MASOMO YA MISA, JUNI 24, 2019: JUMATATU, JUMA L A 12 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUNI 24, 2019: JUMATATU, JUMA L A 12 LA MWAKA

SHEREHE YA KUZALIWA MTAKATIFU YOHANE MBATIZAJI

SOMO 1

Isa 49:1-6

Nisikilizeni. enyi visiwa; tegeni masikio yenu. enyi kabila za watu mlio mbali sana; Bwana ameniita tangu tumboni: toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu. Naye anifanya kinywa changu kuwa kama upanga mkali; katika kivuli cha mkono wake amenisitiri; naye amenifanya kuwa mshale uliosuguliwa; katika podo lake amenificha.

Akaniambia; Wewe u mtumishi wangu, Israeli, ambaye katika wewe nitatukuzwa. Lakini nikasema. Nimejitaabisha bure, nimetumia nguvu zangu bure bila faida; lakini hakika hukumu yangu ina Bwana, na thawabu yangu ina Mungu wangu.

Na sasa Bwana asema hivi, yeye aliyeniumba tangu tumboni niwe mtumishi wake, ili nimletee Yakobo tena. na Israeli wakusanyike mbele zake tena; (maana mimi nimepata heshima mbele ya macho ya Bwana, na Mungu wangu amekuwa nguvu zangu); naam, asema hivi, Ni neno dogo sana wewe kuwa mtumishi wangu ili kuziinua kabila za Yakobo. na kuwarejeza watu wa Israeli waliohifadhiwa; zaidi ya hayo nitakutoa uwe nuru ya mataifa, upate kuwa wokovu wangu hata miisho ya dunia.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 139:1-3, 13-15 (K) 14

(K) Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa.

Ee Bwana umenichunguza na kunijua.
Wewe wajua kuketi kwangu na kuondoka kwangu;
Umelifahamu wazo langu tokea mbali.
Umepepeta kwenda kwangu na kulala kwangu,
Umeelewa na njia zangu zote. (K)

Maana Wewe ndiwe uliyeniumba mtima wangu,
Uliniunga tumboni mwa mama yangu.
Nitakushukuru kwa kuwa nimeumbwa
Kwa jinsi ya ajabu ya kutisha.
Matendo yako ni ya ajabu. (K)

Na nafsi yangu yajua sana,
Mifupa yangu haikusitirika kwako,
Nilipoumbwa kwa siri,
Nilipoungwa kwa ustadi
pande za chini za nchi. (K)

SOMO 2

Mdo. 13 : 22-26

Paulo alisema, Mungu alimwinua Daudi awe mfalme wao ambaye alimshuhudia, akisema, Nimemwona Daudi, mwana wa Yese, mtu anayeupendeza moyo wangu, atakayefanya mapenzi yangu yote. Katika uzao wake mtu huyo Mungu amewaletea Israeli Mwokozi, yaani, Yesu, kama alivyoahidi; Yohane alipokuwa amekwisha kuwahubiri watu wote wa Israeli habari za ubatizo wa toba, kabla ya kuja kwake. Naye Yohane alipokuwa akimaliza mwendo wake alinena, Mwanidhani mimi kuwa nani? Mimi siye. Lakini, angalieni, anakuja mmoja nyuma yangu ambaye mimi sistahili kumlegezea viatu vya miguu yake. Ndugu zangu, wana wa ukoo wa Ibrahimu, na hao miongoni mwenu wanaomcha Mungu, kwetu sisi neno la wokovu huu limepelekwa.

SHANGILIO

Lk. 1 : 76

Aleluya, aleluya, Nawe, mtoto, utaitwa nabii wake aliye juu. Utatangulia mbele za uso wa Bwana, umtengenezee njia zake. Aleluya.

