MASOMO YA MISA, JUNI 30, 2019 DOMINIKA YA 13 YA MWAKA C

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUNI 30, 2019 DOMINIKA YA 13 YA MWAKA C

SOMO 1

1 Fal. 19:16b. 19-21

Bwana alimwambia Eliya: Enenda, mtie mafuta Elisha mwana wa Shafati wa Abel-Mehola awe nabii mahali pako. Basi akaondoka huko, akamkuta Elisha mwana wa Shafati, aliyekuwa akilima, mwenye jozi za ng’ombe kumi na mbili mbele yake, na yeye mwenyewe alikuwa pamoja na lile la kumi na mbili. Eliya akapita karibu naye, akatupa vazi lake juu yake. Naye akawaacha ng’ombe, akamfuata Eliya mbio, akasema, Nipe ruhusa, nakuomba, nimbusu baba yangu na mama yangu, kisha mimi nitakufuata. Akamwambia, Enenda, urudi; ni nini niliyokutendea. Akarudi akiacha kumfuata, akatwaa lile jozi la ng’ombe, akawachinja, akatokosa nyama zao kwa ile miti ya ng’ombe, akawapa watu, wakala. Kisha akainuka, akamfuata Eliya, akamhudumia.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab16:1-2, 5, 7-11 (K) 5

(K) Bwana ndiye fungu la posho langu.

Mungu, unihifadhi mimi,
Kwa maana nakukimbilia Wewe.
Nimemwambia Bwana, Ndiwe Bwana wangu;
Bwana ndiye fungu la posho langu.
Na la kikombe changu;
Wewe unaishika kura yangu. (K)

Nitamhimidi Bwana aliyenipa shauri,
Naam, mtima wangu umenifundisha usiku.
Nimemweka Bwana mbele yangu daima,
Kwa kuwa yako kuumeni kwangu, sitaondoshwa. (K)

Kwa hiyo moyo wangu unafurahi,
Na utukufu wangu unashangilia,
Naam, mwili wangu nao utakaa kwa kutumaini.
Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu,
Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. (K)

Utanijulisha njia ya uzima;
Mbele za uso wako ziko furaha tele
Na katika mkono wako wa kuume
Mna mema ya milele. (K)

SOMO 2

Gal. 5 :1,13-18

Katika ungwana huo Kristo alituandika huru; kwa hiyo simamemi, wala msinaswe tena chini ya kongwa la utumwa. Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo. Maana torati yote imetimilika katika neno moja, nalo ni hili, Umpende jirani yako kama nafsi yako. Lakini mkiumana na kulana, angalieni msije mkaangamizana. Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingama, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Lakini mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu

SHANGILIO

Yn. 17:17

Aleluya, aleluya,
Neno lako ndiyo kweli, ee Bwana; Ututakase sisi kwa ile kweli.
Aleluya.

INJILI

Lk. 9:51-62

Ikawa, siku za kupaa kwake zilipokuwa karibu kutimia, Yesu aliukaza uso wake kwenda Yerusalemu; akatuma wajumbe kutangulia mbele ya uso wake; wakaenda wakaingia katika kijiji cha Wasamaria, ili kumtengenezea mahali. Lakini wenyeji hawakumkaribisha kwa vile alivyouelekeza uso wake kwenda Yerusalemu. Wanafunzi wake Yakobo na Yohane walipoona hayo, walisema, Bwana, wataka tuagize moto ushuke kutoka mbinguni, uwaangamize; [kama Eliya naye alivyofanya]? Akawageukia akawakanya. Akasema, Hamjui ni roho ya namna gani mliyo nayo. Kwa maana Mwana wa Adamu hakuja kuziangamiza roho za watu, bali kuziokoa. Wakaondoka wakaenda mpaka kijiji kingine. Nao walipokuwa wakienda njiani, mtu mmoja alimwambia, Nitakufuata ko kote utakakokwenda. Yesu akamwambia, Mbweha wana pango, na ndege wa angani wana vioto, lakini Mwana wa Adamu hana pa kujilaza kichwa chake. Akamwambia mwingine, Nifuate. Akasema, Bwana, nipe ruhusa kwanza niende kumzika baba yangu. Akamwambia, Waache wafu wawazike wafu wao; bali wewe enenda ukautangaze ufalme wa Mungu. Mtu mwingine pia akamwambia, Bwana nitakufuata; lakini, nipe ruhusu kwanza nikawaage watu wa nyumbani mwangu. Yesu akamwambia, Mtu aliyetia mkono wake kulima, kisha akaangalia nyuma, hafai kwa ufalme wa Mungu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Ni ipi sala bora kwa Bikira Maria? Kwa nini Tunasali kwa Bikira Maria?

Sala bora kwa Bikira Maria ni Rozari Takatifu.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Uaminifu

Uaminifu ni kipimo na kigezo cha Ukamilifu na Utakatifu… soma zaidi

a.gif Ubahili ni nini?

Ubahili ni kupenda mno mali za dunia na kumsahau Mungu.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 30, 2019 DOMINIKA YA 13 YA MWAKA C

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 30, 2019 DOMINIKA YA 13 YA MWAKA C

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Njia ya sala

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Fransisko wa Sales

JE-MARIA-NI-MAMA-YETU-PIA.JPG

a.gif Malaika Walinzi wanatutendea nini?

Malaika walinzi hutupenda, hutuongoza, na kutulinda roho na mwilini (Zab 90:11).. soma zaidi

a.gif Mtume Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu… soma zaidi

a.gif Kuna Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso?

Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso ni;-.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Vishawishi

Kuhusu vishawishi soma hapa;.. soma zaidi

a.gif Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?

Majina haya;.. soma zaidi

a.gif Katika Amri ya Nne ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa haya;.. soma zaidi

a.gif Kwa nini Mungu aliumba vyote?

Mungu aliumba vyote bila ya kulazimika, kusudi tu adhihirishe na kushirikisha utukufu wake… soma zaidi

a.gif Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti huenda wapi?

Anayekufa akiwa na dhambi ya mauti hutupwa motoni milele. (Mt 25:41).. soma zaidi

a.gif Uelewa wa namba katika Biblia

Biblia imeandikwa na Mungu kupitia waandishi wanadamu kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni Neno la Mungu. Hivyo mwandishi wa Biblia ni Mungu kupitia wanadamu (God is the primary author of the Bible while human authors are secondary authors). Mungu aliwavuvia (inspiration by the Holy Spirit) waandishi wanadamu ili waweze kuandika kile tu ambacho Yeye (Mungu) alitaka kiandikwe kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Kusema kuwa Biblia imeandikwa na Mungu kupitia wanadamu haina maana ya kuandikwa kwa njia ya imla (dictation), kana kwamba Mungu anataja sentensi au neno na wao wanaandika. Hapana, pamoja na kuwavuvia Roho Mtakatifu, waandishi wanadamu walikuwa huru kutumia vipawa mbalimbali vya uandishi na mazingira yao ili kufikisha ujumbe ambao Mungu amewavuvia. Hivyo walikuwa “active writers of the Bible, and not passive writers.” Walitumia akili (reason), utashi (will), ujengaji picha (imagination) na vipawa vingine. Lakini vipawa hivi vyote vilikuwa chini ya maongozi ya Roho Mtakatifu ili kuwawezesha waandishi wa Biblia kufikisha ujumbe kwa ufasaha bila makosa… soma zaidi

a.gif Sala ya kanisa ni nini?

Sala ya kanisa ni sala maalumu wasaliyo Maklero, Watawa, na Walei kwa ajili ya Kanisa zima.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.