MASOMO YA MISA, MEI 9, 2019 ALHAMISI: JUMA LA 3 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.


MASOMO YA MISA, MEI 9, 2019 ALHAMISI: JUMA LA 3 LA PASAKA

SOMO 1

Mdo. 8:26-40

Malaika wa Bwana akasema na Filipo, akamwambia, Ondoka ukaende upande wa kusini hata njia ile itelemkayo kutoka Yerusalemu kwenda Gaza; nayo ni jangwa. Naye akaondoka, akaenda; mara akamwona mtu wa Kushi, towashi, mwenye mamlaka chini ya Kandake malkia wa Kushi, aliyewekwa juu ya hazina yake yote; naye alikuwa amekwenda Yerusalemu kuabudu, akawa akirejea, ameketi garini mwake akisoma chuo cha nabii Isaya. Roho akamwambia Filipo, Sogea karibu na gari hili, ukashikamane nalo. Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma chuo cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili,
Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo, na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake amkataye manyoya, vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake. Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa. Ni nani atakayeeleza kizazi chake? Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.
Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? Filipo akafunua kinywa chake, naye, akakianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiri habari njema za Yesu.
Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji; yule towashi akasema, Tazama, maji haya; ni nini kinachonizuia nisibatizwe? Akaamuru lile gari lisimame; wakatelemka wote wawili majini, Filipo na yule towashi; naye akambatiza. Kisha, walipopanda kutoka majini, Roho wa Bwana akamnyakua Filipo, yule towashi asimwone tena; basi alikwenda zake akifurahi.
Lakini Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akahubiri Injili katika miji yote, hata akafika Kaisaria.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 66:8-9, 16-17, 20 (K) 1

(K) Mpigie Mungu kelele za shangwe, nchi yote.

Enyi mataifa, mtukuzeni Mungu wetu,
Itangazeni sauti ya sifa zake;
Aliyeiweka nafsi yetu katika uhai,
Wala hakuuacha mguu wetu usogezwe. (K)

Njoni sikieni, ninyi nyote mnaomcha Mungu,
Nami nitayatangaza aliyonitendea roho yangu.
Nalimwita kwa kinywa changu,
Na sifa kuu zilikuwa chini ya ulinzi wangu. (K)

Na ahimidiwe Mungu asiyeyakataa maombi yangu;
Wala kuniondolea fadhili zake. (K)

SHANGILIO

Yn. 20: 29

Aleluya, aleluya,
Wewe Toma, umesadiki kwa kuwa umeniona, wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Aleluya.

INJILI

Yn. 6:44-51

Yesu aliwaambia Wayahudi: Hakuna mtu awezaye kuja kwangu, asipovutwa na Baba aliyenipeleka; nami nitamfufua siku ya mwisho. Imeandikwa katika manabii, Na wote watakuwa wamefundishwa na Mungu. Basi kila aliyesikia na kujifunza kwa Baba huja kwangu.
Si kwamba mtu amemwona Baba, ila yeye atokaye kwa Mungu; huyo ndiye aliyemwona Baba. Amin, amin, nawaambia, Yeye aaminiye yuna uzima wa milele.
Mimi ndimi chakula cha uzima. Baba zenu waliila mana jangwani; wakafa. Hiki ni chakula kishukacho kutoka mbinguni; mtu akila chakula hiki, ataishi milele. Na chakula nitakachotoa mimi ni mwili wangu, kwa ajili ya uzima wa ulimwengu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Yesu aliweka sakramenti ngapi?

Yesu aliweka sakramenti saba ambazo ni;
1. Ubatizo (Yoh 3:3, Mk. 16:15-16)
2. Kipaimara (Isa 11:2, Mdo 8:14-17)
3. Ekaristi Takatifu (Yoh 6:1-7, 1Kor 11:24-25)
4. Kitubio (Mt 16:18-19; 18:18; Yoh 20:21-23)
5. Mpako Mtakatifu (Mk 6:13, Yak 5:14-15)
6. Daraja Takatifu (Lk 22:21-25; 1Kor 11:24-25)
7. Ndoa (Mwa 2:21-25; Mt 19:3-9).. soma zaidi

a.gif Mungu aliwaamuru nini watu wa kwanza?

Mungu aliwaamuru watu wa kwanza wasile matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya wasije wakafa. (Mw 2:16-17).. soma zaidi

a.gif Je, sala inaweza kumuendea Yesu?

Ndiyo, sala inaweza kumuendea Yesu, Bwana wetu na kaka yetu, aliye hai mbinguni, kama ilivyomuendea na kusikilizwa alipokuwa duniani… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 9, 2019 ALHAMISI: JUMA LA 3 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 9, 2019 ALHAMISI: JUMA LA 3 LA PASAKA

a.gif TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa

Kiwango cha majukumu uliyonayo kinaamua kiwango cha baraka zinazofuatana na wewe… soma zaidi

a.gif Maana ya Kuabudu kwa Mkatoliki

Kuabudu sio kupiga magoti
Ingekuwa ni kupiga magoti basi wanafunzi wanaopewa adhabu ya kupiga magoti mashuleni wangekuwa wanamwabudu mwalimu wao… soma zaidi

a.gif Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba

Chukua Hii
Yaweza
Kukusaidia.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA MBELE YA SAKRAMENTI KUU I

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kwa Furaha Kuu

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu anasubiri sala zako

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Justin mfiadini

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

a.gif Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Kanisa kwa sababu ni yeye aliyemzaa Yesu Kristo ambaye amelianzisha Kanisa… soma zaidi

a.gif Nani anapaswa kusali?

Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Sala ndiyo njia pekee ya kumuunganisha Mwanadamu na Mungu. Tunapaswa kusali Katika hali yoyote. Tunapokuwa katika hali ya neema tunapaswa kusali vivyo hivyo tunapokuwa katika hali ya dhambi tunapaswa kusali… soma zaidi

a.gif Je, watoto wachanga wanaweza kubatizwa?

Ndiyo, watoto wachanga wanaweza kubatizwa kwa sababu hawakatai neema ya Mungu. Wanafunzi wa Yesu walipotaka kuwazuia wasiletwe kwake “alichukizwa sana, akawaambia, ‘Waacheni watoto wadogo waje kwangu, msiwazuie; kwa maana watoto kama hawa ufalme wa Mungu ni wao. Amin, nawaambieni: Yeyote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa” (Mk 10:14-15).
Yeremia aliambiwa,

“Kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa” (Yer 1:5)… soma zaidi

a.gif Watawa ni akina nani?

Watawa ni Waamini, Walei au Maklero waliowekwa wakfu kwa Mungu katika Kanisa kwa ajilli ya wokovu wao na wa dunia:-.. soma zaidi

a.gif Dhambi za uchafu huleta hasara gani?

Huleta hasara hizi;.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu”?

Maria anastahili kuitwa “Mama wa Mungu” kwa sababu Mwana wa milele wa Mungu, ambaye ni Mungu sawa na Baba, alifanyika mtu toka kwake. Akiwa mja mzito alishangiliwa: “Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi?.. soma zaidi

a.gif Ni nani wahudumu wa Sakramenti ya ndoa?

Wahiudumu rasmi wa Sakramenti ya ndoa ni wachumba wenyewe, Padri kama shahidi rasmi wa kanisa. Tena ni lazima ifungwe mbele ya mashahidi wengine wawili… soma zaidi

a.gif Amri ya saba ya Mungu inakataza nini?

Inakataza haya;.. soma zaidi

a.gif Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga.. soma zaidi

a.gif Nani ni shahidi wa kwanza katika Agano Jipya?

Shahidi wa Kwanza ni Mt Stefano.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.