MASOMO YA MISA, MEI 19, 2019: DOMINIKA YA 5 YA PASAKA, MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

MWANZO:

Zab. 98:1-2

Mwimbieni Bwana wimbo mpya, kwa maana ametenda mambo ya ajabu; machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake, aleluya.

SOMO 1

Mdo. 14:2lb-27

Paulo na Barnaba wakarejea mpaka Listra na Ikonio na Antiokia, wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika ile Imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya dhiki nyingi. Na walipokwisha kuwachagulia wazee katika kila kanisa, na kuomba pamoja na kufunga, wakawaweka katika mikono ya Bwana waliyemwamini.
Wakapita kati ya Pisidia wakaingia Pamfilia. Na baada ya kuhubiri lile neno katika Perge wakatelemka mpaka Atalia. Na kutoka huko wakaabiri kwenda Antiokia. Huko ndiko walikoombewa neema ya Mungu kwa ile kazi waliyokwisha kuitimiza.
Hata walipofika wakalikutanisha kanisa, wakawaeleza mambo yote aliyoyafanya Mungu pamoja nao, na ya kwamba amewafungulia Mataifa mlango wa imani.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KAT1KATI

Zab. 145:8-13, (K) 1

(K) Ee Mungu wangu, Mfalme, nitakutukuza, Nitalihimidi jina lako milele na milele.

1. Bwana ana fadhili, ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema,
Bwana ni mwema kwa watu wote,
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. (K)

2. Bwana, kazi zako zote zitakushukuru,
Na wacha Mungu wako watakuhimidi.
Wataunena utukufu wa ufalme wako,
Na kuuhadithia uweza wako. (K)

3. Hi kuwajulisha watu matendo yake makuu,
Na utukufu wa fahari ya ufalme wake.
Ufalme wako ni ufalme wa zamani zote,
Na mamlaka yako ni ya vizazi vyote. (K)

SOMO 2

Ufu 21:1-5;

Siku ile, mimi, Yohane, niliona mbingu mpya na nchi mpya; kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zimekwisha kupita, wala hapana bahari tena. Nami nikauona mji ule mtakatifu, Yerusalemu mpya, ukishuka kutoka mbinguni kwa Mungu, umewekwa tayari, kama bibi-arusi aliyekwisha kupambwa kwa mumewe. Nikasikia sauti kubwa kutoka katika kile kiti cha enzi ikisema, Tazama, maskani ya Mungu ni pamoja na wanadamu, naye atafanya maskani yake pamoja nao, nao watakuwa watu wake. Naye Mungu mwenyewe atakuwa pamoja nao. Naye atafuta kila chozi katika macho yao. wala mauti haitakuwapo tena; wala maombolezo wala kilio, wala maumivu hayatakuwapo tena; kwa kuwa mambo ya kwanza yamekwisha kupita. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Yn. 13 :3

Aleluya, aleluya,
Bwana alisema: Amri mpya nawapa, mpendane, kama vile nilivyowapenda ninyi.
Aleluya.

INJILI

Yn. 13 :31-33a, 34-35

Yuda alipokwisha kutoka, Yesu alisema, Sasa ametukuzwa Mwana wa Adamu, naye Mungu ametukuzwa ndani yake. Mungu naye atamtukuza ndani ya nafsi yake; naye atamtukuza mara. Enyi watoto wadogo, bado kitambo kidogo nipo pamoja nanyi. Amri mpya nawapa, Mpendane. Kama vile nilivyowapenda ninyi, nanyi mpendane vivyo hivyo. Hivyo watu wote watatambua ya kuwa ninyi mmekuwa wanafunzi wangu, mkiwa na upendo ninyi kwa ninyi.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu.


a.gif Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu lini?

Ubatizo unatolewa pia kwa maji machache tangu mwanzo. Kutokana na umuhimu wa sakramenti hiyo Yesu ametuagiza twende kubatiza watu duniani kote… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa inaadhimishwaje?

Inaadhimishwa kwa Padre kumuombea mgonjwa, kumuwekea mikono na kumpaka mafuta katika panda la uso na viganja vya mikono; kwa kutumia mafuta aliyobariki Askofu siku ya Alhamisi kuu… soma zaidi

a.gif Vizuizi vya ndoa ni vipi?

Vizuizi vya ndoa ni;
1. Upungufu wa umri
2. Uhanithi
3. Ndoa awali halali
4. Tofauti za dini au upagani.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 19, 2019: DOMINIKA YA 5 YA PASAKA, MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 19, 2019: DOMINIKA YA 5 YA PASAKA, MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Sali daima

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu John Fisher

Mama-Bikira-Maria.jpg

a.gif Neno Bwana lina maana gani katika Biblia?

Neno Bwana Katika Biblia linamaanisha "Mungu Mtawala".. soma zaidi

a.gif Nani ni Mitume wa Mataifa?

Mitume wa mataifa ni Paulo na Barnaba.. soma zaidi

a.gif Dhambi za uchafu huleta hasara gani?

Huleta hasara hizi;.. soma zaidi

a.gif Huruma ya Yesu Kristo kwa mwenye dhambi

Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio wakati ambao Yesu anakua karibu na mtu sana hata kuzidi wakati mwingine wowote.
Wakati mtu anapoanguka dhambini ndio Yesu anakua karibu zaidi, lakini tatizo ni kwamba huo ni wakati ambao mtu hawezi kutambua uwepo wa Yesu. Neno moja tuu la Matumaini na Upendo wakati huo linaweza kumfungua mtu na kumbadilisha… soma zaidi

a.gif Kilindi cha Huruma ya Mungu

Habari njema ni kwamba Yesu sasa anakuja kwako Kama Bwana wa Huruma, Mwalimu na Rafiki Mwema Akupendaye, Angalia Usichelewe Wakati akija Kama Hakimu asikukute bado huna ushirika nae na hujui haki na hukumu yake. Wakati ndo huu wa kukimbilia Huruma na Upendo wake wa Bure Kwako... soma zaidi

a.gif Kwa kusudi gani Yesu alianzisha Kanisa?

Yesu alianzisha Kanisa kwa nia ya Kuutangaza na kuueneza Ufalme wa Mungu (Mt 28:19-20).. soma zaidi

a.gif Kwa ajili gani Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu?

Mwana wa Mungu (Yesu) alijifanya mtu kwa ajili yetu wanadamu na wokovu wetu ili atupatanishe na Mungu na kutushirikisha tabia ya umungu. (2Pet, 1:4).. soma zaidi

a.gif Je, Ubatizo ni lazima kwa wokovu?

Ndiyo, nilazima kwa wokovu kwa wale ambao wametangaziwa injili na wanasifa ya kuomba Sakramenti hiyo.. soma zaidi

a.gif Majilio ni nini?

Majilio ni kipindi cha Dominika nne cha kujiandaa na Sherehe ya Kuzaliwa Bwana wetu Yesu Kristo, yaani NOELI… soma zaidi

a.gif Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni nini?

Kusadiki kwa Roho Mtakatifu maana yake ni kusadiki kwa nafsi ya Tatu ya Utatu Mtakatifu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.