MASOMO YA MISA NOVEMBA 4, 2017 JUMATATU, JUMA LA 31 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA NOVEMBA 4, 2017 JUMATATU, JUMA LA 31 LA MWAKA

SOMO 1

Rum. 11:29-36

Karama za Mungu hazina majuto, wala mwito wake.
Kwa maana kama ninyi zamani mlivyomwasi Mungu, lakini sasa mmepta rehema kwa kuasi kwao; kadhalika na hao wameasi sasa, ili kwa kupata rehema kwenu wao nao wapate rehema. Maana Mungu amewafunga wote pamoja katika kuasi ili awarehemu wote.
Jinsi zilivyo kuu utajiri na hekima na maarifa ya Mungu! Maana ni nani aliyeijua nia ya Bwana? Au ni nani aliyekuwa mshauri wake? Au ni nani aliyempa yeye kitu kwanza, naye atalipwa tena? Kwa kuwa vitu vyote vyatoka kwake, viko kwa uweza wake, tena vinarejea kwake. Utukufu una yeye milele. Amina.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.
_

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 69:29-30, 32-33, 35-36 (K) 14

(K) Kwa wingi wa fadhili zako unijibu, Ee Bwana.

Nami niliye maskini na mtu wa huzuni.
Mungu, wokovu wako utaniinua.
Nitalisifu jina la Mungu kwa wimbo,
Nami nitamtukuza kwa shukrani. (K)

Walioonewa watakapoona watafurahi;
Enyi mmtafutao Mungu, mioyo yenu ihuishwe.
Kwa kuwa Bwana huwasikia wahitaji,
Wala hawadharau wafunga wake. (K)

Maana Mungu ataiokoa Sayuni,
Na kuijenga miji ya Yuda,
Na watu watakaa ndani yake na kuimiliki.
Wazao wa watumishi wake watairithi,
Nao walipendao jina lake watakaa humo. (K)
_

SHANGILIO

Zab. 119:105

Aleluya, aleluya,
Neno lako ni taa ya miguu yangu, na mwanga wa njia yangu.
Aleluya.
_

INJILI

Lk. 14:12 – 14

Yesu alimwambia yule aliyemwalika, Ufanyapo chakula cha mchana au cha jioni, usiwaite rafiki zako, wala ndugu zako, wala jamaa zako, wala jirani zako wenye mali; wao wasije wakakualika wewe ukapata malipo. Bali ufanyapo karamu waite maskini, vilema, viwete, vipofu, nawe utakuwa heri, kwa kuwa hao hawana cha kukulipa; kwa maana utalipwa katika ufufuo wa wenye haki.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Mkristo Mkatoliki awezaje kufunga ndoa mchanganyiko au utofauti wa dini kwa uhalali?

Aweza kufunga ndoa hiyo kwa uhalali baada ya kupata ruhusa maalumu ya Askofu kwa Barua… soma zaidi

a.gif Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi mpaka lini?

Baada ya mageuzo Yesu anabaki katika ekaristi moja kwa moja. Maumbo ya mkate na divai yanazidi kudokeza uwepo wake kama chakula na kinywaji chetu, hata kwa faida ya wagonjwa na wengineo wasiohudhuria.
Ndiyo sababu tunazidi kumuabudu katika ekaristi, ingawa hatumuoni… soma zaidi

a.gif Mpende mkeo, okoa nyumba yako leo

Mpende mke wako mzuri
Usimkaripie mke wako ukiwa unaongea nae. Inamuumiza sana.
Mithali 15:1.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA NOVEMBA 4, 2017 JUMATATU, JUMA LA 31 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA NOVEMBA 4, 2017 JUMATATU, JUMA LA 31 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA MBELE YA SAKRAMENTI KUU II

[Wimbo Mzuri PA.gif] Ewe Maria Umebarikiwa

[Tafakari ya Sasa] 👉Umuhimu wa kumsogelea Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Ambrosi

a.gif Yesu Alianza kuhubiri injili kwa maneno gani?

"Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili" (Mk 1:15).. soma zaidi

a.gif Kama padri hatapatika na mgonjwa afanye nini?

Kama padri hatapatikana mgonjwa aweke nia ya kuungama na afanye majuto kamili.. soma zaidi

a.gif Kilindi cha Huruma ya Mungu

Habari njema ni kwamba Yesu sasa anakuja kwako Kama Bwana wa Huruma, Mwalimu na Rafiki Mwema Akupendaye, Angalia Usichelewe Wakati akija Kama Hakimu asikukute bado huna ushirika nae na hujui haki na hukumu yake. Wakati ndo huu wa kukimbilia Huruma na Upendo wake wa Bure Kwako... soma zaidi

a.gif Je, miujiza inaweza kutusaidia tusadiki?

Ndiyo, miujiza inaweza kutusaidia tusadiki, lakini inaweza kutudanganya pia… soma zaidi

a.gif Dhambi zinatofautianaje katika uzito?

Kuna:
1. Dhambi ya Mauti (Dhambi kubwa) na
2. Dhambi nyepesi (Dhambi ndogo).. soma zaidi

a.gif Mambo yanayowazuia Waumini na Watumishi wa Mungu Kufikia Ukamilifu na Utakatifu

Leo nimekuandalia Tafakari kuhusu Mambo yanayowazuia Waumini na watumishi wa Mungu Kuishi Kitakatifu na kufikia Ukamilifu. Mambo haya yanaweza yakaonekana sio dhambi au makosa kwa mtu lakini ni vikwazo kwa mtu kufikia Ukamilifu hasa anaposhindwa kuyajua na kuyaepuka. Wengi wanajiona kwamba wako salama lakini kumbe wako katika dhambi… soma zaidi

a.gif Yesu Kristu alizaliwa wapi?

Yesu Kristu alizaliwa Bethlehemu pangoni (Lk 2:4-7).. soma zaidi

a.gif Kanisa linaheshimu marehemu kwa namna gani?

Kanisa linaheshimu marehemu kwa kuwafanyia mazishi huku likiwaombea kwa Mungu… soma zaidi

a.gif MITAGUSO MIKUU

Yesu Kristo aliwakabidhi mitume kumi na wawili uongozi wa Kanisa wakiwa kundi moja lenye mkuu wake, yaani Petro. Vilevile waandamizi wao, yaani maaskofu wote, ni kundi moja na Papa wa Roma ndiye mkuu wao. Huyo peke yake, na kundi la maaskofu likiwa pamoja naye na chini yake, ndio wenye mamlaka ya juu katika Kanisa lote. Mamlaka hiyo inatumika kwa namna ya pekee unapofanyika mtaguso mkuu, yaani mkutano maalumu wa maaskofu uliokubaliwa na Papa kuwa unawakilisha kundi hilo lote. Hakuna uamuzi wa kudumu kuhusu ipi ni mikuu kati ya mitaguso yote iliyofanyika katika historia ya Kanisa. Tangu karne XVI Wakatoliki wataalamu wa sheria za Kanisa wanatoa orodha yao, ambayo kwa sasa ni kama ifuatavyo… soma zaidi

a.gif Je yatupasa kufanya kazi?

Ndiyo, kwa sababu:.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.