MASOMO YA MISA, OCTOBER 19, 2019, JUMAMOSI YA 28 YA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA, OCTOBER 19, 2019, JUMAMOSI YA 28 YA MWAKA

SOMO 1

Rum. 4:13, 16-18

Ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake si kwa sheria bali kwa haki aliyohesabiwa kwa Imani. Kwa hiyo ilitoka katika Imani, iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa Imani ya Ibrahimu; aliye baba yetu sisi sote; mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.
Naye aliamini kwa kutarajia yasiyoweza kutarajiwa, ilia pate kuwa baba wa mataifa mengi, kama ilivyonenwa, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 105:6-9, 42-43 (K)

(K) Bwana analikumbuka agano lake milele.

Enyi wazao wa Ibrahimu, mtumishi wake;
Enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
Yeye, Bwana, ndiye Mungu wetu;
Duniani mwote mna hukumu zake. (K)

Analikumbuka agano lake milele;
Neno lile aliloviamuru vizazi elfu.
Agano alilofanya na Ibrahimu,
Na uapo wake kwa Isaka (K)

Maana alilikumbuka neno lake takatifu,
Na Ibrahimu, mtumishi wake.
Akawatoa watu wake kwa shangwe,
Na wateule wake kwa nyimbo za furaha. (K)

SHANGILIO

Mt. 4:4

Aleluya, aleluya,
Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Mungu.
Aleluya.

INJILI

Lk. 12:8-12

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Nami nawaambia, kila atakayenikiri mbele ya watu, Mwana wa Adamu naye atamkiri yeye mbele ya malaika wa Mungu; na mwenye kunikana mbele ya watu, huyo atakanwa mbele ya malaika wa Mungu.
Na kila mtu atakayenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali aliyemkufura Roho Mtakatifu hatasamehewa.
Na watakapowapeleka ninyi mbele ya masinagogi na maliwali na wenye mamlaka, msifadhaike kwa kuwaza maneno yenu jinsi mtakavyojibu au kusema; kwa kuwa Roho Mtakatifu atawafundisha saa ile ile yawapasayo kuyasema.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Kujitambua Mbele ya Mungu

Kujitambua wewe ni nani na unanafasi gani mbele ya Mungu, hii ndio njia ya kuelekea Wokovu na Utakatifu… soma zaidi

a.gif Nifunge nini Kwaresma? Mambo ya kufunga kipindi cha Kwaresima

NIFUNGE NINI?
Funga huzuni upate furaha,
Funga ulabu upate siha,
Funga majivuno upata utukufu,
Funga uzinzi upate wongofu,
Funga kisirani upate utakatifu,.. soma zaidi

a.gif Imani ni cheti cha Kuweza kupata yote

Imani ni kuwa na uhakika hata kwa mambo yasiyoonekana na yasiyowezekana. Ni kujua au kutarajia kwa uhakika kwa mambo ambayo bado hayajawa bayana (wazi) kuwa yapo au yatafanyika… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, OCTOBER 19, 2019, JUMAMOSI YA 28 YA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, OCTOBER 19, 2019, JUMAMOSI YA 28 YA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Kanuni ya imani

[Wimbo Mzuri PA.gif] Mama wa Mkombozi

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo mkuu wa Yesu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Picha ya Yesu wa Huruma

a.gif Je, Kanisa linahimiza waamini wapokee Ekaristi wakati gani?

Kanisa linahimiza waamini wapokee Komunyo Takatifu kila siku wanaposhiriki Misa.. soma zaidi

a.gif Tunatambuaje Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu?

Tunatambua Maandiko Matakatifu kati ya maandishi yote ya binadamu kwa njia ya Mapokeo, yaani kwa sababu yametumiwa na Kanisa tangu mwanzo kwa kulisha kwa hakika imani yake… soma zaidi

a.gif Je, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya mwamba?

Ndiyo, Yesu amejenga Kanisa lake imara juu ya Mtume Petro, alichunge lote kwa niaba yake. Papa kama Askofu wa Roma ndiye mwandamizi wa Petro na mkuu wa kundi zima la Maaskofu, waandamizi wa Mitume… soma zaidi

a.gif Faida ya kuabudu Ekaristi Takatifu

1.Kila saa moja tunayotumia kuabudu, inafurahisha moyo wa Yesu na hivyo majina yetu huandikwa mbinguni kwa ajili ya uzima wa milele (Mama Thereza wa Calcuta).. soma zaidi

a.gif Je, Kuangalia Picha za Ngono ni dhambi?

Neno la Msingi:
Zaburi 101:3
“Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.”
Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya "AIBU" wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Watakatifu ndani ya Kanisa Katoliki

Soma haya kuhusu watakatifu;.. soma zaidi

a.gif Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vina maana gani?

Mungu akiwa Roho, viungo ambavyo pengine anapewa vinamaanisha tu sifa fulani: k.mf. macho ujuzi wake, mikono uwezo wake, mabawa ulinzi wake, n.k. “Roho haina mwili na mifupa” (Lk 24:39)… soma zaidi

a.gif Mungu ajua yote maana yake nini?

Mungu ajua yote maana yake ajua ya sasa, ya zamani na ya wakati ujao hata mawazo yetu.. soma zaidi

a.gif Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi mpaka lini?

Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji chetu, hata kwa faida ya wagonjwa na wengineo wasiohudhuria.
Ndiyo sababu tunazidi kumuabudu katika ekaristi, ingawa hatumuoni… soma zaidi

a.gif Mtakatifu Petro Mtume

Petro alikuwa Myahudi wa karne ya 1, mfuasi wa Yesu Kristo, tena kati ya wandani wake… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.