MASOMO YA MISA NOVEMBA 5, 2019 JUMANNE, JUMA LA 31 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA NOVEMBA 5, 2019 JUMANNE, JUMA LA 31 LA MWAKA

SOMO 1

Rum. 12:5-16

Sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema tuliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya Imani; ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia, kwa bidi; mwenye kurehemu, kwa furaha.
Pendo na lisiwe na unafiki; lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.
Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
_

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 131

(K) Moyo wangu uwe na Amani kwako, Ee Bwana.

Bwana, moyo wangu hauna kiburi,
Wala macho yangu hayainuki.
Wala sijishughulishi na mambo makuu,
Wala na mambo yashindayo nguvu zangu. (K)

Hakika nimeituliza nafsi yangu,
Na kuinyamazisha.
Kama mtoto aliyeachishwa
Kifuani mwa mama yake;
Ndivyo roho yangu ilivyo kwangu. (K)

Ee Israeli, umtarajie Bwana,
Tangu leo n ahata milele. (K)
_

SHANGILIO

Zab. 147:12,15

Aleluya, aleluya,
Msifu Bwana, Ee Yerusalemu, huipeleka amri yake juu ya nchi.
Aleluya.
_

INJILI

Lk. 14:15-24

Mmojawapo wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu alimwambia, Heri yule atakayekula mkate katika ufalme wa Mungu. Akamwambia, Mtu mmoja alifanya karamu kubwa, akaalika watu wengi, akamtuma mtumwa wake saa ya chakula awaambie wale walioalikwa, Njoni, kwa kuwa vitu vyote vimekwisha kuwekwa tayari. Wakaanza wote kutoa udhuru kwa nia moja. Wa kwanza alimwambia, Nimenunua shamba, sharti niende nikalitazame; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimenunua ng’ombe jozi tano, ninakwenda kuwajaribu; tafadhali unisamehe. Mwingine akasema, Nimeoa mke, na kwa sababu hiyo siwezi kuja.
Yule mtumwa akaenda, akampa bwana wake habari ya mambo hayo. Basi, yule mwenye nyumba akakasirika, akamwambia mtumwa wake, Toka upesi, uende katika njia kuu na vichochoro vya miji, ukawalete hapa maskini, na vilema, na vipofu, na viwete. Mtumwa akasema, Bwana, hayo uliyoagiza yamekwisha tendeka, n ahata sasa ingaliko nafasi.
Bwana akamwambia mtumwa, Toka nje uende barabarani na mipakani, ukawashurutishe kuingia ndani, nyumba yangu ipate kujaa. Maana nawaambia ya kwamba katika wale walioalikwa, hapana hata mmoja atakayeionja karamu yangu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Agano la Kale lina vitabu vingapi?

Agano la Kale lina vitabu 46.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu, Umoja

Karibu Tafakari,.. soma zaidi

a.gif Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?

Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA NOVEMBA 5, 2019 JUMANNE, JUMA LA 31 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA NOVEMBA 5, 2019 JUMANNE, JUMA LA 31 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu anasubiri sala zako

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Justin mfiadini

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

a.gif Watoto wa Yakobo ni Wepi?

Watoto wa Yakobo ni
1. Reubeni
2. Simeoni
3. Lawi
4.Yuda
5. Dani.. soma zaidi

a.gif Kifungu cha Biblia kinachothibitisha kua Bikira Maria Mama wa Yesu ni Mama wa Wakristu Wote

Kwa ufupi.. soma zaidi

a.gif Ni fadhila ipi yenye kuondoa wivu?

Fadhila inayoondoa wivu ni fadhila ya wema.. soma zaidi

a.gif Jina Yesu lina maana gani?

Jina Yesu lina maana kuwa "Mungu Anaokoa". (Mdo 4:12).. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki, Namna ya Kuwa na Amani

Namna pekee ya kuwa na Amani ni kuishi Mapenzi ya Mungu,.. soma zaidi

a.gif Kampeni ya usafi na Utunzaji wa mazingira

Kampeni hii ilianzishwa na Melkisedeck Leon Shine mwaka 2018.
Lengo la kampeni Hii ni kuhamasisha watu kusafisha na kutunza mazingira yao kwa manufaa yao ya sasa na kwa manufaa ya vizazi vijavyo.
Kampeni hii inaamini kuwa mazingira yakisafishwa na kutunzwa vizuri yanaweza kuwa msaada kijamii, kiuchumi na kiafya kwa kizazi hiki na kizazi kijacho… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Daraja ina ngazi ngapi?

Sakramenti ya Daraja inazo ngazi tatu, nazo ni Ushemasi, Upadre, Uaskofu.. soma zaidi

a.gif Mungu na Mikogo yake

Mimi sio msomi wa Biblia na wala sio muhibiri, lakini kwa nilipofanikiwa kuisoma na kuielewa Biblia nimegundua jambo:-
Watu wote wa kiagano katika Biblia(Bible Covenant People), walifanikiwa sana wakati wa nyakati ngumu na zenye changamoto kali. Angalia mifano:-.. soma zaidi

a.gif Hatua za maisha ya kitawa ni zipi?

Hatua za maisha ya kitawa ni
1. Uaspiranti - Mtarajiwa wa Maisha ya Kitawa
2. Ukandidati - Mtarajiwa wa maisha ya kitawa
3. Upostulanti - uombaji wa Maisha ya kitawa.. soma zaidi

a.gif Safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu

Leo tunatafakari kuhusu safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu,.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.