MASOMO YA MISA, JUNI 6, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 7 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

Mdo. 22 : 30; 23 : 6-11

Wakati ule, Jemadari alitaka kujua hakika, ni kwa sababu gani Paulo ameshitakiwa na Wayahudi, akamfungua, akawaamuru wakuu wa makuhani na baraza yote wakutane. Akamleta Paulo chini, akamweka mbele yao.

Paulo alipotambua ya kuwa sehemu moja ni Masadukayo, na sehemu ya pili ni Mafarisayo, akapaza sauti yake katika ile baraza, Ndugu zangu, mimi ni Farisayo, mwana wa Farisayo; mimi ninahukumiwa kwa ajili ya tumaini la ufufuo wa wafu. Alipokwisha kunena hayo palikuwa na mashindano baina ya Mafarisayo na Masadukayo, mkutano ukafarakana. Kwa maana Masadukayo husema ya kwamba hakuna kiyama wala malaika wala roho; bali Mafarisayo hukiri yote. Pakawa na makelele mengi. Waandishi wengine wa upande wa Mafarisayo wakasimama, wakateta, w'akisema, Hatuoni uovu wo wote katika mtu huyu; bali ikiwa roho au malaika amesema naye, ni nini? Ugomvi mkubwa ulipotokea, yule jemadari akachelea Paulo asije akararuliwa nao, akaamuru askari washuke na kumwondoa kwa nguvu mikononi mwao, na kumleta ndani ya ngome.

Usiku ule Bwana akasimama karibu naye, akasema, Uwe na moyo mkuu; kwa sababu, kama ulivyonishuhudia habari zangu Yerusalemu, imeku- pasa kunishuhudia vivyo hivyo Rumi nako.
Hilo ndilo neno la Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 16:1-2, 7-11 (K) 1

(K) Mungu unihifadhi mimi, kwa maana nakukimbilia Wewe. au: Aleluya.

Mungu unihifadhi mimi,
kwa maana nakukimbilia Wewe.
Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu,
sina wema ila utokao kwako. (K)

Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri,
Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
Nimemweka Bwana mbele yangu daima,
Kwa kuwa yako kuumeni kwangu, sitaondoshwa. (K)

Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,
Nao utukufu wangu unashangilia,
Naam, mwili wangu nao utakaa kw;a kutumaini.
Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,
Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. (K)

Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele;
Na katika mkono wako wa kuume
Mna mema ya milele. (K)

SHANGILIO

Yn. 16:28

Aleluya, aleluya,
Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena naucha ulimwengu, na kwenda kwa Baba.
Aleluya.

INJILI

Yn. 17 :20-26

Siku ile, Yesu alisali akisema: Wala si hao tu ninaowaombea; lakini na wale watakaoniamini kwa sababu ya neno lao. Wote wawe na umoja; kama wewe, Baba, ulivyo ndani yangu, nami ndani yako; hao nao wawe ndani yetu; ili ulimwengu upate kusadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Nami utukufu ule ulionipa nimewapa wao; ili wawe na umoja kama sisi tulivyo umoja. Mimi ndani yao, nawe ndani yangu, ili wawe wamekamilika katika umoja; ili ulimwengu ujue ya kuwa ndiwe uliyenituma, ukawapenda wao kama ulivyonipenda mimi.

Baba, hao ulionipa nataka wawe pamoja nami po pote nilipo, wapate na kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa msingi ulimwengu. Baba mwenye haki, ulimwengu haukukujua; lakini mimi nalikujua, na hao wamejua ya kuwa ndiwe uliyenituma. Nami naliwajulisha jina lako, tena nitawajulisha hilo; ili pendo lile ulilonipenda mimi liwe ndani yao, nami niwe ndani yao.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Mwenyezi Mungu yukoje basi?

Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote… soma zaidi

a.gif Ishara ya Msalaba

Ishara ya Msalaba ni tendo la mtu kugusa panda la uso, kifua na mabega kwa kutumia mkono wa kulia na kutamka 'Kwa Jina la Baba, na la Mwana na la Roho Mtakatifu, Amina'… soma zaidi

a.gif Tupokeeje ufunuo wa Mungu?

Tupokee ufunuo wa Mungu kwa kusadiki mafundisho ya Kanisa lake, ili tuzidi kumjua na kuambatana naye bila ya kudanganyika. Yesu aliwaambia Mitume wake,.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 6, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 7 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 6, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 7 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE 1

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo wa siku zote

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Justin mfiadini

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

UJUMBE-WA-ASUBUHI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Upendo Mkuu wa Mungu

Mungu alimpenda sana binadamu hata akauvaa Mwili wa Binadamu akashuka duniani na kuishi kama Binadamu ili amkomboe Mwanadamu na hata akaamua kufa kwa ajili ya Binadamu kwa malipizi ya dhambi za Binadamu na kwa maondoleo ya dhambi… soma zaidi

a.gif Kwa nini Binti usivae Suruali, ubaya wa Suruali kwa wanawake

By : Ntogwisangu J. C
🔹Kumekuwa na mada nyingi na maswali mengi kuhusu mabinti kuvaa suruali (hasa waliookoka), michango mingi na mafundisho mengi yametolewa, nami naomba niongezee kitu kidogo.
🔹Zifuatazo ni sababu kwanin binti hautakiwi kuvaa suruali….. soma zaidi

a.gif Mataifa yaliyotokana na Noa

1 Hivi ndivyo vizazi vya wana wa Nuhu, Shemu, na Hamu, na Yafethi. Na kwao walizaliwa wana wa kiume baada ya gharika… soma zaidi

a.gif Kwa nini yatupasa kuwaheshimu Watakatifu?

Kwa sababu hao ni washindi, rafiki wa Mungu na waombezi wetu… soma zaidi

a.gif Je Malaika wote ni sawa?

Hapana. Malaika wote sio sawa, maana kuna;.. soma zaidi

a.gif Ni nanai ana kosa kumuabudu Mungu?

Anayekosa kumuabudu Mungu ni yule;.. soma zaidi

a.gif Utawa ni nini?

Utawa ni njia ya kipekee ya kuufikia ukamilifu wa Kristo kwa kujifunga hadharani kuishi mashauri ya Injili.. soma zaidi

a.gif Mtume Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu… soma zaidi

a.gif Mkatoliki anaabuduje?

Mkatoliki anaabudu kwa kupiga goti au magoti mawili na ni mbele ya sakramenti ya Ekaristi Takatifu tuu hasa wakati wa kuingia na kutoka kanisani.. soma zaidi

a.gif TAFAKARI YA MAISHA: Vile unavyobariki, ndivyo unavyobarikiwa

Kiwango cha majukumu uliyonayo kinaamua kiwango cha baraka zinazofuatana na wewe… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.