MASOMO YA MISA, JUNI 4 , 2019: JUMANNE, JUMA LA 7 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Je, ekaristi ni kafara (sadaka)?

SOMO 1

Mdo. 20 :17-27

Siku zile, toka Mileto Paulo alituma watu kwenda Efeso, akawaita wazee wa kanisa. Walipofika
kwake, akawaambia, Ninyi wenyewe mnajua tangu siku ya kwanza nilipokanyaga hapa Asia, jinsi nilivyokuwa kwenu wakati wote, nikimtumikia Bwana kwa unyenyekevu wote, na kwa machozi na majaribu yaliyonipata kwa hila za Wayahudi; ya kuwa sikujiepusha katika kuwatangazia neno lo lote liwezalo kuwafaa, bali naliwafundisha waziwazi, na nyumba kwa nyumba, nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo.

Basi sasa, angalieni, nashika njia kwenda Yerusalemu hali nimefungwa rohoni, nisiyajue mambo yatakayonikuta huko; isipokuwa Roho Mtakatifu mji kwa mji hunishuhudia akisema, ya kwamba vifungo na dhiki vyaningoja. Lakini siyahesabu maisha yangu kuwa kitu cha thamani kwangu kama kuumaliza mwendo wangu na huduma ile niliyopokea kwa Bwana Yesu, kuishuhudia Habari njema ya neema ya Mungu. Na sasa, tazameni, mimi najua ya kuwa ninyi nyote niliowahubiria ufalme wa Mungu, nikienda huko na huko, hamtaniona uso tena. Kwa hiyo nawashuhudia wote siku hii ya leo, ya kuwa mimi sina hatia kwa damu ya mtu awaye yote. Kwa maana sikujiepusha na kuwahubiria habari ya kusudi lote la Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 68 : 9-10, 19-20 (K) 32

K. Enyi falme wa dunia, mwimbieni Mungu. Au: K. Aleluya.

Ee Mungu, ulinyesha mvua ya neema;
Urithi wako ulipochoka uliutia nguvu.
Kabila yako ilifanya kao lake huko;
Ee Mungu, kwa wema wako uliwaruzuku walioonewa. (K)

Na ahimidiwe Bwana,
Siku kwa siku hutuchukulia mzigo wetu;
Mungu ndiye wokovu wetu.
Mungu kwetu sisi ni Mungu wa kuokoa;
Na njia za kutoka mautini. (K)

SHANGILIO

Yn. 14:16

Aleluya, aleluya,
Nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele.
Aleluya.

INJILI

Yn. 17:1-11

Siku ile, Yesu aliinua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe. Kama vile ulivyompa mamlaka juu ya wote wenye mwili, ili kwamba wote uliompa awape uzima wa milele. Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimekutukuza duniani, hali nimeimaliza kazi ile uliyonipa niifanye.

Na sasa, Baba, unitukuze mimi pamoja nawe, kwa utukufu ule niliokuwa nao pamoja nawe kabla ya ulimwengu kuwako. Jina lako nimewadhihirishia watu wale ulionipa katika ulimwengu; walikuwa wako, ukanipa mimi, na neno lako wamelishika. Sasa wamejua ya kuwa yote uliyonipa yatoka kwako. Kwa kuwa maneno uliyonipa nimewapa wao; nao wakayapokea, wakajua hakika ya kuwa nalitoka kwako, wakasadiki ya kwamba wewe ndiwe uliyenituma. Mimi nawaombea hao; siuombei ulimwengu; bali hao ulionipa, kwa kuwa hao ni wako; na wote walio wangu ni wako, na walio wako ni wangu; nami nimetukuzwa ndani yao. Wala mimi simo tena ulimwenguni, lakini hawa wamo ulimwenguni, nami naja kwako.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristu


a.gif Mwenyezi Mungu yukoje basi?

Mwenyezi Mungu ni ukamilifu mtupu usio na mipaka kwa milele yote… soma zaidi

a.gif Usafi wa Moyo ndio nini?

Usafi wa Moyo ni fadhila ya kiutu, zawadi ya Mungu, neema na tunda la Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Je, wenye daraja wanastahili heshima?

Ndiyo, wenye daraja wanastahili heshima kwa sababu ya mamlaka ya Kiroho waliyonayo kutoka kwa Kristo… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 4 , 2019: JUMANNE, JUMA LA 7 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 4 , 2019: JUMANNE, JUMA LA 7 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Kwa Neema ya Mungu

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwema

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Anna

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

KADI-MZAZI-ASUBUHI.JPG

a.gif Walei ni wakina nani?

Walei ni wote katika Kanisa wasio na Daraja Takatifu.. soma zaidi

a.gif Kabla ya kupokea Sakramenti ya Ndoa hutakiwa nini?

Kabla ya kupokea Sakramenti ya Ndoa hutakiwa;
1. Uhuru wa kila mmoja
2. Matangazo ya ndoa
3. Wachumba wawe na nia ya kweli ya kuoana.. soma zaidi

a.gif Sala ya fikara ni nini?

Sala ya fikra ni sala asaliyo mtu peke yake au akiwa na wengine kimya kimya akimuwaza Mungu.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya kwanza daima ni ipi?

Sakramenti ya kwanza daima ni ubatizo, kwa kuwa ndio kupata uzima mpya kwa kushiriki kifo na ufufuko wa Yesu, inavyodokezwa wazi zaidi mtu akizamishwa na kutolewa majini… soma zaidi

a.gif Ni kipi cha kutunza kwa makini zaidi kati ya mwili na roho yako?

Yatupasa kutunza roho zetu zaidi kwni Yesu mwenyewe alisema:.. soma zaidi

a.gif Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake nini?

Kumpokea Roho Mtakatifu maana yake ni kuja kuongozwa naye badala ya kutawaliwa na shetani… soma zaidi

a.gif Mungu ni nani?

Mungu ndiye muumba wa kila kitu katika uwingu na nchi, Mkubwa wa ulimwengu mwenye kuwatuza watu wema na kuwaadhibu watu wabaya… soma zaidi

a.gif Je, ubatizo tuu unatosha?

Hapana, ubatizo hautoshi, bali unahitaji kukamilishwa na kipaimara na ekaristi, kama vile baada ya kuzaliwa tunahitaji kukomaa na kudumisha uhai wetu kwa chakula… soma zaidi

a.gif Je, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa?

Ndiyo, mwenye daraja anaweza kuwa na ndoa… soma zaidi

a.gif Anayevunja Amri ya Tatu ya Mungu yampasa nini?

Yampasa atubu na aungame kabla ya kushiriki Sakramenti nyingine.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.