MASOMO YA MISA, MEI 12, 2019: JUMAPILI YA 4 YA PASAKA, MWAKA C

Tumsifu Yesu Kristu…

Karibu tena katika Website yako uipendayo ya Wakatoliki yenye mambo mengi kuhusu Imani na Mafundisho ya Kikatoliki. Kama una wasiwasi kuhusu Imani ya Kanisa Katoliki nimekuandalia makala maalumu ya kukufunulia Ukweli hapa>>.

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandikia makala nzuri inayopendwa kuhusu; Ujumbe kwa wakina dada, kwa sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

MASOMO YA MISA, MEI 12, 2019: JUMAPILI YA 4 YA PASAKA, MWAKA C.

Unaweza pia kupokea makala zote mpya zinazopostiwa hapa kwenye email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo.

Endelea kuelimika na kubarikiwa kila siku unapotembelea tovuti hii.

MASOMO YA MISA, MEI 12, 2019: JUMAPILI YA 4 YA PASAKA, MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

JUMAPILI YA MCHUNGAJI MWEMA

SIKU YA KUOMBEA MIITO

MWANZO:

Zab. 33:5-6

Nchi imejaa fadhili za Bwana. Kwa neno la Bwana mbingu zilifanyika, aleluya.

SOMO 1

Mdo 13:14, 43-52

Paulo na Barnaba walitoka Perge, wakapita kati ya nchi, wakafika Antiokia, mji wa Pisidia, wakaingia katika sinagogi siku ya sabato, wakaketi. Sinagogi ilipofumukana, Wayahudi na waongofu watauwa wengi wakashikamana na Paulo na Barnaba; ambao, wakisema nao, wakawatia moyo kudumu katika neema ya Mungu.
Hata sabato ya pili, watu wengi, karibu mji wote, wakakusanyika walisikie neno la Mungu. Bali Wayahudi walipowaona makutano, wakajaa wivu, wakayakanusha maneno yaliyonenwa na Paulo, wakibisha na kutukana. Paulo na Barnaba wakanena kwa ushujaa wakasema, Ilikuwa lazima neno la Mungu linenwe kwenu kwanza; lakini kwa kuwa mnalisukumia mbali, na kujiona nafsi zenu kuwa hamkustahili uzima wa milele, angalieni, twawageukia Mataifa. Kwa sababu ndivyo tulivyoamriwa na Bwana.
Nimekuweka uwe nuru ya Mataifa, Upate kuwa wokovu hata mwisho wa dunia.
Mataifa waliposikia hayo wakafurahi, wakalitukuza neno la Bwana, nao waliokuwa wamekusudiwa uzima wa milele wakaamini. Neno la Bwana likaenea katika nchi ile yote.
Lakini Wayahudi wakawafitinisha wanawake watauwa wenye cheo na wakuu wa mji, wakawataharakisha watu wawaudhi Paulo na Barnaba; wakawatoa katika mipaka yao, wakaenda Ikonio. Na wanafunzi walijaa furaha na Roho Mtakatifu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 100:1-3,5 (K) 3

(K) Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake.

Mfanyieni Bwana shangwe, dunia yote;
Mtumikieni Bwana kwa furaha;
Njoni mbele zake kwa kuimba. (K)

Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu;
Ndiye aliyetuumba na sisi tu watu wake;
Tu watu wake, na kondoo wa malisho yake. (K)

Kwa kuwa Bwana ndiye mwema;
Rehema zake ni za milele;
Na uaminifu wake vizazi na vizazi. (K)

SOMO 2

Ufu. 7:9, 14b-17

Wakati ule, mimi, Yohane, niliona, na tazama, mkutano mkubwa sana ambao hapana mtu awezaye kuuhesabu, watu wa kila taifa, na kabila, na jamaa, na lugha, wamesimama mbele ya kile kiti cha enzi, na mbele za Mwana-kondoo, wamevikwa mavazi meupe, wana matawi ya mitende mikononi mwao.
Mmoja wa wale wazee akiniambia, Hao ndio wanatoka katika dhiki ile iliyo kuu, nao wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-kondoo. Kwa hiyo wako mbele ya kiti cha enzi cha mungu, nao wanamtumikia mchana na usiku katika hekalu lake, na yeye aketiye katika kiti cha enzi atatanda hema yake juu yao. Hawataona njaa tena, wala hawataona kiu tena, wala jua halitawapiga, wala hari iliyo yote. Kwa maana huyo Mwana-kondoo, aliye katikati ya kiti cha enzi, atawachunga, naye atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na Mungu atayafuta machozi yote katika macho yao.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

SHANGILIO

Yn. 10:14

Aleluya, aleluya,
Mimi ndimi mchungaji mwema; nao walio wangu nawajua; nao walio wangu wanijua mimi.
Aleluya.

INJILI

Yn. 10:27-30

Yesu alisema; Kondoo wangu waisikia sauti yangu; nami nawajua, nao wanifuata. Nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe; wala hakuna mtu atakayewapokonya katika mkono wangu. Baba yangu aliyenipa hao ni mkuu kuliko wote; wala hakuna mtu awezaye kuwapokonya katika mkono wa Baba yangu. Mimi na Baba tu umoja.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 12, 2019: JUMAPILI YA 4 YA PASAKA, MWAKA C. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

Ikiwemo Makala hii ya MASOMO YA MISA, MEI 12, 2019: JUMAPILI YA 4 YA PASAKA, MWAKA C, makala nyingine zinazosomwa sana ni kama ifuatavyo;

• Soma hii stori unaweza ukajifunza kitu, isome hapa

• Kanuni za kuishi maisha ya ushindi na baraka, isome hapa

• IBADA YA HURUMA KUU YA MUNGU, isome hapa

• Imani ni cheti cha Kuweza kupata yote, isome hapa

• TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa, isome hapa

• Maana ya Kuabudu kwa Mkatoliki, isome hapa

• Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba, isome hapa

• Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?, isome hapa

• Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha, isome hapa

• Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili, isome hapa

Ujumbe wangu kwako kwa sasa wa Kutafakari

"Mungu anasubiri sala zako kila siku. Anasubiri sala zako akujibu ili uone utukufu wake. Anasubiri sala zako ili akuze mahusiano yake na wewe. Sali daima kwani Mungu yupo milele kukusikiliza na kukuhudumia."

Mungu Akubariki Daima. Tukumbukane katika sala.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 12, 2019: JUMAPILI YA 4 YA PASAKA, MWAKA C, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Mtakatifu-John-Bosco.jpg

Mtakatifu wa Sasa
Leo tunatafakari na kujifunza kutoka kwa Mtakatifu John Bosco.
Soma zaidi kuhusu Mtakatifu John Bosco hapa.

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..

.

.

IMG_20180108_171304.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Sala sio maneno tuu. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!