MASOMO YA MISA OCTOBER 17, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 28 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA OCTOBER 17, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 28 LA MWAKA

SOMO 1

Rum. 3:21-30

Haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; ina shuhudiwa na torati na manabii; ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya Imani katika yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya Imani katika damu yake, ili aonyeshe haki yake, kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa Mungu dhambi zote zilizotangulia kufanywa; apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabia haki yeye amwaminiye Yesu.
Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya Imani. Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa Imani pasipo matendo ya sheria. Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; kama kwa kweli Mungu ni mmoja.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 130:1-6 (K)

(K) Kwa Bwana kuna fadhili na ukombozi mwingi.

Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia,
Bwana, uisikie sauti yangu.
Masikio yako na yaisikilize,
Sauti ya dua zangu. (K)

Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu,
Ee Bwana, nani angesimama?
Lakini kwako kuna msamaha,
Ili Wewe uogopwe. (K)

Nimemngoja Bwana, roho yangu imemngoja;
Na neno lake nimelitumainia.
Nafsi yangu inamngoja Bwana,
Kuliko walinzi waingojavyo asubuhi,
Naam, walinzi waingojao asubuhi. (K)

SHANGILIO

Zab. 119:28,33

Aleluya, aleluya,
Unitie nguvu sawasawa na neno lako, Ee Bwana, unifundishe njia ya amri zako.
Aleluya.

INJILI

Lk. 11:47-54

Yesu aliwaambia wanasheria: Ole wenu, kwa kuwa mwajenga maziara ya manabii, na baba zenu ndio waliowaua. Basi, mwashuhudia na kuziridhia kazi za baba zenu; kwa kuwa wao waliwaua nanyi mwawajengea maziara.
Na kwa sababu hiyo hekima ya Mungu ilisema, Tazama, nitatuma kwao manabii na mitume, nao watawaua baadhi yao na kuwafukuza, ili kwa kizazi hiki itakwe damu ya manabii wote, iliyomwagika tangu kupigwa msingi wa ulimwengu; tangu damu ya Habili hata damu ya Zakaria, aliyeuawa kati ya madhabahu na hekalu. Naam, nawaambieni ya kwamba itatakwa kwa kizazi hiki.
Ole wenu, enyi wanasheria, kwa kuwa mmeuondoa ufunguo wa maarifa; wenyewe hamkuingia na wale waliokuwa wakiingia mmewazuia.
Alipotoka humo, waandishi na Mafarisayo walianza kumsonga vibaya, na kumchokoza kwa maswali mengi, wakimvizia, ili wapate neno litokalo kinywani mwake.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Ishara ya Msalaba

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka 'Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina'… soma zaidi

a.gif Mapaji Saba ya Roho Mtakatifu ndio nini?

Mapaji saba ya Roho Mtakatifu ni msaada wake wa kuimarisha na kuzoesha akili na moyo wetu kwa mambo ya utumishi wa Mungu.. soma zaidi

a.gif Agano la Kale lina vitabu vingapi?

Agano la Kale lina vitabu 46.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA OCTOBER 17, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 28 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA OCTOBER 17, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 28 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

a.gif X-mass inavyohusishwa na mpinga Kristo

X-MASS INAYOHUSISHWA NA MPINGA KRISTO NI TAFSIRI YA MTU BINAFSI, MWENYE MALENGO YAKE.. soma zaidi

a.gif Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu lini?

Ubatizo wa watoto wachanga unafanyika tangu mwanzo, usipingwe na yeyote kwa miaka elfu na zaidi. Ni kwamba Wayahudi walipokea watoto katika dini yao kwa kuwatahiri siku ya nane baada ya kuzaliwa.

“Hata zilipotimia siku nane za kumtahiri, aliitwa jina lake Yesu” (Lk 2:21)… soma zaidi

a.gif Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni vipi?

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano la Kale ni.. soma zaidi

a.gif Neema ni nini?

Neema ni kipaji cha roho kinachopita nguvu za viumbe vyote; ndicho kipaji tupewacho na Roho Mtakatifu ili tupate uzima wa milele. (Lk 1:30, Rum 5:2).. soma zaidi

a.gif Sala ya Baba yetu

Inasaliwa Hivi;.. soma zaidi

a.gif Matunda ya kuongozwa na Roho Mtakatifu ni yapi?

Matunda ya Roho Mtakatifu ni;.. soma zaidi

a.gif Tunaweza kusadiki vipi?

Tunaweza kusadiki kwa msaada wa Roho Mtakatifu tu, anayetuelekeza kwa Mungu, akituangazia Neno lake na kutuvuta tulikubali kwa moyo… soma zaidi

a.gif Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni nini?

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni kusadiki kwa nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu.. soma zaidi

a.gif Ni fadhila ipi inayoondoa uchafu?

Fadhila inayoondoa uchafu ni fadhila ya Usafi wa Moyo.. soma zaidi

a.gif Swali la kutisha

.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.