MASOMO YA MISA, NOVEMBA 2, 2019 JUMAMOSI JUMA LA 30 LA MWAKA KUWAKUMBUKA MAREHEMU WOTE

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?


MASOMO YA MISA, NOVEMBA 2, 2019 JUMAMOSI JUMA LA 30 LA MWAKA KUWAKUMBUKA MAREHEMU WOTE

SOMO 1

Isa 25: 6-9

Na katika mlima huu Bwana wa majeshi atawafanyia mataifa yote karamu ya vitu vinono, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, karamu ya vinono vilivyojaa mafuta, karamu ya divai iliyokaa juu ya urojorojo wake, iliyochujwa sana. Naye katika mlima huu atauharibu uso wa sitara iliyowekwa juu ya watu wote, na utaji ule uliotandwa juu ya mataifa yote. Amemeza mauti hata milele; na Bwana Mungu atafuta machozi katika nyuso zote; na aibu ya watu wake ataiondoa katika ulimwengu wote; maana Bwana amenena hayo. Katika siku hiyo watasema,Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidiye; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu

_

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 23 (K) 1 au 4

(K. 1) Bwana ndiye mchungaji wangu, sitapungukiwa na kitu. (au)

(K. 4) Nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti, sitaogopa mabaya;

Kwa maana wewe upo pamoja nami

Bwana ndiye mchungaji wangu,
Sitapungukiwa na kitu.
Katika malisho ya majani mabichi hunilaza.
Kando ya maji ya utulivu huniongoza. (K)

Hunihuisha nafsi yangu; na kuniongoza,
Katika njia za haki kwa ajili ya jjina lake.
Naam, nijapopita kati ya bonde la uvuli wa mauti,
Sitaogopa mabaya;
Kwa maana wewe upo pamoja nami,
Gongo lako na fimbo yangu vyanifariji. (K)

Waandaa meza mbele yangu,
Machoni pa watesi wangu.
Umenipaka mafuta kichwani pangu,
Na kikombe changu kinafurika. (K)

Hakika wema na fadhili zitanifuata,
Siku zote za maisha yangu;
Nami nitakaa nyumbani mwa Bwana milele. (K)
_

SOMO 2

Rum 5:5-11

Tumaini halitahayarishi; kwa maana pendo la Mungu limekwisha kumiminwa katika mioyo yetu na Roho Mtakatifu tuliyepewa sisi. Kwa maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Kwa kuwa ni shida mtu kufa kwa ajili ya mtu mwenye haki; lakini yawezekana mtu kuthubutu kufa kwa ajili ya mtu aliye mwema. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikuwa kwa ajili yetu, tulipokwa tungali wenye dhambi. Basi zaidi sana tukiisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tutaokolewa na ghadhabu kwa yeye. Kwa maana ikiwa tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu

_

SHANGILIO

Ufu. 14:13

Aleluya, aleluya,
Heri wafu wafao katika Bwana tangu sasa! Wapate kupumzika baada ya taabu zao, kwa kuwa matendo yao yafuatana nao.
Aleluya.

_

INJILI

Mk 15: 33-39, 16: 1-6.

Ilipokuwa saa sita, palikuwa na giza juu ya nchi yote, hata saa tisa. Na saa tisa Yesu akapaza sauti yake kwa nguvu, Eloi, Eloi, lama sabakthani? Maana yake, Mungu wangu, Mungu wangu, mbona
umeniacha? Na baadhi yao waliosimama pale, walisema, Tazama, anamwita Eliya. Na mmoja akaenda mbio, akajaza sifongo siki, akaitia juu ya mwanzi, akamnywesha, akisema, Acheni; na tuone kwamba Eliya anakuja kumtelemsha. Naye Yesu akatoa sauti kuu, akakata roho. Pazia la hekalu likapasuka vipande viwili toka juu hata chini. Basi yule akida, aliyesimama hapo akimwelekea, alipoona ya kuwa alikata roho jinsi hii, akasema, Hakika mtu huyu alikuwa Mwana wa Mungu.

