MASOMO YA MISA OCTOBER 7, 2019 JUMATATU, JUMA LA 27 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA OCTOBER 7, 2019 JUMATATU, JUMA LA 27 LA MWAKA

SOMO 1

Yon. 1:1- 2:11

Neno la Bwana lilimjia Yona, mwana wa Amitai, kusema, Ondoka, uende Ninawi, mji ule mkubwa, ukapige kelele juu yake; kwa maana uovu wao umepanda juu mbele zangu. Lakini Yona akaondoka akimbilie Tarshishi, apate kujiepusha na uso wa Bwana; akatelemka hata Yafa, akaona merikebu inayokwenda Tarshishi; basi, akatoa nauli, akapanda merikebuni, aende pamoja nao Tarshishi, ajiepushe na uso wa Bwana. Lakini Bwana alituma upepo mkuu baharini, ikawa tufani kubwa baharini, hata merikebu ikawa karibu na kuvunjika.
Basi wale mabaharia wakaogopa, kila mtu akamwomba mungu wake; nao wakatupa baharini shehena iliyokuwa merikebuni, ili kuupunguza uzito wake. Lakini Yona alikuwa ameshuka hata pande za ndani za merikebu; akajilaza, akapata usingizi. Basi nahodha akamwendea, akamwambia, Una nini Ewe ulalaye usingizi? Amka, ukamwombe Mungu wako; labda Mungu huyo atatukumbuka, tusipotee.
Wakasemezana kila mtu na mwenzake, Haya, na tupige kura, tupate kujua mabaya haya yametupata kwa sababu ya nani. Basi wakapiga kura, nayo kura ikamwangukia Yona. Ndipo wakamwambia, Tafadhali utuambie, wewe ambaye mabaya haya yametupata kwa sababu yako; kazi yako ni kazi gani? Nawe umetoka wapi? Nchi yako ni nchi ipi? Nawe u mtu wa kabila gani? Akawaambia, Mimi ni Mwebrania, nami namcha Bwana, Mungu wa mbingu, aliyeviumba bahari nan chi kavu.
Ndipo watu wale wakaogopa mno, wakamwambia, Ni jambo gani hili ulilolitenda! Kwa maana watu wale walijua ya kuwa amekimbia, ajiepushe na uso wa Bwana, kwa sababu alikuwa amewajulisha. Basi wakamwambia, Tukutende nini, ili bahari itutulilie? Kwa maana bahari ilikuwa inazidi kuchafuka. Naye akawaambia, Nikamateni, mnitupe baharini; basi bahari itawatulilia; kwa maana najua ya kuwa ni kwa ajili yangu tufani hii imewapata. Lakini wale watu wakavuta makasia kwa nguvu, ili wapate kurudi pwani, wasiweze; kwa maana bahari ilizidi kuwachafukia sana.
Basi wakamlilia Bwana, wakasema, Twakuomba, Ee Bwana, twakuomba, tusiangamie kwa ajili kwa ajili ya uhai wa mtu huyu, wala usitupatilize kwa ajili ya damu isiyo na hatia; kwa maana wewe, Bwana, umefanya kama ulivyopenda. Basi wakamkamata Yona, wakamtupa baharini, nayo bahari ikaacha kuchafuka. Ndipo wale watu wakamwogopa Bwana mno, wakamtolea Bwana sadaka, na kuweka nadhiri.
Bwana akaweka tayari samaki mkubwa ili ammeze Yona, naye Yona akawa ndani ya tumbo la samaki yule muda wa siku tatu, mchana na usiku. Bwana akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Yon. 2:1-3, 7 (K) 6

(K) Umenipandisha nafsi yangu kutoka shimoni. Ee Bwana.

Nalimlilia Bwana kwa sababu ya shida yangu,
Naye akaniitikia;
Katika tumbo la kuzimu naliomba,
Nawe ukasikia sauti yangu. (K)

Maana ulinitupa vilindini,
Ndani ya moyo wa bahari;
Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;
Mawimbi yako yote na gharika zako zote
Zimepita juu yangu. (K)

Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;
Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu. (K)

Roho yangu ilipozimia ndani yangu.
Nalimkumbuka Bwana;
Maombi yangu yakakuwasilia.
Katika hekalu lako takatifu. (K)

SHANGILIO

Yn. 17:17

Aleluya, aleluya,
Neno lako ndiyo kweli, Ee Bwana ututakase kwa ile kweli.
Aleluya.

