MASOMO YA MISA, MEI 13, 2019: JUMATATU, JUMA LA 4 LA PASAKA

Tumsifu Yesu Kristu…

Karibu tena katika Website yako uipendayo ya Wakatoliki yenye mambo mengi kuhusu Imani na Mafundisho ya Kikatoliki. Kama una wasiwasi kuhusu Imani ya Kanisa Katoliki nimekuandalia makala maalumu ya kukufunulia Ukweli hapa>>.

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandikia makala nzuri inayopendwa kuhusu; Kanuni za kuishi maisha ya ushindi na baraka, kwa sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

MASOMO YA MISA, MEI 13, 2019: JUMATATU, JUMA LA 4 LA PASAKA.

Unaweza pia kupokea makala zote mpya zinazopostiwa hapa kwenye email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo.

Endelea kuelimika na kubarikiwa kila siku unapotembelea tovuti hii.

MASOMO YA MISA, MEI 13, 2019: JUMATATU, JUMA LA 4 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO LA 1

Mdo 11:1-18

Siku zile, mitume na ndugu waliokuwako katika Uyahudi wakapata habari ya kwamba watu wa Mataifa nao wamelipokea neno la Mungu. Na Petro alipopanda kwenda Yerusalemu, wale walio wa tohara wakashindana naye, wakisema, uliingia kwa watu wasiotahiriwa ukala nao.
Petro akaanza kuwaeleza kwa taratibu, akasema, Nalikuwa katika mji wa Yafa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kinashuka, kama nguo kubwa inatelemshwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikia. Nikakitazama sana, nikifikiri, nikaona wanyama wan chi wenye miguu mine, na wanyama wa mwituni, nao watambaao, na ndege wa angani. Nikasikia na sauti ikiniambia, Ondoka, Petro, ukachinje ule. Nikasema, Hasha, Bwana, kwa maana kitu kilicho kichafu au kilicho najisi hakijaingia kabisa kinywani mwangu. Sauti ikanijibu mara ya pili kutoka mbinguni, Alivyovitakasa Mungu, usivinene wewe najisi. Jambo hili likatendeka mara tatu, kisha vitu vyote vikavutwa tena juu mbinguni.
Na tazama, mara hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba tuliyokuwamo waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria. Roho akaniambia nifuatane nao, nisione tashwishwi. Ndugu hawa sita nao wakaenda nami, tukaingia katika nyumba ya mtu yule; akatueleza jinsi alivyomwona malaika aliyesimama nyumbani mwake na kumwambia, Tuma watu kwenda Yafa ukamwite Simoni aitwaye Petro, atakayekuambia maneno ambayo yatakuokoa, wewe na nyumba yako yote.
Ikawa nilipoanza kunena, Roho Mtakatifu akawashukuia kama alivyotushukia sisi mwanzo. Nikalikumbuka neno lile la Bwana, jinsi alivyosema, Yohane alibatiza kwa maji kweli, bali ninyi mtabatiza kwa Roho Mtakatifu. Basi ikiwa Mwenyezi Mungu amewapa wao karama ile ile aliyotupa sisi tuliomwamini Bwana Yesu Kristo, mimi ni nani niweze kumpinga Mungu?
Waliposikia maneno haya wakanyamaza, wakamtukuza Mungu, wakisema, Basi, Mungu amewajalia hata mataifa nao toba lilitalo uzima.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 42:1-2, 43:2-3 (K) 42:2

(K) Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai.
Au Aleluya.

Kama ayala aioneavyo shauku mito ya maji,
Vivyo hivyo nafsi yangu inakuonea shauku, ee Mungu. (K)

Nafsi yangu inamwonea kiu Mungu, Mungu aliye hai,
Lini nitakapoikuja nionekane mbele za Mungu? (K)

Niletewe nuru yako na kweli yako ziniongoze,
Zinifikishe kwenye mlima wako mtakatifu na hata maskani yako. (K)

Hivyo nitakwenda madhabahuni mwa Mungu,
Kwa Mungu aliye furaha yangu na shangwe yangu;
Nitakusifu kwa kinubi, ee Mungu, Mungu wangu. (K)

SHANGILIO

Ufu. 1:5

Aleluya, aleluya,
Ee Kristo, yu shahidi aliye mwaminifu mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia.
Aleluya.

INJILI

Yn. 10:1-10

Yesu aliwaambia Wayahudi: Amin, amin, nawaambieni, Yeye asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni mwivi naye ni mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo wake wote, huwatangulia; na awatoapo nje kondoo wake wote, huwatangulia; na wale kondoo humfuata, kwa maana waijua sauti yake. Mgeni hawatamfuata kabisa, bali watamkimbia; kwa maana hawazijui sauti za wageni.
Mithali hiyo Yesu aliwaambia; lakini wao hawakuelewa na mambo hayo aliyowaambia.
Basi Yesu aliwaambia tena, Amin, amin, nawaambieni, Mimi ndimi mlango wa kondoo. Wote walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi; lakini kondoo hawakuwasikia. Mimi ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka; ataingia na kutoka, naye atapata malisho. Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 13, 2019: JUMATATU, JUMA LA 4 LA PASAKA. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

Ikiwemo Makala hii ya MASOMO YA MISA, MEI 13, 2019: JUMATATU, JUMA LA 4 LA PASAKA, makala nyingine zinazosomwa sana ni kama ifuatavyo;

• Tofauti kati ya Ibada, Sadaka na Sala/maombi | Tofauti ya Misa ya Kikatoliki na Ibada za dini au madhehebu Mengine, isome hapa

• Tafakari ya leo ya Katoliki, Namna ya Kuwa na Amani, isome hapa

• Maswali na majibu kuhusu Sakramenti ya kipaimara, isome hapa

• Imani ni cheti cha Kuweza kupata yote, isome hapa

• TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa, isome hapa

• Maana ya Kuabudu kwa Mkatoliki, isome hapa

• Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba, isome hapa

• Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?, isome hapa

• Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha, isome hapa

• Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili, isome hapa

Ujumbe wangu kwako kwa sasa wa Kutafakari

"Kutubu ndio njia pekee ya kumrudia Mungu. Toba ya kweli ndiyo iletayo maondoleo ya dhambi. Ukiondolewa dhambi unaimarishwa na kufanywa mya. Tubu usamehewe na kufanywa mpya."

Mungu Akubariki Daima. Tukumbukane katika sala.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 13, 2019: JUMATATU, JUMA LA 4 LA PASAKA, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

[WIMBOPA.gif👉] Ewe Mama Uliyeumbwa
[WIMBOPA.gif👉] Kwa Neema ya Mungu
Dismas-Mtakatifu.jpg

Mtakatifu wa Sasa
Leo tunatafakari na kujifunza kutoka kwa Dismas Mtakatifu.
Soma zaidi kuhusu Dismas Mtakatifu hapa.

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..

.

.

IMG_20180108_171540.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Mungu ni mwenye Huruma. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!