MASOMO YA MISA, MEI 14, 2019: JUMANNE YA 4 YA PASAKA

Tumsifu Yesu Kristu…

Karibu tena katika Website yako uipendayo ya Wakatoliki yenye mambo mengi kuhusu Imani na Mafundisho ya Kikatoliki. Kama una wasiwasi kuhusu Imani ya Kanisa Katoliki nimekuandalia makala maalumu ya kukufunulia Ukweli hapa>>.

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandikia makala nzuri inayopendwa kuhusu; Picha ya Yesu wa Huruma, kwa sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

MASOMO YA MISA, MEI 14, 2019: JUMANNE YA 4 YA PASAKA.

Unaweza pia kupokea makala zote mpya zinazopostiwa hapa kwenye email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo.

Endelea kuelimika na kubarikiwa kila siku unapotembelea tovuti hii.

MASOMO YA MISA, MEI 14, 2019: JUMANNE YA 4 YA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

SIKUKUU YA MT. MATHIA, MTUME

SOMO 1

Mdo. 1:15-17, 20-26

Siku zile Petro alisimama kati ya ndugu zake (jumala ya majina ilipata mia na ishirini), akasema, Ndugu, ilipasa andiko litimizwe, alilolinena Roho Mtakatifu zamani kwa kinywa cha Daudi. katika habari za Yuda aliyewaongoza wao waliomkamata Yesu, kwa sababu alikuwa amehesabiwa pamoja na sisi, akapata sehemu ya huduma hii. Kwa maana imeandikwa katika chuo cha Zaburi, Kikao chake na kiwe ukiwa,

Wala asiwepo mtu mwenye kukaa humo; tena, Usimamizi wake autwae mwingine. Basi katika watu waliofuatana nasi wakati wote Bwana Yesu alipokuwa akiingia na kutoka kwetu, kuanza tangu ubatizo wa Yohane, hata siku ile alipochukuliwa kwetu kwenda juu, inapasa mmoja wao awe shahidi wa kufufuka kwake pamoja nasi.

Wakaweka wawili, Yusufu, aitwaye Barsaba, aliyekuwa na jina la pili Yusto, na Mathiya. Kisha wakaomba, wakasema, Wewe, Bwana, ujuaye mioyo ya watu wote, tuonyeshe ni nani uliyemchagua katika hawa wawili, ashike mahali katika huduma hii na utume huu, alioukosa Yuda, aende zake mahali pake mwenyewe. Wakawapigia kura; kura ikamwangukia Mathiya; naye akahesabiwa kuwa pamoja na mitume kumi na mmoja.

W1MBO WA KATI KATI

Zab. 113:1-8 (K) 8

(K) Amketishe pamoja na wakuu, pamoja na wakuu wa watu wake. au: Aleluya.

Aleluya.
Enyi watumishi wa Bwana, sifuni,
Lisifuni jina la Bwana.
Jina la Bwana lihimidiwe
Tangu leo na hata milele. (K)

Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la Bwana husifiwa.
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu. (K)

Ni nani aliye mfano wa Bwana,
Mungu wetu aketiye juu;
Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani? (K)

Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani.
Amketishe pamoja na wakuu,
Pamoja na wakuu wa watu wake. (K)

SHANGILIO

Yn. 15 :16

Aleluya, aleluya, Ni mimi niliyewachagua ninyi, nikawaweka mwende mkazae matunda, na matunda yenu yapate kukaa. Aleluya.

INJILI

Yn. 15:9-17

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Kama vile Baba alivyonipenda mimi, nami nilivyowapenda ninyi, kaeni katika pendo langu. Mkizishika amri zangu, mtakaa katika pendo langu; kama vile mimi nilivyozishika amri za Baba yangu na kukaa katika pendo lake. Hayo nimewaambia, ili furaha yangu iwe ndani yenu, na furaha yenu itimizwe.

Amri yangu ndiyo hii, Mpendane, kama nilivyowapenda ninyi. Hakuna aliye na upendo mwingi kuliko huu, wa mtu kuutoa uhai wake kwa ajili ya rafiki zake. Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo. Siwaiti tena watumwa; kwa maana mtumwa hajui atendalo bwana wake; lakini ninyi nimewaita rafiki; kwa kuwa yote niliyoyasikia kwa Baba yangu nimewaarifu. Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. Haya nawaamuru ninyi, mpate kupendana.

Neno la Bwana………sifa kwako Ee Kristu.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 14, 2019: JUMANNE YA 4 YA PASAKA. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

Ikiwemo Makala hii ya MASOMO YA MISA, MEI 14, 2019: JUMANNE YA 4 YA PASAKA, makala nyingine zinazosomwa sana ni kama ifuatavyo;

β€’ Mtume Thoma, isome hapa

β€’ Ajali mbaya kuliko zote duniani Kiroho, isome hapa

β€’ DOMINIKA YA UTATU MTAKATIFU, isome hapa

β€’ Ahadi 15 za Rozari Takatifu, isome hapa

β€’ Imani ni cheti cha Kuweza kupata yote, isome hapa

β€’ TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa, isome hapa

β€’ Maana ya Kuabudu kwa Mkatoliki, isome hapa

β€’ Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba, isome hapa

β€’ Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?, isome hapa

β€’ Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha, isome hapa

Ujumbe wangu kwako kwa sasa wa Kutafakari

"Mungu ni rahisi sana kupatikana. Ugumu ni njia ya Kumtafuta Mungu na namna ya kumuishi Mungu. Hapa ndipo watu wengi wanashindwa."

Mungu Akubariki Daima. Tukumbukane katika sala.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 14, 2019: JUMANNE YA 4 YA PASAKA, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Dismas-Mtakatifu.jpg

Mtakatifu wa Sasa
Leo tunatafakari na kujifunza kutoka kwa Dismas Mtakatifu.
Soma zaidi kuhusu Dismas Mtakatifu hapa.

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..

.

.

IMG_20180109_192035.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Sifa za Sala yeyote. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!