MASOMO YA MISA, MEI 20, 2019: JUMATATU, JUMA LA 5 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Mdo. 14:5-18

Siku zile, palipotokea shambulio la watu wa Mataifa na Wayahudi pamoja na wakubwa wao juu yao, kuwatenda jeuri na kuwapiga kwa mawe, wao wakapata habari wakakimbilia Listra na Derbe, mji wa Likaonia, na nchi zilizo kando kando; wakakaa huko, wakiihubiri Injili. Na huko Listra palikuwa na mtu mmoja, dhaifu wa miguu, kiwete tangu tumboni mwa mamaye, ambaye hajaenda kabisa. Mtu huyo alimsikia Paulo alipokuwa akinena; ambaye akamkazia macho na kuona ya kuwa ana imani ya kuponywa, akasema kwa sauti kuu, Simama kwa miguu yako sawasawa. Akasimama upesi akaenda.
Na makutano walipoona aliyoyafanya Paulo wakapaza sauti zao, wakisema kwa Kilikaonia, Miungu wametushukia kwa mifano ya wanadamu. Wakamwita Barnaba, Zeu, na Paulo, Herme, kwa sababu ndiye aliyekuwa mnenaji. Kuhani wa Zeu ambaye hekalu lake lilikuwa mbele ya mji, akaleta ng’ombe na taji za maua hata malangoni, akitaka kutoa dhabihu pamoja na makutano. Walakini mitume Barnaba na Paulo, walipopata habari, wakararua nguo zao, wakaenda mbio wakaingia katika makutano, wakipiga kelele, wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi ni wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo; ambaye zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe. Lakini hakujiacha pasipo ushuhuda, kwa kuwa alitenda mema, akiwapeni mvua kutoka mbinguni, na nyakati za mavuno, akiwashibisha mioyo yenu chakula na furaha. Na kwa maneno hayo wakawazuia makutano kwa shida, wasiwatolee dhabihu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 115 :1-4, 15-16 (K) 1

(K) Ee Bwana, kutukuza usitutukuze sisi, Bali ulitukuze jina lako.

Ee Bwana, kutukuza usitutukuze sisi,
Bali ulitukuze jina lako.
Kwa ajili ya fadhili zako,
Kwa ajili ya uaminifu wako.
Kwa nini mataifa kusema,
Yuko wapi Mungu wao? (K)

Lakini Mungu wctu yuko mbinguni,
Alitakalo lote amelitenda.
Sanamu zao ni fedha na dhahabu,
Kazi ya mikono ya wanadamu. (K)

Na mbarikiwe ninyi na Bwana,
Aliyezifanya mbingu na nchi.
Mbingu ni mbingu za Bwana,
Bali nchi amewapa wanadamu. (K)

SHANGILIO

Col. 3:1

Aleluya, aleluya,
Mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
Aleluya.

INJILI

Yn. 14:21-26

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Yeye aliye na amri zangu, na kuzishika, yeye ndiye anipendaye; naye anipendaye atapendwa na Baba yangu, nami nitampenda na kujidhihirisha kwake. Yuda (siye Iskariote), akamwambia, Bwana, imekuwaje ya kwamba wataka kujidhihirisha kwetu, wala si kwa ulimwengu?
Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Mtu asiyenipenda, yeye hayashiki maneno yangu; nalo neno mnalolisikia silo langu, ila ni lake Baba aliyenipeleka. Hayo ndiyo niliyowaambia wakati nilipokuwa nikikaa kwenu. Lakini huyo Msaidizi, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atampeleka kwa jina langu, atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Moyo Mtakatifu wa Yesu unawakilisha nini?

Moyo Mtakatifu wa Yesu unawakilisha Upendo na Huruma ya Mungu isiyo na mipaka… soma zaidi

a.gif Malaika Walinzi wanatutendea nini?

Malaika walinzi hutupenda, hutuongoza, na kutulinda roho na mwilini (Zab 90:11).. soma zaidi

a.gif Dhambi ya asili ndio nini?

Dhambi ya asili ambayo binadamu wote wanazaliwa nayo, ni hali ya kukosa utakatifu na hali ya asili ya urafiki na Mungu.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 20, 2019: JUMATATU, JUMA LA 5 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 20, 2019: JUMATATU, JUMA LA 5 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Wanaruka kwa shangwe

[Tafakari ya Sasa] 👉Mwenendo wa Roho

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Gemma Galgani

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

BIKIRA-MARIA-KUITWA-MAMA-WA-MUNGU-KWA-NINI.JPG

a.gif Fadhila inayoondoa uvivu ni ipi?

Fadhila inayoondoa uvivu ni utendaji.. soma zaidi

a.gif Kujinyima ni nini?

Kujinyima ni kujikatalia kitu ukipendacho mfano nyama, pombe, sigara, muziki, safari, maongezi n.k… soma zaidi

a.gif Kanisa ni Takatifu maana yake ni nini?

Kanisa ni Takatifu maana yake:-.. soma zaidi

a.gif Je, Baada ya kupokea Sakramenti ya Kipaimara ni lazima kuendelea kujifunza Dini?

Ndiyo, Baada ya kupokea Sakramenti ya Kipaimara ni lazima kuendelea kujifunza Dini ili tuweze kuelewa na kulinda Imani yetu na kutumia vema neema ya Kipaimara… soma zaidi

a.gif Kuungama ni kufanya nini?

Kuungama ni kumwambia Padri wazi wazi dhambi zako ulizotenda, zipi na ngapi ili upate maondoleo… soma zaidi

a.gif MAANA YA SALA KWA MKRISTO

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Watu wote wanapaswa kusali, wema na wabaya. Inatupasa kusali kila siku bila kukata tama kwa ibada, kwa matumaini na kwa saburi. Kama mfano Yesu Alitufundisha sala ya Baba yetu.
Yatupasa kuwaombea wengine, watu wote wenye shida wakosefu na hata maadui zetu, vilevile tumtolee Mungu shukrani kila wakati na hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu… soma zaidi

a.gif Kwa nini Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai? Watu na mitume hawakuwa wanasali kumuomba yeye

Bikira Maria hakuwa anaombwa akiwa hai kwa sababu alikua bado hajatukuzwa na kupewa cheo cha Umalkia wa Mbinguni… soma zaidi

a.gif Kwa kuwa tumekombolewa kwa damu azizi ya Mwana wa Mungu, tunaonywa vipi?

Kwa kuwa tumekombolewa kwa damu azizi ya Mwana wa Mungu, tunaonywa kwamba,.. soma zaidi

a.gif Nani Mkombozi wa watu wote?

Mkombozi wa watu wote ni Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, Bwana wetu… soma zaidi

a.gif Mafundisho na mapokeo Katika Kanisa Katoliki yanapopatikana kwenye Biblia

JE IMANI AU MAPOKEO YA KANISA KATOLIKI YANAPATIKANA KATIKA BIBLIA?.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.