MASOMO YA MISA, MEI 21, 2019: JUMANNE, JUMA LA 5 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

SOMO 1

Mdo. 14 :19-28

Wayahudi walifika toka Antiokia na Ikonio, wakawashawishi makutano hata wakampiga kwa mawe Paulo, wakamburuta nje ya mji, wakidhania ya kuwa amekwisha kufa. Lakini wanafunzi walipokuwa wakimzunguka pande zote, akasimama, akaingia ndani ya mji; na siku ya pili yake akatoka, akaenda zake pamoja na Barnaba mpaka Derbe.
Hata walipokwisha kuhubiri Injili katika mji ule, na kupata wanafunzi wengi, wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawa weka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Wakapita kati ya Pisidia wakaingia Pamfilia. Na baada ya kuhubiri lile neno katika Perge wakatelemka mpaka Atalia. Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza. Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, waka- waeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani. Wakaketi huko wakati usiokuwa mcha che, pamoja na wanafunzi.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 145 :10-13, 21 (K) 12

(K) Watawajulisha watu matendo yake makuu, Na utukufu wa fahari wa zamani zote.
Au: Aleluya.

1. Ee Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako,
Ili kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake. (K)

2. Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. (K)

3. Kinywa changu kitazinena sifa za Bwana;
Wote wenye mwili na walihimidi jina lake
takatifu milele na milele. (K)

SHANGILIO

Ufu. 1:5

Aleluya, aleluya,
Ee Kristo, yu shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.
Aleluya.

INJILI

Yn. 14 : 27-31

Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga. Mlisikia ya kwamba mimi naliwaambia, Naenda zangu, tena naja kwenu. Kama mngalinipenda, mngalifurahi kwa sababu naenda kwa Baba; kwa maana Baba ni mkuu kuliko mimi. Na sasa nimewaambia kabla halijatokea, kusudi litakapotokea mpate kuamini. Mimi sitasema nanyi maneno mengi tena, kwa maana yuaja mkuu wa ulimwengu huu, wala hana kitu kwangu. Lakini ulimwengu ujue ya kuwa nampenda Baba; na kama vile Baba alivyoniamuru; ndivyo nifanyavyo. Ondokeni, twendeni zetu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Je, tunapoadhimisha mafumbo hayo tuko peke yetu?

Hapana, tunapoadhimisha mafumbo hayo hatuko peke yetu, bali tunashiriki ibada ambayo Yesu anamtolea Baba milele… soma zaidi

a.gif Je, Maria amechangia wokovu wetu?

Ndiyo, Maria amechangia wokovu wetu kwa kukubali mpango wote wa Mungu aliyetaka amzae Mwanae, amlee na kumfuata kiaminifu hadi msalabani, aliposhiriki kumtoa kama sadaka ya kutuokoa… soma zaidi

a.gif Kutafuta dhambi maana yake ni nini?

Kutafuta dhambi maana yake ni kujiuliza moyoni dhambi nilizotenda Tangu ungamo la mwisho (Ef 4:17-32).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 21, 2019: JUMANNE, JUMA LA 5 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 21, 2019: JUMANNE, JUMA LA 5 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Uwe na maono

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Margareta Maria Alacoque

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

UJUMBE-UNAVYOMMISI-NDUGU.JPG

a.gif Anayekufuru Sakramenti ya Kitubio yampasa nini?

Yampasa kuziungama tena dhambi zake zote alizotenda tangu ondoleo la mwisho.. soma zaidi

a.gif Je, Kanisa ni muhimu kwa wote?

Ndiyo, Kanisa ni muhimu kwa wote kwa kuwa ndilo ishara na chombo cha umoja wa watu na Mungu na kati yao… soma zaidi

a.gif Ni nani anayetoa Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa?

Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa hutolewa na kuhani tuu yaani Askofu au Padri.. soma zaidi

a.gif Wito wa Katekista ni nini?

Ni wito maalumu kutoka kwa Roho Mtakatifu na ni karama maalumu inayotambuliwa na Kanisa na kufanywa dhahiri kwa mamlaka ya Askofu.. soma zaidi

a.gif Nini maana ya Roho Mtakatifu?

Roho Mtakatifu ni nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu, ni Mungu Halisi sawa na Mungu Baba na Mwana. (Yoh 14:16-17,26).. soma zaidi

a.gif Msimamizi wa ubatizo ana wajibu gani?

Msimamizi wa ubatizo ana wajibu hizi;.. soma zaidi

a.gif Mungu aliumbaje vyote?

Mungu aliumba vyote kwa kutaka tu, bila ya kutumia chochote… soma zaidi

a.gif Mungu ni Roho maana yake ni nini?

Mungu ni Roho maana yake haonekani wala hashikiki. (Lk: 24:39).. soma zaidi

a.gif Watoto wa Nuhu ni wepi?

Watoto wa Nuhu ni Shemu, Hamu na Nefteli.. soma zaidi

a.gif Kanisa Katoliki linavyofundisha kuhusu Yesu

Haya ndiyo mafundisho makuu;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.