MASOMO YA MISA, MEI 17, 2019: IJUMAA, JUMA LA 4 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, Mungu amegawanyika sehemu tatu?


MASOMO YA MISA, MEI 17, 2019: IJUMAA, JUMA LA 4 LA PASAKA

SOMO 1

Mdo. 13:26-33

Paulo alisimama akawapungia mkono, akasema: Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa. Kwa maana wakaao Yerusalemu, na wakuu wao, kwa kuwa hawakumjua yeye, wala maneno ya manabii yanayosomwa kila sabato, wameyatimiza kwa kumhukumu. Na ijapokuwa hawakuona sababu ya kumfisha wakamwomba Pilato auawe. Hata walipokwisha kumaliza yote aliyoandikiwa, wakamtelemsha katika ule mti, wakamweka kaburini. Lakini Mungu akamfufua katika wafu; akaonekana siku nyingi na wale waliopanda naye kutoka Galilaya hata Yerusalemu, ambao sasa ndio walio mashahidi wake mbele ya watu.
Na sisi tunawahubiri habari njema ya ahadi ile waliyopewa mababa, ya kwamba Mungu amewatimizia watoto wetu ahadi hiyo, kwa kumfufua Yesu kama ilivyoandikwa katika Zaburi ya pili, Wewe ndiwe Mwanangu, mimi leo nimekuzaa.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 2:6-11 (K) 7

(K) Ndiwe Mwanangu, Mimi leo nimekuzaa.
Au: Aleluya.

Nami nimemweka mfalme wangu
Juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.
Nitaihubiri amri; Bwana aliniambia,
Ndiwe mwanangu, Mimi leo nimekuzaa. (K)

Uniombe, nami nitakupa mataifa kuwa urithi wako,
Na miisho ya dunia kuwa milki yako.
Utawaponda kwa fimbo ya chuma,
Na kuwavunja kama chombo cha mfinyanzi. (K)

Na sasa, enyi wafalme, fanyeni akili,
Enyi waamuzi wa dunia, mwadibiwe.
Mtumikieni Bwana kwa kicho,
Shangilieni kwa kutetemeka. (K)

SHANGILIO

Yn. 20: 29

Aleluya, aleluya,
Wewe Toma, umesadiki kwa kuwa umeniona, wa heri wale wasioona, wakasadiki.
Aleluya.

INJILI

Yn. 14:1-6

Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Msifadhaike mioyoni mwenu; mnamwamini Mungu, niaminini na mimi. Nyumbani mwa Baba yngu mna makao mengi; kama sivyo, ningaliwaambia, maana naenda kuwaandalia mahali. Basi mimi nikienda na kuwaandalia mahali, nitakuja tena niwakaribishe kwangu; ili nilipo mimi, nanyi mwepo. Nami niendako mwaijua njia.
Tomaso akamwambia, Bwana, sisi hatujui uendako; nasi twaijuaje njia?
Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Kwa nini Mungu aliumba ulimwengu?

Mungu aliumba ulimwengu ili adhihirishe utukufu wake na kutushirikisha wema, ukweli na uzuri wake.. soma zaidi

a.gif Sikukuu Kubwa Kupita zote Katika Kanisa ni ipi?

Sikukuu Kubwa Kupita zote Katika Kanisa ni PASAKA.. soma zaidi

a.gif Tumeumbwa kwa sura na mfano wa Mungu maana yake ni nini?

Tumeumbwa kwa mfano na sura ya Mungu maana yake tuna roho zenye akili na utashi yaani uwezo wa kutofautisha mema namabaya, na zitakazoishi milele… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 17, 2019: IJUMAA, JUMA LA 4 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 17, 2019: IJUMAA, JUMA LA 4 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwenye Huruma

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

a.gif Ni fadhila gani inayoondoa ubahili?

Fadhila inayoondoa ubahili ni ukarimu.. soma zaidi

a.gif Utafuteje dhambi wakati wa kujiandaa kuungama?

Tafuta dhambi kwa njia hizi.. soma zaidi

a.gif Rehema kamili ni nini?

Rehema kamili ni msamaha wa kufutiwa adhabu zote za muda za dhambi.. soma zaidi

a.gif Tabernakulo ni nini?

Tabernakulo ni mahali Patakatifu anapokaa Yesu wa Ekaristi siku zote.. soma zaidi

a.gif Je, divai (pombe) ni halali?

Ndiyo, divai ni halali, mradi itumike kwa kiasi isije ikaleta madhara… soma zaidi

a.gif Tushiriki mafumbo hayo mara ngapi?

Tushiriki mafumbo hayo kadiri ya umbile la kila mojawapo. Kuna “ubatizo mmoja” (Ef 4:5) kwa sababu ni kuzaliwa upya “kwa maji na kwa Roho” (Yoh 3:5), jambo lisiloweza kurudiwa… soma zaidi

a.gif Katika hukumu zake dhamira ifuate nini?

Katika hukumu zake dhamira ifuate daima Injili, Amri za Mungu na za Kanisa na wajibu zetu… soma zaidi

a.gif Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu ngapi?

Litrujia ya Ekaristi ina sehemu kuu tatu.. soma zaidi

a.gif Akili ni nini?

Ni mwangaza wa Roho Mtakatifu wa Kutusaidia tumjue zaidi Mungu na Ukamilifu wake na kuwa na Hakika kwamba Mungu peke yake aweza kutuliza roho zetu.. soma zaidi

a.gif Motoni ni nini?

Motoni ni makao mabaya kwa Shetani walaaniwa wakaapo mbali na Mungu wakiteswa milele. (Mt 25:41, Mik 9:42-43, 1Yoh 14:15).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.