MASOMO YA MISA, MEI 23, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 5 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Vyanzo vya sala za Kikristo

SOMO 1

Mdo. 15:7-21

Wakati wa Mtaguso wa Yerusalemu, baada ya hoja nyingi Petro alisimama, akawaambia, Ndugu zangu, ninyi mnajua ya kuwa tangu siku za kwanza Mungu alichagua miongoni mwenu ya kwamba Mataifa walisikie neno la Injili kwa kinywa changu, na kuliamini. Na Mungu, ajuaye mioyo ya watu, akawashuhudia, akiwapa Roho Mtakatifu vile vile kama alivyotupa sisi; wala hakufanya tofauti kati yetu sisi na wao, akiwasafisha mioyo yao kwa imani. Basi sasa mbona mnamjaribu Mungu na kuweka kongwa juu ya shingo za wanafunzi, ambalo baba zetu wala sisi hatukuweza kulichukua. Bali twaamini kwamba tutaokoka kwa neema ya Bwana Yesu vile vile kama wao.

Basi mkutano wote wakanyamaza, wakawasikiliza Barnaba na Paulo wakiwapasha habari za ishara na maajabu, ambayo Mungu aliyafanya kwa ujumbe wao katika Mataifa. Na hao walipokwisha kunyamaza Yakobo akajibu, akisema, Ndugu zangu, nisikilizeni. Simeoni ametueleza jinsi Mungu hapo kwanza alivyowaangalia Mataifa ili achague watu katika hao kwa ajili ya jina lake. Na maneno ya manabii yapatana na hayo, kama ilivyoandikwa.

Baada ya mambo haya nitarejea, nami nitaijenga tena nyumba ya Daudi iliyoanguka. Nitajenga tena maanguko yake, nami nitaisimamisha; ili wanada- mu waliosalia wamtafute Bwana, na mataifa yote ambao jina langu limetajwa kwao; asema Bwana, ajulishaye hayo tangu milele.

Kwa sababu hiyo mimi naamua hivi; Tusiwata- abishe wale waliomgeukia Mungu katika Mataifa; bali tuwaandikie kwamba wajiepushe na unajisi wa sanamu, na uasherati, na nyama zilizosongolewa, na damu. Kwa maana tangu zamani za kale Musa anao watu wahubirio mambo yake; katika kila mji husomwa kila sabato katika masinagogi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 96:1-3, 10 (K) 3

(K) Wahubirini mataifa habari za utukufu wake.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Mwimbieni Bwana nchi yote.
Mwimbieni Bwana, libarikini jina lake. (K)

Tangazeni wokovu wake siku kwa siku.
Wahubirini mataifa habari za utukufu wake,
Na watu wote habari za maajabu yake. (K)

Semeni katika mataifa, Bwana ametamalaki;
Naam, ulimwengu umethibitika usitikisike,
Atawahukumu watu kwa adili. (K)

SHANGILIO

Lk. 24 : 25-26

Aleluya, aleluya,
Ilimpasa Kristo kupata mateso haya na kuingia katika utukufu wake.
Aleluya.

INJILI

Yn. 15:9-11

Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?

Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha "Mungu Mtawala".. soma zaidi

a.gif Kwa sababu gani cheo cha Padri ni kikubwa sana?

Kwa sababu Padri anashiriki Upadri wa Yesu Kristo na ni mjumbe kati ya Mungu na Mwanadamu.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Visakramenti

Haya ndiyo mambo yanayoulizwa sana kuhusu visakramenti.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 23, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 5 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 23, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 5 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA KUTUBU

[Wimbo Mzuri PA.gif] Salamu Mama Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Maisha ya Kikristo ni sala

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Bakhita

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

BIKIRAMARIA-ALIKUA-NA-WATOTO-WENGINE-AU.JPG

a.gif Sala ya sauti ni nini?

Sala ya sauti ni sala asaliyo mtu au kundi kwa kutamka maneno.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Neema na Rehema

Mafundisho ya Kanisa Katoliki kuhusu Neema na Rehema.. soma zaidi

a.gif Kuimba wakati wa ibada ni kazi ya nani?

Kuimba ni kazi ya kusanyiko lote, yaani ya kila mwamini. Kwaya ziimbishe watu wamwadhimishe Mungu, zisiwaimbie tu na kuwanyima nafasi ya kuimba… soma zaidi

a.gif Tofauti Wakati Wa Kukomunika Wakati Wa Kupokea Mwili Na Damu ya Yesu Kristo

Wakati wa kukomunika Kila mtu anampokea Yesu kwa namna tofauti kulingana na yeye alivyojiandaa, utayari wake, IMANI, na anachokitaka kutoka kwa Yesu… soma zaidi

a.gif Siku Sita za Mungu kuumba Dunia

1 Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi… soma zaidi

a.gif Je Yesu yupo mzima katika Ekaristi Takatifu? Kwa nini tunaabudu Ekaristi Takatifu?

Ndiyo. Ekaristi Takatifu inamuwakilisha Yesu Mwenyewe aliye Mungu na aliyeamua Mwenyewe kuwepo katika Maumbo ya Mkate na Divai.
Ukisoma Yoh 6:51-57 inasema hivi;.. soma zaidi

a.gif Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa sababu gani?

Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa kuzingatia umbile letu, kwamba binadamu ni umoja wa roho na mwili, hivyo anahitaji mwili na hisi zake ili kuingiza chochote rohoni na kutokeza yaliyomo katika roho yake isiyoonekana… soma zaidi

a.gif Je, anayejiunga na Kanisa na kudumu ndani yake ana hakika ya kuingia mbinguni?

Hapana, anayejiunga na Kanisa na kudumu ndani yake lakini haongozwi na Roho Mtakatifu kuishi kadiri ya ubatizo wake atahukumiwa na Mungu vikali zaidi kwa kuchezea neema kubwa hivi… soma zaidi

a.gif Je, nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji?

Ndiyo, nafsi tatu za Mungu zina Umoja hata katika utendaji, kila nafsi akiuchangia kulingana na sifa yake maalumu ndani ya Utatu. Baba Mwenyezi sifa yake ni Uwezo. Mwana kama Neno la Baba sifa yake ni Hekima. Roho kama Pumzi ya uhai ya Baba sifa yake ni Upendo… soma zaidi

a.gif Masomo Ya Leo

Usikose masomo ya misa kwa kila siku hapa.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.