Hata sabato ilipokwisha kupita, Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yakobo, na Salome walinunua manukato wapate kwenda kumpaka. Hata alfajiri mapema, siku ya kwanza ya juma, wakaenda kaburini, jua lilipoanza kuchomoza.

Wakasemezana wao kwa wao, Ni nani atakaye-vingirisliia lile jiwe mlangoni pa kaburi? Hata waalipotazama, waliona ya kuwa lile jiwe limekwisha kuvingirishwa; nalo lilikuwa kubwa mno. Wakaingia kaburini wakaona kijana ameketi upande wa kuume, amevaa vazi jeupe; wakastaajabu. Naye akawaambia, Msistaajabu; mnamtafuta Yesu Mnazareti, aliyesulibiwa; amefufuka; hayupo hapa; patazameni mahali walipomweka.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif MIUJIZA NA MATOKEO YA MUNGU NA WATAKATIFU

Ingiza kichwa cha habari cha Muujiza au matokeo hapa chini kwenye kaboksi kisha bofya mbele yake.. soma zaidi

a.gif Kwa nini ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo?

Ekaristi inaitwa sakramenti ya upendo kwa sababu kila tunapofanya ukumbusho wa sadaka hiyo pekee tunazidi kujifunza na kupokea upendo ambao siku hiyo Yesu “ali amewapenda watu wake katika ulimwengu, aliwapenda upeo” (Yoh 13:1)... soma zaidi

a.gif Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu ngapi?

Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu tatu.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, NOVEMBA 2, 2019 JUMAMOSI JUMA LA 30 LA MWAKA KUWAKUMBUKA MAREHEMU WOTE

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, NOVEMBA 2, 2019 JUMAMOSI JUMA LA 30 LA MWAKA KUWAKUMBUKA MAREHEMU WOTE

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉ROZARI YA MATESO SABA YA BIKIRA MARIA

[Tafakari ya Sasa] 👉Maisha ya Kikristo ni sala

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Picha ya Yesu wa Huruma

a.gif Je ni dhambi kukosa Misa Jumapili?

NDIYO. Ni dhambi kubwa kukosa Misa kwa Makusudi siku ya Jumapili/Dominika na Sikukuu zilizoamriwa… soma zaidi

a.gif Yesu alitufundisha sala gani?

Yesu alitufundisha sala ya Baba Yetu (Mt. 6:9-13).. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Daraja ina ngazi ngapi?

Sakramenti ya Daraja inazo ngazi tatu, nazo ni Ushemasi, Upadre, Uaskofu.. soma zaidi

a.gif Safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu

Leo tunatafakari kuhusu safari ya kupata fadhila ya Unyenyekevu,.. soma zaidi

a.gif Chagua kunyamaza: Huu ni ushauri kwa Leo

MITHALI 11:12 Asiye na akili humdharau mwenziwe; Bali mtu aliye na ufahamu hunyamaza… soma zaidi

a.gif Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa vipi?

Tunapoadhimisha mafumbo hayo, Mungu anatukuzwa kwa kuwa ndivyo anavyotufanya “tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo… tupate kuwa sifa ya utukufu wake” (Ef 1:4,12)… soma zaidi

a.gif Wazazi wawaleeje watoto wao katika imani ya Kikristo?

Wawalee hasa kwa mfano wao, kwa sala, kwa katekesi ya kifamilia na kushiriki maisha ya Kanisa.. soma zaidi

a.gif Yesu alihalalisha ulaji wa vyakula vyote, Hakuna chakula kinachoweza kumtia mtu unajisi

Marko 7:14-23
14 Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, "Nisikilizeni nyote, mkaelewe. 15 Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu toka nje ambacho chaweza kumtia mtu najisi. Lakini kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia mtu najisi." 16 Mwenye masikio na asikie!.. soma zaidi

a.gif Jinsi Biblia inavyomueleza Bikira Maria

Biblia inafundisha hivi,.. soma zaidi

a.gif Imani ni cheti cha Kuweza kupata yote

Imani ni kuwa na uhakika hata kwa mambo yasiyoonekana na yasiyowezekana. Ni kujua au kutarajia kwa uhakika kwa mambo ambayo bado hayajawa bayana (wazi) kuwa yapo au yatafanyika… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.