MASOMO YA MISA, NOVEMBA 1, 2019 IJUMAA, JUMA LA 30 LA MWAKA SHEREHE YA WATAKATIFU WOTE

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA, NOVEMBA 1, 2019 IJUMAA, JUMA LA 30 LA MWAKA SHEREHE YA WATAKATIFU WOTE

SOMO 1

Ufu. 7:2-4,9-14

Mimi Yohane, niliona malaika mwingine, akipanda kutoka maawio ya jua, mwenye muhuri ya Mungu aliye hai; akawapigia kelele kwa sauti kuu wale malaika wanne waliopewa kuidhuru nchi na bahari, akisema, Msiidhuru nchi, wala bahari, wala miti, hata tutakapokwisha kuwatia muhuri watumwa wa Mungu wetu juu ya vipaji vya nyuso zao. Nikasikia hesabu yao waliotiwa muhuri katika kila kabila ya Waisraeli, watu mia na arobaini na nne elfu.

Baada ya hayo nikaona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao; wakilia kwa sauti kuu wakisema, Wokovu una Mungu wetu aketiye katika kiti cha enzi, na Mwana-kondoo.
Na malaika wote walikuwa wakisimama pande zote za kile kiti cha enzi, na za hao wazee, na za wale wenye uhai wanne, nao wakaanguka kifulifuli mbele ya kile kiti cha enzi, wakamsujudu Mungu, wakisema, Amina; Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu hata milele na milele. Amina. Akajibu mmoja wa wale wazee akiniambia, Je! Watu hawa aliovikwa mavazi meupe ni akina nani? Nao wametoka wapi? Nikamwambia, Bwana wangu, wajua wewe. Akaniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu
_

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 24:1-6 (K) 6

(K) Hiki ndicho kizazi cha wakutafutao, Ee Bwana.

Nchi na vyote viijazavyo ni mali ya Bwana,
Dunia na wote wakaao ndani yake.
Maana ameiweka misingi yake juu ya bahari,
Na juu ya mito ya maji aliithibitisha. (K)

Ni nani atakayepanda katika mlima wa Bwana?
Ni nani atakayesimama katika patakatifu pake?
Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe,
Asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili. (K)

Atapokea Baraka kwa Bwana,
Na haki kwa Mungu wa wokovu wake.
Hiki ndicho kizazi cha wamtafutao,
Wakutafutao uso wako, Ee Mungu wa Yakobo. (K)

_

SOMO 2

1 Yoh. 3:1-3

Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. Wapenzi, sasa tu wana wa Mungu, wala haijadhihirika bado tutakavyokuwa; lakini twajua ya kuwa atakapodhihirishwa, tutafanana naye; kwa maana tutamwona kama alivyo. Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa; kama yeye alivyo mtakatifu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu
_

SHANGILIO

Mt. 11:28

Aleuya, aleluya.
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa
na mizigo, nami nitawapumzisha, asema Bwana.
Aleluya.

_

INJILI

Mt. 5:1-12

Yesu alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjua; akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,

Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Agano la Kale lina vitabu vingapi?

Agano la Kale lina vitabu 46.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu, Umoja

Karibu Tafakari,.. soma zaidi

a.gif Hadhi ya nafsi ya mtu inadai nini kuhusu dhamiri adilifu?

Hadhi ya nafsi ya mtu inadai unyofu wa dhamiri adilifu, yaani upande wa akili na sheria ya Mungu.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, NOVEMBA 1, 2019 IJUMAA, JUMA LA 30 LA MWAKA SHEREHE YA WATAKATIFU WOTE

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, NOVEMBA 1, 2019 IJUMAA, JUMA LA 30 LA MWAKA SHEREHE YA WATAKATIFU WOTE

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA KUMWOMBA MTAKATIFU TERESIA

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala za kila siku

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Gemma Galgani

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

a.gif Mungu aliwahi kujifunua kwa watu gani?

Mungu aliwahi kujifunua kwa wazazi wetu wa kwanza, akaendelea hasa kwa taifa la Israeli, hadi alipomtuma Mwanae ajifanye mtu wa taifa hilo teule… soma zaidi

a.gif Baba Mtakatifu ni nani?

1. Ndiye Askofu Mkuu wa Maaskofu wote.. soma zaidi

a.gif Kujikweza Mbele ya Mungu

Rejea Luka 14:7-24 na Luka 18 :9-18.. soma zaidi

a.gif Mwenyezi Mungu yukoje basi?

Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote… soma zaidi

a.gif Akili ni nini?

Ni mwangaza wa Roho Mtakatifu wa Kutusaidia tumjue zaidi Mungu na Ukamilifu wake na kuwa na Hakika kwamba Mungu peke yake aweza kutuliza roho zetu.. soma zaidi

a.gif Yatupasa kusali lini?

Yatupasa kusali kila siku bila kukata tamaa (Lk 18:1) Sala ndiyo njia pekee ya kutuunganisha na Mungu… soma zaidi

a.gif Shauri ni nini?

Ni utaratibu wa Kuchagua Siku zote mambo yenye kufaa kwa sifs ya Mungu na kwa Wokovu wetu.. soma zaidi

a.gif Kwa nini yatupasa kuwaheshimu Watakatifu?

Kwa sababu hao ni washindi, rafiki wa Mungu na waombezi wetu… soma zaidi

a.gif Katika Amri ya Nne ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa haya;.. soma zaidi

a.gif Neema ya Msaada ni nini?

Neema ya Msaada ni msaada tupatao kwa Roho Mtakatifu kutuongezea nguvu Rohoni tutende mambo mema na tuepuke Mabaya.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.