MASOMO YA MISA, JUNI 8, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 7 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, ubatizo tuu unatosha?

SOMO 1

Mdo. 28 :16-20, 30-31

Tulipoingia Rumi Paulo alipewa ruhusa kukaa kwake mwenyewe pamoja na askari aliyemlinda.
Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane; hata walipokutanika akawaambia, Ndugu zangu, ingawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, hali nimefungwa, tokea Yerusalemu. Na hao walipokwisha kuniuliza-uliza walitaka kunifungua, kwa maana hapakuwa na sababu yo yote kwangu ya kuuawa.

Lakini Wayahudi walipotoa hoja juu ya shauri hili nalishurutishwa kutaka rufani kwa Kaisari. Si kwamba nalikuwa na neno la kuwashitaki watu wa taifa langu. Basi kwa ajili ya hayo, nimewaita mje kunitazama na kusema nami; kwa maana nimefungwa kwa mnyororo huu kwa ajili ya tumaini la Israeli.

Akakaa muda wa miaka miwlli mizima katika nyumba yake aliyokuwa ameipanga, akawakaribi sha watu wote waliokuwa wakimwendea, akihubiri habari za ufalme wa Mungu, na kuyafundisha mambo ya Bwana Yesu Kristo, kwa ujasiri mwingi, asikatazwe na mtu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 11 :4-5, 7 (K) 7

(K) Wanyofu wa moyo wauona uso wake, Ee Bwana. au: Aleluya.

Bwana yu katika hekalu lake takatifu.
Bwana ambaye kiti chake kiko mbinguni,
Macho yake yanaangalia;
Kope zake zinawajaribu wanadamu. (K)

Bwana humjaribu mwenye haki;
Bali nafsi yake humchukia asiye haki,
Na mwenye kupenda udhalimu. (K)

Kwa kuwa Bwana ndiye mwenye haki,
Apenda matendo ya haki,
Wanyofu wa moyo watamwona uso wake. (K)

SHANGILIO

Mt. 28 :19-20

Aleluya, aleluya,
Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi. Mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, Hata ukamilifu wa dahari.
Aleluya.

INJILI

Yn. 21:20-25

Petro aligeuka akamwona yule mwanafunzi aliyependwa na Yesu anafuata; (ndiye huyo aliyeegama kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni, akasema, Bwana, ni nani akusalitiye?). Basi Petro akamwona huyo, akamwambia Yesu, Bwana, na huyu je? Yesu akamwambia, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Wewe unifuate mimi.

Basi neno hilo lilienea katikati ya ndugu ya kwamba mwanafunzi yule hafi. Walakini Yesu hakumwambia ya kwamba hafi; bali, Ikiwa nataka huyu akae hata nijapo, imekupasaje wewe? Huyu ndiye yule mwanafunzi ayashuhudiaye haya, na aliyeyaandika haya; nasi twajua ya kuwa ushuhuda wake ni kweli. Kuna na mambo mengine mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Nani ana lazima ya kufunga?

Kila Mkristo aliyetimiza miaka 14 na zaidi anapaswa kufunga kula nyama (Ijumaa kuu) na mwenye miaka zaidi ya 21 kufunga chakula. (Jumatano ya Majivu).. soma zaidi

a.gif Agano la Mungu na Abramu

Mwanzo 15
1 Baada ya mambo hayo neno la Bwana likamjia Abramu katika njozi, likinena, Usiogope, Abramu, Mimi ni ngao yako, na thawabu yako kubwa sana… soma zaidi

a.gif Mungu aliwapa watu (mapadri) amri/uwezo ya kusamehe dhambi kwa njia ya nani? Ni halali kuungama kwa padre?

Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa njia ya Mwanae. Yesu mfufuka aliwaonyesha Mitume alama ya mateso mwilini mwake, “akawavuvia, akawaambia, ‘Pokeeni Roho Mtakatifu. Wowote mtakaowaondolea dhambi, wameondolewa; na wowote mtakaowafungia dhambi, wamefungiwa” (Yoh 20:22-23)... soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 8, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 7 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 8, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 7 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA KUTUBU

[Wimbo Mzuri PA.gif] Tunakushukuru Mama Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala ni Hazina

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Katarina wa Siena

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

New-Microsoft-PowerPoint-Presentation-2.gif

a.gif Uchaji wa Mungu ni nini?

Ni hofu ya kumchukiza Mungu kwa Dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumchukiza mzazi au mlezi wake… soma zaidi

a.gif Mfano wa sanamu takatifu ni zipi?

Sanamu ya Bikira Maria, Mtoto Yesu, Mt. Yosefu, Moyo wa Yesu na za Watakatifu… soma zaidi

a.gif Ni vitu gani vya msingi na vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu?

Vitu vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu ni.. soma zaidi

a.gif Je, mwili wetu ni muhimu?

Ndiyo, mwili wetu ni muhimu, kwa sababu umeumbwa na Mungu, umetwaliwa na Mwanae ili atuokoe, umehuishwa na Roho Mtakatifu atakayeutukuza siku ya ufufuo kwa mfano wa Yesu… soma zaidi

a.gif Tofauti ya Sala na Maombi

Sala na Maombi vinatofautiana kama ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Anayevunja Amri ya Tatu ya Mungu yampasa nini?

Yampasa atubu na aungame kabla ya kushiriki Sakramenti nyingine.. soma zaidi

a.gif Mali ya mtu ni ipi?

Mali ya mtu ni ile aliyoipata kwa njia halali yaani kwa haki… soma zaidi

a.gif Kisha kosa la Adamu na Eva Mungu aliahidi nini?

Kisha kosa la Adamu na Eva Mungu aliahidi kuwaletea Mkombozi. (Mwa 3:15).. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Mitume

Maswali kuhusu mitume ni;.. soma zaidi

a.gif Baba wa Yesu Kristo ni nani?

Baba wa Yesu Kristo ni Mungu Mwenyewe.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.