MASOMO YA MISA, JUNI 3, 2019: JUMATATU, JUMA LA 7 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUNI 3, 2019: JUMATATU, JUMA LA 7 LA PASAKA

SOMO 1

Mdo. 19:1-8

Ikawa, Apolo alipokuwa Korintho, Paulo, akiisha kupita kati ya nchi za juu, akafika Efeso; akakutana na wanafunzi kadha wa kadha huko; akawauliza, Je! mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini? Wakamjibu, La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia. Akawauliza, basi mlibatizwa kwa ubatizo gani? Wakasema, kwa ubatizo wa Yohane. Paulo akasema, Yohane alibatiza kwa ubatizo wa toba, akiwaambia watu wamwamini yeye atakayekuja nyuma yake, yaani, Yesu.

Waliposikia haya wakabatizwa kwa jina la Bwana Yesu. Na Paulo, alipokwisha kuweka mikono yake juu yao, Roho Mtakatifu akaja juu yao; wakaanza kunena kwa lugha, na kutabiri. Na jumla yao walipata wanaume kumi na wawili. Akaingia ndani ya sinagogi, akanena kwa ushujaa kwa muda wa miezi mitatu, akahojiana na watu, na kuwavuta katika mambo ya ufalme wa Mungu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATI KATI

Zab. 68 :1-6 (K) 32

(K) Enyi falme za dunia, mwimbieni Mungu. au: Aleluya.

Mungu huondoka, adui zake wakatawanyika,
Nao wamchukiao huukimbia uso wake.
Kama moshi upeperushwavyo,
Ndivyo uwapeperushavyo wao;
Kama nta iyeyukavyo mbele ya moto,
Ndivyo waovu wapoteavyo usoni pa Mungu. (K)

Bali wenye haki hufurahi,
Na kuushangilia uso wa Mungu,
Naam, hupiga kelele kwa furaha.
Mwimbieni Mungu, lisifuni jina lake,
Shangilieni mbele zake. (K)

Baba wa yatima na mwamuzi wa wajane,
Mungu katika kao lake takatifu.
Mungu huwakalisha wapweke nyumbani;
Huwatoa wafungwa wakae hali ya kufanikiwa;
Bali wakaidi hukaa katika nchi kavu. (K)

SHANG1LIO

Mt. 28 :19, 20

Aleluya, aleluya,
Enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mimi nipo pamoja nanyi sikuzote, hata ukamilifu wa dahari.
Aleluya.

INJILI

Yn. 16:29-33

Wanafunzi walimwambia Yesu: Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni mithali yo yote. Sasa tumejua ya kuwa wewe wafahamu mambo yote wala huna haja ya mtu akuulize; kwa hiyo twasadiki ya kwamba ulitoka kwa Mungu.

Yesu akawajibu, Je! mnasadiki sasa? Tazama. saa yaja, naam, imekwisha kuja ambapo mtatawanyika kila mmoja kwao kwao, na kuniacha mimi peke yangu; walakini mimi si peke yangu, kwa kuwa Baba yupo pamoja nami. Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Sakramenti ya Kipaimara ni nini?

Ni Sakramenti yenye kumpa Mkristu Roho Mtakatifu na ukamilifu wa mapaji yake saba, kumfanya mkristu mkamilifu na kumwandika Askari hodari wa Yesu Kristo Mpaka Kufa.. soma zaidi

a.gif MAFUNDISHO KUHUSU NAFASI YA MAMA BIKIRA MARIA

Sisi Wakatoliki nyakati hizi zilizojaa madhehebu mbalimbali ya Kikristo, yanayotumia Biblia na kuitafsiri kadiri ya
imani yao ama wenyewe wanavyojisikia kwa namna fulani, tunajikuta tukichanganyikiwa na pengine kuona aibu ya
kumheshimu Mama Bikira Maria. Tunapoanza kuchunguza nafasi yake katika fumbo la ukombozi wa mwanadamu,
tunakiri pamoja naye kuwa ni Mwenyezi Mungu aliyemtendea makuu (Lk 1:49). Halafu tunakiri kwa unyenyekevu
wote pamoja na Yohane Mbatizaji, “Mtu hawezi kuwa na kitu asipopewa na Mungu” (Yoh 3:27). Hivyo yale yote
tunayoyasadiki kuhusu Bikira Maria, hakujipatia mwenyewe bali amejaliwa na Mwenyezi Mungu na kuitikia kwa
hiari fumbo la mpango wake… soma zaidi

a.gif Kutubu dhambi maana yake ni nini?

Kutubu dhambi maana yake ni kuona uchungu na chuki moyoni juu ya dhambi tulizotenda na kukusudia kutotenda dhambi tena (Yoh 8:11).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 3, 2019: JUMATATU, JUMA LA 7 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 3, 2019: JUMATATU, JUMA LA 7 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉LITANIA YA KUWAOMBEA MAPADRE WOTE II

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwema

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Anna

KADI-TUKUTANE-MZAZI.JPG

a.gif Uchaji wa Mungu ni nini?

Ni hofu ya kumchukiza Mungu kwa Dhambi kama vile mtoto mwema aogopavyo kumchukiza mzazi au mlezi wake… soma zaidi

a.gif Nyaraka za Mitume katika Biblia ni zipi?

Nyaraka za Mitume ni;
1. Waroma
2. 1 Wakorinto
3. 2 Wakorinto
4. Wagalatia
5. Waefeso
6. Wafilipi
7. Wakolosai
8. 1 Wathesalonike.. soma zaidi

a.gif Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lingekuwaje?

Bila ya Maaskofu, mapadri na mashemasi, Kanisa lisingekuwepo kwa sababu uhai wake unategemea kabisa ekaristi iliyokabidhiwa kwao… soma zaidi

a.gif MPANGILIO WA KURASA ZA POSTI NA MAKALA

Makala kuu za Wakatoliki;.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Watakatifu ndani ya Kanisa Katoliki

Soma haya kuhusu watakatifu;.. soma zaidi

a.gif Ipi ni shule ya kwanza ya sala?

Familia ni shule ya kwanza ya sala.. soma zaidi

a.gif Ndoa imewekwa na nani?

Ndoa imewekwa na Mungu mwenyewe na Yesu Kristo ameeinua na kuifanya Sakramenti. (Mwz 2:18; Mt 19:1-12).. soma zaidi

a.gif Dhamiri adilifu ni nini?

Dhamiri adilifu, iliyo ndani kabisa mwa mtu, ni uamuzi wa akili ambao kwa wakati wake unamuagiza mtu atende mema na kukwepa maovu.. soma zaidi

a.gif Amani ya Moyoni au Rohoni

Amani ya Moyoni au Rohoni ni hali ya kutokua na wasiwasi na hofu moyoni kuhusu Mambo ya Rohoni na ya kidunia… soma zaidi

a.gif Je, mafumbo yote saba yanazaa matunda yaleyale?

Hapana, mafumbo yote saba hayazai matunda yaleyale, bali Yesu aliweka kila moja kwa lengo maalumu, litupatie Roho Mtakatifu kadiri ya nafasi na haja fulani ya maisha yetu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.