MASOMO YA MISA, MEI 11, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA PASAKA

Tumsifu Yesu Kristu…

Karibu tena katika Website yako uipendayo ya Wakatoliki yenye mambo mengi kuhusu Imani na Mafundisho ya Kikatoliki. Kama una wasiwasi kuhusu Imani ya Kanisa Katoliki nimekuandalia makala maalumu ya kukufunulia Ukweli hapa>>.

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandikia makala nzuri inayopendwa kuhusu; Maswali na majibu kuhusu Visakramenti, kwa sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

MASOMO YA MISA, MEI 11, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA PASAKA.

Unaweza pia kupokea makala zote mpya zinazopostiwa hapa kwenye email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo.

Endelea kuelimika na kubarikiwa kila siku unapotembelea tovuti hii.

MASOMO YA MISA, MEI 11, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Mdo. 9:31-42

Kanisa lilipata raha katika Uyahudi wote na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongoezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.
Hata Petro alipokuwa akizunguka-zunguka pande zote akawatelemkia na watakatifu waliokaa Lida. Akamwona mtu mmoja huko, jina lake Ainea, mtu huyo amelala kitandani miaka minane; maana alikuwa amepooza. Petro akamwambia. Ainea, Yesu Kriso akuponya; ondoka, ujitandikie. Mara akaondoka. Na watu waliokaa Lida na Sharani wakamwona, wakamgeukia Bwana.
Na mwanafunzi mmoja alikuwako Yafa, jina lake Tabitha, tafsiri yake ni Dorkasi (yaani paa); mwanamke huyu alikuwa amejaa matendo mema na sadaka alizozitoa. Ikawa siku zile akaugua, akafa; hata walipokwisha kumwosha, wakamweka orofani. Na kwa kuwa mji wa Lida ulikuwa karibu na Yafa, nao wanafunzi wamesikia ya kwamba Petro yuko huko, wakatuma watu wawili kwake, kumsihi na kusema, Usikawie kuja kwetu.

Petro akaondoka akafuatana nao. Alipofika, wakampeleka juu orofani wajane wote wakasimama karibu naye, wakilia na kumwonyesha zile kanzu na nguo alizozishona Dorkasi wakati ule alipokuwa pamoja nao. Petro akawatoa nje wote, akapiga maogi, akaomba, kisha akaelekea yule maiti, akanena, Tabitha, ondoka. Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi. Akampa mkono, akamwinua, hata akiisha kuwaita wale watakatifu na wajane akamweka mbele yao, hali yu hai. Ikajulikana katika mji mzima wa Yafa; watu wengi wakamwamini Bwana.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 116:12-17 (K) 12

(K) Nimrudishie Bwana nini kwa ukarimu wake wote alionitendea?

Nimrudishie Bwana nini
Kwa ukarimu wake wote alionitendea?
Nitakipokea kikombe cha wokovu;
Na kulitangaza jina la Bwana. (K)

Nitaziondoa nadhiri zangu kwa Bwana,
Naam, mbele ya watu wake wote.
Ina thamani machoni pa Bwana
Mauti ya wacha Mungu wake. (K)

Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
Mtumishi wako, mwana na mjakazi wako,
Umenifungua vifungo vyangu.
Nitakutolea dhabihu ya kushukuru;
Na kulitangaza jina la Bwana. (K)

SHANGILIO

Kol. 3:1

Aleluya, aleluya,
Mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu, Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu.
Aleluya.

INJILI

Yn. 6:60:69

Siku ile, watu wengi miongoni mwa wanafunzi wake waliposikia maneno ya Yesu juu ya mkate wa uzima, walisema: Neno hili ni gumu, ni nani awezaye kulisikia? Naye Yesu akafahamu nafsini mwake ya kuwa wanafunzi wake wanalinung’unukia neno hilo, akawaambia, Je! Neno hili linawakwaza? Itakuwaje basi, mmwonapo Mwana wa Adamu akipaa huko alikokuwako kwanza? Roho ndiyo itiayo uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Lakini kuna wengine miongoni mwenu wasiomini. Kwa maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini, naye ni nani atakayemsaliti. Akasema, kwa sababu hiyo nimewaambia ya kwamba hakuna mtu awezaye kuja kwangu isipokuwa amejaliwa na Baba yangu. Kwa ajili ya hayo wengi miongoni mwa wanafunzi wake wakarejea nyuma wasiandamane naye tena.

Basi Yesu akawambia wale Thenashara, Je! Ninyi nanyi mwataka kuondoka? Basi Simoni Petro akamjibu, Bwana! Twende kwa nani? Wewe unayo maneno ya uzima wa milele. Nasi tumesadiki, tena tumejua, ya kuwa wewe ndiwe Mtakatifu wa Mungu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 11, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA PASAKA. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

Ikiwemo Makala hii ya MASOMO YA MISA, MEI 11, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA PASAKA, makala nyingine zinazosomwa sana ni kama ifuatavyo;

• Mtakatifu Andrea Mtume, isome hapa

• Maswali na majibu kuhusu Neema na Rehema, isome hapa

• Mafundisho kuhusu kitubio, isome hapa

• TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa, isome hapa

• Maana ya Kuabudu kwa Mkatoliki, isome hapa

• Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba, isome hapa

• Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?, isome hapa

• Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha, isome hapa

• Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili, isome hapa

• Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki, isome hapa

Ujumbe wangu kwako kwa sasa wa Kutafakari

"Mungu anasubiri sala zako kila siku. Anasubiri sala zako akujibu ili uone utukufu wake. Anasubiri sala zako ili akuze mahusiano yake na wewe. Sali daima kwani Mungu yupo milele kukusikiliza na kukuhudumia."

Mungu Akubariki Daima. Tukumbukane katika sala.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 11, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 3 LA PASAKA, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

Mtakatifu-John-Fisher.jpg

Mtakatifu wa Sasa
Leo tunatafakari na kujifunza kutoka kwa Mtakatifu John Fisher.
Soma zaidi kuhusu Mtakatifu John Fisher hapa.

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..

.

.

IMG_20180109_190725.jpg

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Kuomba na Kushukuru. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!