinganisha mhusika na Kristo.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.