MASOMO YA MISA, MEI 25, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 5 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Wokovu unapatikana wapi?

SOMO 1

Mdo 16:1-10

Siku zile, Paulo alifika Derbe na Listra na hapo palikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Timotheo, mwana wa mwanamke Myahudi aliyeamini; lakini babaye alikuwa Myunani. Mtu huyo alishuhudiwa vema na ndugu waliokaa Listra na Ikonio. Paulo akamtaka huyo afuatane naye, akamtwaa akamtahiri kwa ajili ya Wayahudi waliokuwako pande zile; kwa maana wote walijua ya kuwa babaye ni Myunani. Basi walipokuwa wakipita kati ya miji ile, wakawapa zile amri zilizoamriwa na mitume na wazee walioko Yerusalemu, ili wazishike. Makanisa yakatiwa nguvu katika ile Imani, hesabu yao ikaongezeka kila siku.
Wakapita katika nchi ya Frigia na Galatia, wakikatazwa na Roho Mtakatifu, wasilihubiri lile neno katika Asia. Walipofika kukabili Misia, wakajaribu kwenda Bithinia, lakini Roho wa Yesu hakuwapa ruhusa, wakapita Misia wakatelemka Troa. Paulo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi, na kumwambia, Vuka, uje Makedonia utusaidie. Basi alipo- kwisha kuyaona vale maono, mara tukataka kutoka kwenda Makedonia. kwa kuwa tuliena hakika ya kwamba Mungu ametuita tuwahubiri Habari Njema.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATI KATI

Zab. 100 :1-3, 5 (K) I

(K) Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote. au: Aleluya.

Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yole.
Mtumikieni Bwana kwa furaha.
Njoni mbelc zake kwa kuimba; (K)

Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake:
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)

Kwa kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)

SHANGILIO

Yn. 20-29

Aleluya, aleluya,
Wewe Toma, umesadiki kwa kuwa umeniona, wa heri wale wasioona wakasadiki.
Aleluya,

INJILI

Yn 15 : 18-21

Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Iwapo ulimwengu ukiwachukia, mwajua ya kuwa umenichukia mimi kabla ya kuwachukia ninyi. Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Likumbukeni lile neno nililowaambia, Mtumwa si mkubwa kuliko bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi; ikiwa walilishika neno langu watalishika na lenu. Lakini haya yote watawatenda kwa ajili ya jina langu, kwa kuwa hawamjui yeye aliyenipeleka.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Roho Mtakatifu ni nani?

Roho Mtakatifu ni upendo wa Mungu, nafsi ya tatu ya Utatu Mtakatifu, mwenye Umungu mmoja na Baba na Mwana… soma zaidi

a.gif Kwa nini Yesu alipaa Mbinguni?

Yesu alipaa Mbinguni ili;.. soma zaidi

a.gif Anayeficha kusudi dhambi ya mauti katika ungamo anaondolewa?

Haondolewi, Bali anatenda dhambi kubwa ya kukufuru Sakramenti ya Kitubio. (Mt 7:21-23, Yoh 20:23, Gal 6:7).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 25, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 5 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 25, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 5 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA MBELE YA KITI CHA ENZI CHA MUNGU

[Wimbo Mzuri PA.gif] Tumsifu Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Uzuri wa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Getrudi Mkuu

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

mtu-akifa-nini-hutokea.JPG

a.gif Padri aitwe kwa mgonjwa lini?

Padri aitwe kwa mgonjwa mara inapoonekana Hatari ya Kifo na kamwe isisubiriwe mpaka mgonjwa apoteze fahamu… soma zaidi

a.gif Sifa kuu za Kanisa ni zipi na zinapatikana wapi?

Sifa kuu za Kanisa ni kuwa moja, takatifu, katoliki na la Mitume. Sifa hizo zinalitambulisha kati ya madhehebu mengi Kanisa pekee lililoanzishwa na Yesu kumpitia Mtume aliyembadilishia jina aitwe Petro, yaani Mwamba wa Kanisa lake lisilokoma wala kupotoka kamwe:.. soma zaidi

a.gif Tofauti ya Sala na Maombi

Sala na Maombi vinatofautiana kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Kabla ya Kupokea Ekaristi Takatifu Tunasali sala gani?

Tunasali "Ee Bwana sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona".. soma zaidi

a.gif Aliyeharibu heshima ya mwingine yampasa afanye nini?

Aliyeharibu heshima ya mwingine yampasa kuirudisha kadiri awezavyo… soma zaidi

a.gif Tafakari ya Zaburi 127:1-2

Leo tunatafakari Zaburi ya 127:1-2 kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Sherehe na tarehe ya Kuzaliwa kwa Yesu Kristo

by Fr TITUS AMIGU.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Kanisa linabatiza watoto wadogo?

Kwa sababu wanazaliwa na dhambi ya asili hivyo wanahitaji kuwekwa huru kutoka mamlaka ya yule mwovu na kuingizwa katika ufalme wa uhuru wa wana wa Mungu.. soma zaidi

a.gif Injili ni nini?

Injili ni Habari njema ya wokovu iliyoletwa na Yesu Kristo.. soma zaidi

a.gif Ajali mbaya kuliko zote duniani Kiroho

Hizi ndio ajali mbaya kuliko zote hapa Duniani, japo wengi huziona za kawaida tu, omba usikutane nazo kabisa!.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.