MASOMO YA MISA, NOVEMBA 10, 2019 DOMINIKA YA 32 YA MWAKA C WA KANISA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA, NOVEMBA 10, 2019 DOMINIKA YA 32 YA MWAKA C WA KANISA

WIMBO WA MWANZO

Zab 88:2

Maombi yangu yafike mbele zako, uutegee ukelele wangu sikio lako, Ee Bwana.

SOMO 1

2Mak. 7:1 – 2, 9 – 14

Ilitokea ya kuwa ndugu saba, pamoja na mama yao, walikamatwa kwa amri ya mfalme na kuteswa sana kwa mijeledi na mapigo ili kuwashurutisha kuonja nyama marufuku ya nguruwe. Mmoja akajifanya menaji wao, akasema, Wataka kuuliza nini na kujua nini juu yetu? Sisi tu tayari kufa kuliko kuzivunja amri za wazee wetu. Wa pili alipokuwa kufani alisema, Wewe, mdhalimu, unatufarikisha na maisha ya sasa lakini Mungu wa ulimwengu atatufufua sisi tuliokufa kwa ajili ya amri zake, hata tupate uzima wa milele. Na baada yake alidhihakiwa yule wa tatu. Naye mara alipoagizwa, alitoa ulimi wake, akanyosha mikono yake bila hofu, akasema kw aushujaa, Kutoka mbinguni nalipewa hivi, na kwa ajili ya amri za Mungu navihesabu kuwa si kitu, na kwake natumaini kuvipokea tena. Hata mfalme na watu wake walishangazwa kwa roho ya kijana huyu, kwa jinsi alivyoyadharau maumivu yake. Akiisha kufa huyu, walimtesa wan ne na kumtendea mabaya yale yale. Naye alipokaribia kufa alisema hivi; Ni vema kufa kwa mikono ya wanadamu na kuzitazamia ahadi zitokazo kwa Mungu, kuwa tutafufuliwa naye. Lakini kwako wewe hakuna ufufuo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 17:1, 5 – 6, 8, 15 (K) 15

(K) Ee, Bwana niamkapo nitashibishwa kwa sura yako.

Ee Bwana, usikie haki, usikilize kilio changu,
Utege sikio lako kwa maombi yangu.
Yasiyotoka katika midomo ya hila. (K)

Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako,
Hatua zangu, hazikuondoshwa.
Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika,
Utege sikio lako ulisikie neno langu. (K)

Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
Bali mimi nikutazame uso wako katika haki.
Niamkapo nishibishwe kwa sura yako. (K)

SOMO 2

2Thes. 2:16 – 3:1 – 5

Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe, na Mungu Baba yetu, aliyetupenda akatupa faraja ya milele na tumaini jema, katika neema, awafariji mioyo yenu, na kuwafanya imara katika kila neno na tendo jema. Hatimaye, ndugu, tuombeeni, neno la Bwana liendelee, na kutukuzwa vile vile kama ilivyo kwenu; tukaokolewe na watu wasio haki, wabaya; maana si wote walio na Imani. Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu. Nasi tumemtumaini Bwana kwa mambo yenu, kwamba mnayafanya tuliyowaagiza, tena kwamba mtayafanya. Bwana awaongoze mioyo yenu mkapate pendo la Mungu, na saburi ya Kristo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Yn. 1:12, 14

Aleluya, aleluya,
Naye neno alifanyika mwili, akakaa kwetu; wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu.
Aleluya.

INJILI

Lk. 20:27 – 18

Baadhi ya Masadukayo, wale wasemao ya kwamba hakuna ufufuo, walimwendea Yesu, wakamwuliza, wakisema, Mwalimu, Musa alituandikia ya kuwa, mtu akifiwa na ndugu yake mwenye mke, lakini hana mtoto, na amtwae huyu mke, ampatie ndugu yake mzao. Basi, kulikuwa na ndugu saba. Wa kwanza alioa mke, akafa hana mtoto; na wa pili akamtwaa yule mke, akafa hana mtoto; hata wa tatu akamwoa, na kadhalika wote saba, wakafa, wasiache watoto. Mwisho akafa yule mke naye. Basi, katika ufufuo atakuwa mke wa yupi? Maana aliolewa na wote saba. Yesu akawaambia, Wana wa ulimwengu huu huoa na kuolewa; lakini , wale wahesabiwao kuwa wamestahili kuupata ulimwengu ule, na kule kufufuka katika wafu, hawaoi wala hawaolewi, wala hawawezi kufa tena; kwa sababu huwa sawasawa na malaika, nao ni wana wa Mungu, kwa vile walivyo wana wa ufufuo. Lakini, ya kuwa wafu hufufuliwa, hata na Musa alionyesha katika sura ya Kijiti, hapo alipomtaja Bwan akuwa ni Mungu wa Ibrahimu, na Mungu wa Isaka, na Mungu wa Yakobo. Naye si Mungu wa wafu, bali wa walio hai; kwa kuwa wote huishi kwake.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Agano la Mungu na Abramu

Mwanzo 15
1 Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana… soma zaidi

a.gif Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala.. soma zaidi

a.gif Mungu ni Muumba vyote maana yake ni nini?

Mungu ni Muumba vyote Maana yake amefanya vitu vyote kwa kutaka tu pasipo kutumia chochote. (2Wamakabayo 7:28, Yoh 1:3).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, NOVEMBA 10, 2019 DOMINIKA YA 32 YA MWAKA C WA KANISA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, NOVEMBA 10, 2019 DOMINIKA YA 32 YA MWAKA C WA KANISA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉AMRI ZA MUNGU

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala inayojibiwa

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Karoli Lwanga

a.gif Masifu ni nini?

Masifu ni sala au wimbo unaomsifu na kumtambua Mungu kuwa Mungu.. soma zaidi

a.gif Hasira ni nini?

Hasira ni kukasirika bure kuonea na kulipiza kisasi.. soma zaidi

a.gif Je, Mungu amejitambulisha pia kwa jina?

Ndiyo, Mungu amejitambulisha pia kwa majina mbalimbali. Katika Agano la Kale jina muhimu kuliko yote liliandikwa “YHWH” yaani, “Mimi Ndimi”. Tangu zamani Wayahudi hawalitamki, hivyo wakilifikia wanasoma kwa kutafsiri, “Bwana”… soma zaidi

a.gif Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote… soma zaidi

a.gif Katika unyonge wetu tutumainie nini?

Katika unyonge wetu tutumainie huruma ya Mungu aliyetutumia Mkombozi hata “dhambi ilipozidi, neema ikawa kubwa zaidi” (Rom 5:20)… soma zaidi

a.gif Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu.. soma zaidi

a.gif Malaika wema kazi yao ni nini?

Malaika wema kazi yao ni kutuombea, kutumwa na Mungu kwetu, na wanatulinda kama Malaika wetu Walinzi. (Ebr 13:2).. soma zaidi

a.gif Hasa Mungu amejifunua kuwa nani?

Hasa Mungu amejifunua kuwa upendo wenyewe… soma zaidi

a.gif Je, kuna viumbe ambavyo tunaviheshimu kwa kumtukuza Mungu?

Ndiyo twamuheshimu Bikira Maria, Malaika na Watakatifu… soma zaidi

a.gif Mambo makuu manne ya mwisho ni yapi?

Mambo hayo ni;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.