MASOMO YA MISA, MEI 31, 2019: IJUMAA, JUMA LA 6 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, MEI 31, 2019: IJUMAA, JUMA LA 6 LA PASAKA

SIKUKUU YA MAAMKIO YA BIKIRA MARIA

SOMO 1

Rum. 12:9-16

Pendo na lisiwe na unafiki; lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni, mkijitahidi.
Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Furahini pamoja nao wafuraio; lieni pamoja nao waliao. Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Isa. 12:2-6 (K) 6

(K) Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako.

Tazama, Mungu ndiye wokovu wangu;
Nitatumaini wala sitaogopa;
Maana Bwana Yeshova ni nguvu zangu na wimbo wangu;
Naye amekuwa wokovu wangu.
Basi, kwa furaha mtateka maji katika visima vya wokovu. (K)

Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake;
Yatangazeni matendo yake kati ya mataifa,
Litajeni jina lake kuwa limetukuka. (K)

Mwimbieni Bwana; kwa kuwa ametenda makuu;
Na yajulikane haya katika dunia yote.
Paza sauti, piga kelele, mwenyeji wa Sayuni;
Maana Mtakatifu wa Israeli ni mkuu kati yako. (K)

SHANGILIO

Lk. 1:45

Aleluya.
Heri Bikira Maria aliyesadiki ya kuwa aliyoambiwa na Bwana yatatimizwa.
Aleluya.

INJILI

Lk. 1:39-56

Mariamu aliondoka siku hizo, akaenda hata nchi ya milimani kwa haraka mpaka mji mmoja wa Yuda, akaingia nyumbani kwa Zakaria akamwamkia, Elisabeti. Ikawa Elisabeti aliposikia kule kuamkia kwake Mariamu, kitoto kichanga kikaruka ndani ya tumbo lake; Elisabeti akajazwa Roho Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Mtakatifu; akapaza sauti kwa nguvu akasema, Umebarikiwa wewe katika wanawake, naye mzao wa tumbo lako amebarikiwa. Limenitokeaje neno hili, hata mama wa Bwana wangu anijilie mimi? Maana sauti ya kuamkia kwako ilipoingia masikioni mwangu, kitoto kichanga kikaruka kwa shangwe ndani ya tumbo langu. Naye heri aliyesadiki; kwa maana yatatimizwa aliyoambiwa na Bwana.
Mariamu akasema, Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, Na roho yangu imemfurahia Mungu, Mwokozi wangu; kwa kuwa ameutazama unyonge wa mjakazi wake. Kwa maana, tazama, tokea sasa vizazi vyote wataniita mbarikiwa; Kwa kuwa mwenye nguvu amenitendea makuu, na jina lake ni takatifu. Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi kwa hao wanaomcha. Amefanya nguvu kwa mkono wake; Amewatawanya walio na kiburi katika mawazo ya mioyo yao; Amewaangusha wakuu katika ivti vyao vya enzi; na wanyonge amewakweza. Wenye njaa amewashibisha mema, Na wenye mali amewaondoa mikono mitupu. Amemsaidia Israeli, mtumishi wake; Ili kukumbuka rehema zake; Kama alivyowaambia baba zetu, Ibrahimu na uzao wake hata milele. Mariamu akakaa naye kadiri ya miezi mitatu, kisha akarudi kwenda nyumbani kwake.

Neno la Bwana… Sifa kwake Ee Kristu.


a.gif Mwenye kuwaondolea watu dhambi ni nani?

Mwenyezi Mungu pekee yake aweza kuwaondolea watu dhambi. Ndiye aliyewapa Mitume, Maaskofu na Mapadri uwezo wa kuwaondolea watu dhambi (Yoh 20:21-23).. soma zaidi

a.gif Daima Tinakumbushwa kuungama dhambi zetu hata kama ni ndogo kiasi gani

Kulikuwa na vijana wawili walioamua kwenda kwa padri kumwelezea shida zao.
Basi walipofika kwa yule padre, wakamwambia padre, " samahani padre tuko hapa mbele yako kwa kuwa tumejisikia kuwa ni wadhambi ha hivyo tunahitaji kuungama… soma zaidi

a.gif Yesu aliweka makanisa mangapi? Yesu hakufanya makanisa mengi?

Hapana. Yesu alifanya Kanisa moja tuu… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 31, 2019: IJUMAA, JUMA LA 6 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 31, 2019: IJUMAA, JUMA LA 6 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala kwa wenye kuzimia

[Tafakari ya Sasa] 👉Maana ya kubarikiwa

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Picha ya Yesu wa Huruma

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

ni-halali-kwa-bikira-maria-kutuombes.JPG

a.gif Dhamiri adilifu ni nini?

Dhamiri adilifu, iliyo ndani kabisa mwa mtu, ni uamuzi wa akili ambao kwa wakati wake unamuagiza mtu atende mema na kukwepa maovu.. soma zaidi

a.gif Mababu watatu wa Imani Katika Biblia ni wakina nani?

Mababu wa Imani ni Ibrahimu, Isaka na Yakobo.. soma zaidi

a.gif Mashahidi na Wafiadini wa Uganda

Nchi ya Uganda iliwahi kupatwa na dhuluma  dhidi ya  dini, hasa  Ukristo, hususan  madhehebu  ya  Anglikana  na Kanisa Katoliki. Waliouawa katika mazingira ya namna hiyo, wanaitwa wafiadini/mashahidi… soma zaidi

a.gif Yatupasa kusali namna gani?

Yatupasa kusali kwa Unyenyekevu, Ibada, Matumaini na kwa Saburi. Yesu alitufundisha kuhusu kusali kwa kutumia mfano huu;.. soma zaidi

a.gif Ushirika wa Watakatifu ni nini?

Ushirika wa Watakatifu ni:-.. soma zaidi

a.gif Adamu na Eva Walivyotenda dhambi

1 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu. Akamwambia Eva, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani?.. soma zaidi

a.gif Ni nyakati gani zafaa kwa sala?

Nyakati zote zafaa kwa sala hasa:.. soma zaidi

a.gif Muamuzi wa Mwisho ni Mungu

Mungu ndiye Muamuzi;.. soma zaidi

a.gif Maana ya siku ya Jumatano ya Majivu

Wakati umetimia na ufalme wa Mungu umekaribia, tubuni na kuiamini Injili, (Mk 1:15), haya ndiyo maneno ya kwanza ya Yesu ambayo kadri ya Mwinjili Marko yanafungua kazi ya hadhara ya Yesu, kwa maana hiyo kazi ya Yesu inaanza kwa kuwaandaa watu katika toba ili hatimaye, wapate kuukaribia au kuingia katika ufalme wa Mungu… soma zaidi

a.gif Maana ya jina Bikira Maria

Jina asili kwa Kiaramu ni מרים, Maryām lenye maana ya "Bibi"; watafsiri wa kwanza wa Biblia ya Kiebrania wanaojulikana kama Septuaginta (LXX) waliliacha kama lilivyo wakiandika kwa Kigiriki Μαρίαμ, Mariam, au walilifupisha wakiandika Μαρία, Maria… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.