MASOMO YA MISA NOVEMBA 7, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 31 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA NOVEMBA 7, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 31 LA MWAKA

SOMO 1.

Warumi 14:7-12

Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.
Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.
Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
Kwa kuwa imeandikwa,
Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu;
Na kila ulimi utamkiri Mungu.
Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.

Neno la Bwana…….Sifa kwako ee Kristo.

WIMBO WA KATIKATI

Zaburi 27:1,4,13-14 (K)13

(K)Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA Katika nchi ya walio hai.

BWANA ni nuru yangu na wokovu wangu,
Nimwogope nani?
BWANA ni ngome ya uzima wangu,
Nimhofu nani?
(K)

Neno Moja nimelitaka kwa BWANA,
Nalo ndilo nitakalolitafuta,
Nikae nyumbani mwa BWANA
Siku zote za maisha yangu,
Niutazame uzuri wa BWANA,
Na kutafakari hekaluni mwake.
(K)

Naamini ya kuwa nitauona wema wa BWANA
Katika nchi ya walio hai.
Umngoje BWANA, uwe hodari,
Upige moyo konde, naam, umngoje BWANA.
(K)

SHANGILIO.

Mathayo 11:28

Aleluia Aleluia
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Aleluia!

INJILI.

Luka 15:1-10

Basi watoza ushuru wote na wenye dhambi walikuwa wakimkaribia wamsikilize.
Mafarisayo na waandishi wakanung’unika, wakisema, Mtu huyu huwakaribisha wenye dhambi, tena hula nao.
Akawaambia mfano huu, akisema,
Ni nani kwenu, mwenye kondoo mia, akipotewa na mmojawapo, asiyewaacha wale tisini na kenda nyikani, aende akamtafute yule aliyepotea hata amwone?
Naye akiisha kumwona, humweka mabegani pake akifurahi.
Na afikapo nyumbani kwake, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimekwisha kumpata kondoo wangu aliyepotea.
Nawaambia, Vivyo hivyo kutakuwa na furaha mbinguni kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye, kuliko kwa ajili ya wenye haki tisini na kenda ambao hawana haja ya kutubu.
Au kuna mwanamke gani mwenye shilingi kumi, akipotewa na moja, asiyewasha taa na kufagia nyumba, na kutafuta kwa bidii hata aione?
Na akiisha kuiona, huwaita rafiki zake na jirani zake, akawaambia, Furahini pamoja nami, kwa kuwa nimeipata tena shilingi ile iliyonipotea.
Nawaambia, Vivyo hivyo kuna furaha mbele ya malaika wa Mungu kwa ajili ya mwenye dhambi mmoja atubuye.

Neno la Bwana……Sifa kwako ee Kristo.


a.gif Lengo kuu la visakramenti ni lipi?

Lengo kuu la visakramenti ni kuwaandaa watu wapokee kwa imani sakramenti zitakazowatia uzima wa Mungu unaodumu milele. Hivyo visakramenti visitiwe maanani kuliko sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe ziwe kiini cha maisha yetu… soma zaidi

a.gif Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha

Yesu ni Mwanga na Uovu ni giza.. soma zaidi

a.gif Biblia ni nini? Asili, Historia, waandishi na mipaka yake

Biblia ni mkusanyiko wa vitabu mbalimbali vinavyohusu kazi ya Mungu ya kuwakomboa mwanadamu kuanzia enzi za Mababu na manabii Wa Waisraeli, Enzi za Yesu na za Mitume wa Yesu… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA NOVEMBA 7, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 31 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA NOVEMBA 7, 2019 ALHAMISI, JUMA LA 31 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA KWA BIKIRA MARIA WA MATESO

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala za kila siku

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Bakhita

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

a.gif Kampeni ya utunzaji wa miti na misitu

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kupanda na kutunza miti na misitu kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa miti na misitu ikitunzwa vizuri inaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… soma zaidi

a.gif Swali la kutisha

.. soma zaidi

a.gif Katika amri ya kwanza ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tusadiki kuwa Mungu ni mmoja, ndiye Baba yetu na Mkubwa wetu: tumpende, tumwabudu yeye peke yake. (Mt 10:33, Kumb 6:4-9).. soma zaidi

a.gif MPANGILIO WA KURASA ZA POSTI NA MAKALA

Makala kuu za Wakatoliki;.. soma zaidi

a.gif Anayetaka kuwa padri yampasa nini?

Yampasa;
1. Awe na tabia njema, akili za kutosha na afya nzuri… soma zaidi

a.gif Kwa nini Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu”?

Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu” kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: “Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?.. soma zaidi

a.gif Soma stori hii, unaweza ukajifunza kitu

SOMA HII STORY UNAWEZA UKAJIFUNZA KITU.
Kijana mmoja alisafiri kwa meli na rafiki zake,
wakiwa katikati ya safari yao meli ilianza
kuzama. Watu wengi pamoja na rafiki wa yule
kijana walikufa maji wakati wanajaribu kujiokoa
kwa kuogelea, lakini yule kijana alifanikiwa.. soma zaidi

a.gif Kwa sababu gani yatupasa kuwaheshimu Baba na Mama?

Yatupasa kuwaheshimu Baba na Mama kwa sababu;.. soma zaidi

a.gif Mitume kumi na wawili wa Yesu Kristu ni wapi?

Mitume wa yesu ni;
1. Simoni/Petro
2. Yakobo
3. Yohane
4. Andrea
5. Filipo.. soma zaidi

a.gif Taifa la Mungu limeundwa kwa namna gani?

Taifa la Mungu limeundwa kwa Maklero yaani Maaskofu, Mapadri, Mashemasi, Watawa na Walei… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.