INJILI

Lk. 10:25-37

Mwana-sheria mmoja alisimama akamjaribu Yesu, akisema, Mwalimu, nifanye nini ili niurithi uzima wa milele? Akamwambia, Imeandikwa nini katika torati? Wasomaje? Akajibu akasema, Mpende Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote, na kwa nguvu zako zote, na kwa akili zote; na jirani yako kama nafsi yako. Akamwambia, Umejibu vema; fanya hivi nawe utaishi.
Naye akitaka kujidai haki, alimwuliza Yesu, Na jirani yangu ni nani? Yesu akajibu akasema, Mtu mmoja alishuka toka Yerusalemu kwenda Yeriko, akaangukia kati ya wanyang’anyi; wakamvua nguo, wakamtia jeraha, wakaenda zao, wakimwacha karibu ya kufa. Kwa nasibu kuhani mmoja alishuka kwa njia ile; na alipomwona alipitia kando. Na Mlawi vivyo hivyo, alipofika pale akamwona, akapitia kando.
Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipo; na lipomwona alimhurumia, akakaribia, akamfunga jeraha zake, akizitia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza. Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa Zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake, yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi? Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Enenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa wapi?

Sakramenti ya Ekaristi Takatifu Huifadhiwa kwenye Tabernakulo.. soma zaidi

a.gif Je Bikira Maria Alizaa Watoto Wengine?

Mapokeo kuhusu Bikira Maria yanaonyesha alikuwa binti pekee wa wazee watakatifu Yohakimu na Ana. Vilevile
Mt. Yosefu, ingawa kisheria alikuwa mume wake, hakutenda naye tendo la ndoa hata moja. Ndiyo maana kwenye
litania yake tunamuita mwenye usafi kamili. Yosefu likufa kabla Yesu hajaanza utume kwa kubatizwa kwenye mto
Yordani. Sisi tunasadiki Maria ni “Bikira daima”… soma zaidi

a.gif Maana ya kuushinda ulimwengu

Kuushinda ulimwengu ni Kuushinda mwili na akili,.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA OCTOBER 7, 2019 JUMATATU, JUMA LA 27 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA OCTOBER 7, 2019 JUMATATU, JUMA LA 27 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Mkono wako wa kuume

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala za kila siku

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Katarina wa Siena

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

msaada.gif

a.gif Je, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani?

Ndiyo, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani kila wakati hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu.. soma zaidi

a.gif Padri anaondolea dhambi kwa maneno gani?

Padre anaondolea dhambi kwa maneno haya: Nami "Nakuondolea dhambi zako zote kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu"… soma zaidi

a.gif Kabla ya Kupaa mbinguni Yesu aliwaahidi nini Mitume?

Kabla ya kupaa mbinguni Yesu aliwaahidia Mitume kuwapelekea Roho Mtakatifu; ndiye nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu. (Yoh 16:7).. soma zaidi

a.gif Kwa nini Yesu alifanya ishara na miujiza?

Yesu alifanya ishara ili.. soma zaidi

a.gif Mungu aenea pote maaana yake ni nini?

Mungu aenea pote maaana yake yupo kila mahali mbinguni na duniani wala hakuna mahali asipokuwepo?. (Zab, 139:7-12).. soma zaidi

a.gif Kanisa linafafanuaje fumbo la umwilisho?

Linatamka kuwa Yesu Kristo ni Mungu kweli na Mtu kweli. (Ebr 4:15).. soma zaidi

a.gif Kwa nini Kanisa linabatiza watoto wadogo?

Kwa sababu wanazaliwa na dhambi ya asili hivyo wanahitaji kuwekwa huru kutoka mamlaka ya yule mwovu na kuingizwa katika ufalme wa uhuru wa wana wa Mungu.. soma zaidi

a.gif Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,.. soma zaidi

a.gif Tunawaheshimu Watakatifu namna gani?

Tunawaheshimu kwa kuadhimisha sikukuu zao, kwa kuomba maombezi yao, kufuata mifano yao na kuheshimu masalia na sanamu zao, kwa kuinama kichwa kidogo tunapopita mbele yake.. soma zaidi

a.gif Ubahili ni nini?

Ubahili ni kupenda mno mali za dunia na kumsahau Mungu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.