MASOMO YA MISA, OCTOBER 11, 2019, IJUMAA, JUMA LA 27 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, OCTOBER 11, 2019, IJUMAA, JUMA LA 27 LA MWAKA

SOMO 1

Yoe. 1:13-15;2:1-2

Jikazeni mkaomboleze, enyi makuhani; Pigeni yowe, enyi wahudumu wa madhabahu; Njoni mlale usiku kucha katika magunia, Enyi wahudumu wa Mungu wangu; Kwa kuwa sadaka ya unga na sadaka ya kinywaji zimezuiwa katika nyumba ya Mungu wenu. Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa Bwana, Mungu wenu, na kumlilia Bwana, Ole wake siku hii!
Kwa maana siku ya Bwana inakaribia, nayo itakuja kama uangamivu utokao kwake aliye Mwenyezi.
Pigeni tarumbeta katika Sayuni, pigeni na kelele katika mlima wangu mtakatifu; wenyeji wote wa nchi na watetemeke; kwa maana siku ya Bwana inakuja. Kwa sababu inakaribia.
Siku ya giza na weusi, siku ya mawingu na giza kuu. Kama mapambazuko yakitandazwa juu ya milima, hao ni wakuu tena wenye nguvu, mfano wao haukuwako kamwe, wala hautakuwako baada ya hao, hata katika miaka ya vizazi vingi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 9:1-2.5.15.7-8 (K)8

(K) Bwana atauhukumu ulimwengu kwa haki.

Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote;
Nitayasimulia matendo yako yote ya ajabu;
Nitafurahi na kukushangilia Wewe;
Nitaliimbia jina lako, Wewe uliye juu. (K)

Umewakemea mataifa;
Na kumwangamiza mdhalimu;
Umelifuta jina lao milele na milele;
Mataifa wamezama katika shimo walilolifanya;
Kwa wavu waliouficha imenaswa miguu yao. (K)

Bali Bwana atakaa milele,
Ameweka kiti chake tayari kwa hukumu.
Naye atauhukumu ulimwengu kwa haki;
Atawaamua watu kwa adili. (K)

SHANGILIO

1Thes. 2:13

Aleluya, aleluya,
Lipokeeni neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya.

INJILI

Lk.11:15-26

Wengine wa makutano walisema, Atoa pepo kwa Beelzebuli, mkuu wa pepo. Wengine walimjaribu, wakitaka ishara itokayo mbinguni. Naye akajua mawazo yao, akawaambia. Kila ufalme uliofitinika wenyewe kwa wenyewe hufanyika ukiwa; na nyumba juu ya nyumba huanguka. Basi, ikiwa shetani naye amefitinika juu ya nafsi yake, ufalme wake utasimamaje? Kwa kuwa ninyi mnasema kwamba mimi natoa pepo kwa Beelzebuli. Basi, kama mimi nikitoa pepo kwa Beelzebuli, wana wenu je! Huwatoa kwa nani? Kwa sababu hiyo, hao ndio watakaowahukumu. Lakini, ikiwa mimi natoa pepo kwa kidole cha Mungu, basi ufalme wa Mungu umekwisha kuwajilia. Mtu mwenye nguvu aliyejifunga silaha zake, alindapo nyumba yake, vitu vyake vi salama; lakini mtu mwenye nguvu kuliko yeye atakapomwendea na kumshinda, amnyang’anya silaha zake zote alizokuwa akizitegemea, na kuyagawanya mateka yake.
Mtu ambaye si pamoja nami yu kinyume changu; na mtu aliyekusanya pamoja nami hutawanya.
Pepo mchafu amtokapo mtu, hupitia mahali pasipo maji, akitafuta mahali pa kupumzika; asipoona, husema, Nitarudia nyumba yangu niliyotoka. Hata afikapo, akaiona imefagiwa na kupambwa, ndipo huenda akachukua pepo wengine saba, walio waovu kuliko yeye mwenyewe, wakaingia na kukaa humo; na mtu yule hali yake ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Katika Amri ya nne ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tuwaheshimu wazazi wetu na wakubwa wetu wote, tuwapende, tuwatii na tuwaombee. (Kut 20:12, Kol 3:20).. soma zaidi

a.gif Ishara ya msalaba ni nini?

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka "Kwa jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina".. soma zaidi

a.gif Je, Kuangalia Picha za Ngono ni dhambi?

Neno la Msingi:
Zaburi 101:3
“Sitaweka mbele ya macho yangu Neno la uovu. Kazi yao waliopotoka naichukia, Haitaambatana nami.”
Watu wengi wameanguka katika mtego huu wa Ibilisi na kujikuta wakifanya mambo ya "AIBU" wanapokuwa sehemu zao za Siri iwe ni chumbani au bafuni… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, OCTOBER 11, 2019, IJUMAA, JUMA LA 27 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, OCTOBER 11, 2019, IJUMAA, JUMA LA 27 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala kwa Mtakatifu Yosefu

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kwa Furaha Kuu

[Tafakari ya Sasa] 👉Mkono wa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Getrudi Mkuu

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

UJUMBE-WA-SHUKRANI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Muujiza wa Madonda ya padre Pio

Angalia video hapa.. soma zaidi

a.gif Makala mpya kwa sasa

Makala Mpya ni kama ifuatavyo,.. soma zaidi

a.gif Maneno ya busara kwa anayetafuta Mme au Mke

Usifanye maamuzi kwa kutumia vigezo vyepesi.
"Nampenda sana"
"Tunapendana mno"
Unaweza kumpenda mtu yeyote. Upendo huzaliwa na huuawa na mazingira fulani. Kwamba unampenda (sana) sio jambo la msingi… soma zaidi

a.gif Aliyevumbua utaratibu wa kuweka mistari na sura katika Biblia

Je, WAJUA?
Aliyevumbua utaratibu wa kuweka SURA na MISTARI katika BIBLIA.
Ni kasisi (Padri) Mwingereza,.. soma zaidi

a.gif Asili ya uhai wote ni nani?

Asili ya uhai wote ni Mwenyezi Mungu. “Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi” (Mwa 1:1)… soma zaidi

a.gif Sala Mbalimbali za katoliki

Lala Muhimu za Kikatoliki.. soma zaidi

a.gif Je sanamu zimekatazwa?

Sanamu hazijakatazwa, ila tunaziheshimu kwa sababu zinatukumbusha Mungu na Watakatifu. (Kut 25:18-22)… soma zaidi

a.gif MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA

Sisi Wakatoliki nyakati hizi zilizojaa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayotumia Biblia na kuitafsiri kadiri ya
imani yao ama wenyewe wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya
kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu,
tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu
wote pamoja na Yohane Mbatizaji, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27). Hivyo yale yote
tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia kwa
hiari fumbo la mpango wake… soma zaidi

a.gif Askofu ampaje Mkristo Kipaimara?

Kwanza ananyoosha Mikono juu yake akimwombea mapaji saba ya Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni nani?

Mhusika mkuu wa mafumbo hayo ni Mungu ambaye kwa njia hiyo anazidi kutufanyia maajabu alivyoyafanya Yesu alipokuwa duniani. Kama tunda la kutukomboa kwa kifo na ufufuko wake, Baba anatujaza humo Roho Mtakatifu kama advansi ya uzima wa milele… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.