MASOMO YA MISA, MEI 10, 2019 IJUMAA: JUMA LA 3 LA PASAKA

Tumsifu Yesu Kristu…

Karibu tena katika Website yako uipendayo ya Wakatoliki yenye mambo mengi kuhusu Imani na Mafundisho ya Kikatoliki. Kama una wasiwasi kuhusu Imani ya Kanisa Katoliki nimekuandalia makala maalumu ya kukufunulia Ukweli hapa>>.

Mpendwa Msomaji, baada ya kukuandikia makala nzuri inayopendwa kuhusu; Imani na mapokeo ya kanisa Katoliki kwenye Biblia, kwa sasa nimekuandalia makala hii kuhusu;

MASOMO YA MISA, MEI 10, 2019 IJUMAA: JUMA LA 3 LA PASAKA.

Unaweza pia kupokea makala zote mpya zinazopostiwa hapa kwenye email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo.

Endelea kuelimika na kubarikiwa kila siku unapotembelea tovuti hii.

USIKOSE HII👉 Wokovu unapatikana wapi?

MASOMO YA MISA, MEI 10, 2019 IJUMAA: JUMA LA 3 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Mdo. 9:1-20

Siku zile, Sauli, akizidi kutisha na kuwaza kuwaua wanafunzi wa Bwana, akamwendea Kuhani Mkuu, akataka ampe barua za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masinagogi, ili akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemu.
Hapo alipokuwa akisafiri, ikawa anakaribia Dameski; ghafula ikamwangaza kote kote nuru kutoka mbinguni. Akaanguka chini, akasikia sauti ikimwambia, Sauli, Sauli, mbona waniudhi? Akasema, U nani wewe, Bwana? Naye akasema, Mimi ndimi Yesu unayeniudhi wewe. Lakini simama, uingie mjini, nawe utaambiwa yakupasayo kutenda. Na wale watu waliosafiri pamoja naye wakasimama kimya, wakiisikia sauti, wasione mtu. Sauli akainuka katika nchi, na macho yake yalipofumbuka, hakuona kitu; wakamshika mkono wakamleta mpaka Dameski. Akawa siku tatu haoni; hali, wala hanywi.

Basi palipokuwapo Dameski mwanafunzi jina lake Anania. Bwana akamwambia katika maono, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana. Bwana akamwambia, Simama, enenda zako katika njia iitwayo Nyofu, ukaulize katika nyumba ya Yuda mtu aitwaye Sauli, wa Tarso; maana, angalia, anaomba; naye amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, na kumwekea mikono juu yake, apate kuona tena.
Lakini Anania akajibu, Bwana, nimesikia habari za mtu huyu kwa watu wengi, mabaya mengi aliyowatenda watakatifu wako Yerusalemu; hata hapa ana amri itokayo kwa wakuu wa makuhani awafunge wote wakuitiao Jina lako. Lakini Bwana akamwambia, Nenda tu; kwa maan ahuyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya Mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli. Maana nitamwonyesha yalivyo mengi yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu. Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani, akamwekea mikono akisema, Ndugu, Sauli, Bwana amenituma, Yesu yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu. Mara vikaanguka machoni pake vitu kama magamba, akapata kuona, akasimama, akabatizwa, akala chakula, na kupata nguvu.
Akawa huko siku kadha wa kadha pamoja na wanafunzi walioko Dameski. Mara akamhubiri Yesu katika masinagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 117 (K) Mk. 16:15

(K) Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.

Enyi mataifa yote, msifuni Bwana,
Enyi watu wote, mhimidini. (K)

Maana fadhili zake kwetu sisi ni kuu,
Na uaminifu wa Bwana ni wa milele. (K)

SHANGILIO

Rum. 6:9

Aleluya, aleluya,
Kristo akiisha kufufuka katika wafu hafi tena, wala mauti haimtawali tena.
Aleluya.

INJILI

Yn. 6:52-59

Siku ile, Wayahudi walishindana wao kwa wao wakisema, Awezaje mtu huyu kutupa sisi mwili wake ili tuule?
Basi Yesu akawaambia, Amin, amin, nawaambieni, Msipoula mwili wake Mwana wa Adamu na kuinywa damu yake, hamna uzima ndani yenu. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu anao uzima wa milele; nami nitamfufua siku ya mwisho. Kwa maana mwili wangu ni chakula cha kweli, na damu yangu ni kinywaji cha kweli. Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu hukaa ndani yangu, nami hukaa ndani yake. Kama vile Baba aliye hai alivyonituma mimi, nami ni hai kwa Baba; kadhalika naye mwenye kunila atakuwa hai kwa mimi. Hiki ndicho chakula kishukacho kutoka mbinguni; si kama mababa walivyokula, wakafa; bali akilaye chakula hicho ataishi milele.
Maneno hayo aliyasema katika sinagogi, alipokuwa akifundisha, huko Kapernaumu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.

Usisahau kushare makala hii uliyoisoma kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 10, 2019 IJUMAA: JUMA LA 3 LA PASAKA. Share Facebook, Twitter bila kusahau WhatsApp.

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

Ikiwemo Makala hii ya MASOMO YA MISA, MEI 10, 2019 IJUMAA: JUMA LA 3 LA PASAKA, makala nyingine zinazosomwa sana ni kama ifuatavyo;

• Muujiza wa Madonda ya padre Pio, isome hapa

• Mtakatifu Fransisko wa Asizi, isome hapa

• Matumizi ya Neno 'Ameen', isome hapa

• TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa, isome hapa

• Maana ya Kuabudu kwa Mkatoliki, isome hapa

• Jifunze kitu Kwenye mfano huu kuhusu Maombi na kuomba, isome hapa

• Biblia inatuambia nini kuhusu pombe?, isome hapa

• Kujikabidhi Kwa Yesu Kristu Yeye Aliye Mwangaza Wa Maisha, isome hapa

• Vitu 7 katika maisha ambavyo huwezi kuvibadili hadi ubadili, isome hapa

• Uzinzi na Uasherati ndio mtego wa kizazi hiki, isome hapa

Ujumbe wangu kwako kwa sasa wa Kutafakari

"Uwe na maono au ndoto ya mambo unayotaka kufanya maishani naye Mungu atakubariki na kujidhihirisha katika ndoto zako."

Mungu Akubariki Daima. Tukumbukane katika sala.

Unaweza kusoma makala mpya nzuri kila unapotembelea website hii wakati wowote. Baada ya kusoma makala hii kuhusu; MASOMO YA MISA, MEI 10, 2019 IJUMAA: JUMA LA 3 LA PASAKA, sasa endelea kusoma makala hizi nyingine nzuri nilizokuandalia;

[WIMBOPA.gif👉] Mateso yako
Mtakatifu-Juan-Diego.jpg

Mtakatifu wa Sasa
Leo tunatafakari na kujifunza kutoka kwa Mtakatifu Juan Diego.
Soma zaidi kuhusu Mtakatifu Juan Diego hapa.

Chagua aina ya mafundisho unayotaka kusoma hapa..

.

.

width="60px"

Kama Una mashaka na Imani na mafundisho ya Kanisa Katoliki soma hapa>>

Website hii inaletwa kwako na Melkisedeck Leon Shine.

Naomba utafakari kuhusu; Anachokiangalia Mungu. Mungu akubariki sana. Tuombeane…!