MASOMO YA MISA, MEI 16, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 4 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, MEI 16, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 4 LA PASAKA

SOMO 1

Mdo. 13:13-25

Paulo na wenziwe wakang’oa nanga wakasafiri kutoka Pafo, wakafika Perge katika Pamfilia. Yohane akawaacha akarejea Yerusalemu. Lakini wao wakatoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi. Kisha, baada ya kusomwa torati na chuo cha manabii, wakuu wa sinagogi wakatuma mtu kwao, na kuwaambia, Ndugu, kama mkiwa na neno la kuwafaa watu hawa lisemeni.
Paulo akasimama, akawapungia mkono, akasema, Enyi waume wa Israeli, nanyi mnaomcha Mungu, sikilizeni. Mungu wa watu hawa Israeli aliwachagua baba zetu, akawatukuza watu hao, walipokuwa wakikaa kama wageni katika nchi ya Misri, na kwa mkono ulioinuliwa akawatoa, akawaongoza.na kwa muda wa miaka kama arobaini akawavumilia katika jangwa. Na alipokwisha kuwaharibu mataifa saba katika nchi ya Kanaani akawapa nchi yao iwe urithi kwa muda wa miaka kama mia nne na hamsini; baada ya hayo akawapa waamuzi hata zamani za nabii Samweli. Hatimaye wakaomba kupewa mfalme; Mungu akawapa Sauli mwana wa Kishi, mtu wa kabila ya Benyamini, kwa muda wa miaka arobaini. Na alipokwisha kumwondoa huyo, akamwinua DAudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote. Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi; Yohane alipokuwa amekwisha kuwahubiri watu wote wa Israeli habari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake. Naye Yohane alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambaye mimi sisitahili kumlegezea viatu vya miguu yake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 89:1-2, 20-21, 26-27 (K) 1

(K) Fadhili zako, ee Bwana, nitaziimba milele.

Kwa kinywa change
Nitavijulisha vizazi vyote uaminifu wako.
Maana nimesema, FAdhili zitajengwa milele;
Katika mbingu utauthibitisha uaminifu wako. (K)

Nimemwona Daudi, mtumishi wangu,
Nimempaka mafuta yangu matakatifu.
Ambaye mkono wangu utakuwa thabiti kwake,
Na mkono wangu utamtia nguvu. (K)

Yeye ataniita, Wewe baba yangu,
Mungu wangu na mwamba wa wokovu wangu.
Nami nitamjalia kuwa mzaliwa wangu wa kwanza,
Kuwa juu sana kuliko wafalme wa dunia. (K)

SHANGILIO

Yn. 10:27

Aleluya, aleluya.
Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, wao wanifuata.
Aleluya.

SHANGILIO

Yn. 10:27

Aleluya, aleluya,
Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, wao wanifuata.
Aleluya.

INJILI

Yn. 13:16-20

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Amin, amin, nawaambia ninyi, Mtumwa si mkuu kuliko bwana wake; wala mtume si mkuu kuliko yeye aliyempeleka.
Mkiyajua hayo, heri ninyi mkiyatenda. Sisemi habari za ninyi nyote; nawajua wale niliowachagua; lakini andiko lipate kutimizwa, aliyekula chakula change ameniinulia kisigino chake.
Tangu sasa nawaambia kabla hayajatukia, ili yatakapotukia mpate kuamini ya kuwa mimi ndiye. Amin, amin, nawaambieni, Yeye ampokeaye mtu yeyote nimpelekaye, anipokea mimi; naye anipokeaye mimi ampokea yaye aliyenipeleka.

Neno la Bwana… Sifa kwako Eee Kristo.


a.gif Je, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu (Watakatifu)?

Ndiyo, sala inaweza kuwaendea Mama na marafiki wa Yesu, walioungana naye kuwa mwili mmoja, wasiweze kutenganishwa na chochote… soma zaidi

a.gif Ubatizo ni nini?

Ubatizo ni Sakramenti inayotuwezesha kuzaliwa mara ya pili kwa Maji na Roho Mtakatifu, ni mlango (Kiingilio) kwa Sakramenti nyingine zote na ni ufunguo wa uzima wa milele. (Yoh 3:3, Mt28:19).. soma zaidi

a.gif Je, tuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu?

Hatuna ruhusa ya kuwaabudu Watakatifu tunawaheshimu tu… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, MEI 16, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 4 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, MEI 16, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 4 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉AMRI ZA KANISA

[Wimbo Mzuri PA.gif] Bwana ni ngome yangu

[Tafakari ya Sasa] 👉Uhuru na Amani ya Moyoni

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Maria Goretti

BIKIRA-MARIA-NI-KAMA-BAHASHA-TUU.JPG

a.gif Abramu na Loti Watengana

1 Abramu akapanda kutoka Misri, yeye, na mkewe, na kila alichokuwa nacho, na Lutu pamoja naye, mpaka kusini… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Ubatizo yatuletea nini?

Sakramenti ya Ubatizo yatuletea;
1. Maondoleo ya dhambi ya asili
2. Maondoleo ya dhambi zote za binafsi na adhabu zake
3. Neema ya Utakaso kwa mara ya kwanza
4. Yatutia alama isiyofutika (1Kor 6:11, 12:13).. soma zaidi

a.gif Tafakari ya neno la Mungu Luka 16

Tafakari ya Leo;.. soma zaidi

a.gif Masomo ya leo Kanisani

Masomo ya Misa.. soma zaidi

a.gif Kanisa ni Takatifu maana yake ni nini?

Kanisa ni Takatifu maana yake:-.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya ubatizo ni nini?

Sakramenti ya Ubatizo ni Sakramenti yenye kuondoa dhambi ya asili pamoja na dhambi nyingine zote tulizotenda, kufufua roho zetu kwa kututia uzima wa Mungu, Kutuandika Wakristu Watoto wateule wa Mungu na wa Kanisa… soma zaidi

a.gif Upendo, Huruma, Rehema na Neema za Mungu

Mungu ni Mwingi wa Rehema, Huruma, Upendo na Neema… soma zaidi

a.gif Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni vipi?

Kitabu cha kwanza na cha mwisho katika Agano Jipya ni.. soma zaidi

a.gif Je yatupasa kufanya kazi?

Ndiyo, kwa sababu:.. soma zaidi

a.gif Je, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani?

Ndiyo, Yatupasa kumtolea Mungu shukrani kila wakati hasa kwa kuadhimisha Ekaristi Takatifu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.