INJILI

Lk. 1 : 57-66, 30

Ikawa, siku za kuzaa kwake Elisabeti zilipotimia, alizaa mtoto mwanamume. Wakasikia jirani zake na jamaa zake ya kwamba Bwana amemwongezea rehema zake, wakafurahi pamoja naye. Ikawa siku ya nane wakaja kumtahiri mtoto; wakataka kumpa jina la babaye, Zakaria. Mamaye akajibu, akasema, La, sivyo; bali, ataitwa Yohane. Wakamwambia, Hapana mtu katika jamaa" zako aitwaye jina hilo. Wakamwashiria babaye wajue atakavyo kumwita. Akataka kibao, akaandika ya kwamba, Jina lake ni Yohane. Wakastaajabu wote. Papo hapo kinywa chake kikafunguliwa na ulimi wake pia, akaanza kunena akimsifu Mungu. Wakaingiwa na hofu wote waliokuwa wakikaa karibu nao; na mambo hayo yote yakatangazwa katika nchi yote ya milima milima ya Uyahudi. Na wote walioyasikia wakayaweka mioyoni mwao, wakisema, Mtoto huyu atakuwa na namna gani? Kwa sababu mkono wa Bwana ulikuwa pamoja naye. Yule mtoto akakua, akaongezeka nguvu rohoni, akakaa majangwani hata siku ya kutokea kwake kwa Israeli.

Injili ya Bwana……..Sifa kwako Ee Kristo


a.gif Hekima ni nini?

Ni upendaji wa Mambo ya Mungu na Machukio ya Mambo ya Dunia.. soma zaidi

a.gif Je, padri akiwa mkosefu, anaweza kutuondolea dhambi?

Ndiyo, padri akiwa mkosefu, anaweza kutuondolea dhambi kwa niaba ya Mungu aliyempa mamlaka hiyo. Hatusamehewi na utakatifu wa padri, bali na huruma ya Baba kwa njia yake… soma zaidi

a.gif Baada ya hukumu ya mwisho itakuwaje?

Baada ya hukumu ya mwisho, waadilifu watatukuzwa mwili na roho pamoja na Yesu, na ulimwengu pia utageuzwa… soma zaidi



Fwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 24, 2019: JUMATATU, JUMA L A 12 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 24, 2019: JUMATATU, JUMA L A 12 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA MAJITOLEO KWA MAMA WA HUZUNI

[Wimbo Mzuri PA.gif] Mateso yako

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala ni Upendo

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Margareta Maria Alacoque

[Jarida La Bure] 👉Sala za Asubuhi na Sala za Jioni

UJUMBE-KUOMNBA-KUKUTANA-NA-NDUGU.JPG

a.gif Kwa nini Jumapili inapaswa kuitwa siku ya Bwana au Dominika?

Jumapili inapaswa kuitwa Siku ya Bwana au Dominika kwa sababu ndiyo siku Bwana amefufuka Mshindi wa Dhambi na Mauti.. soma zaidi

a.gif Umoja wa Mungu unategemea nini?

Umoja wa Mungu unategemea hasa kwamba Mwana na Roho Mtakatifu wanachanga Umungu wa Baba, ambaye wanatokana naye pasipo utengano wowote. Baba anajifahamu na kujipenda: wazo analojifahamu ndiye Mwana, upendo anaojipenda katika wazo hilo ndiye Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Je, kuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu?

La! Hakuna mahali pa lazima pa kumuadhimishia Mungu, kwa kuwa yeye hafungwi na mahali… soma zaidi

a.gif Kazi nzito zilizokatazwa kufanyika siku ya Bwana ni zipi?

Kazi nzito ni zile za kuchosha mwili na zisizo za lazima kama vile kulima, kujenga, kubeba mizigo mizito, biashara n.k… soma zaidi

a.gif Mambo yanayoweza kusababisha sala au maombi yako yasijibiwe

Mara nyingi tumekua tukiomba lakini hatupati, sababu zinaweza zikawa hizi ;.. soma zaidi

a.gif Maana kamili ya Kwaresma

Neno kwaresma ni neno la kilatini liitwalo Quadragesima maana yake ni arobaini(40). Mpenzi msomaji, katika maisha ya kikristo kuna kipindi cha siku 40.majira haya ya kwaresma huanza siku ya jumatano ya majivu na kuishia jumapili ya pasaka siku ambayo wakristo wanakumbuka kufufuka kwa yesu kristo kutoka katika wafu… soma zaidi

a.gif Sakramenti ya ndoa ni nini?

Sakramenti ya ndoa ndio yenye kuwaunganisha wakristo wawili mume namke waliopendana kwa hiari bila shuruti au vitisho au kizuizi kwa kuwapa neema ya kuishi pamoja kitakatifu wakiwalea watoto wao katika utakatifu.. soma zaidi

a.gif Ni alama zipi zinawakilisha Roho Mtakatifu?

Alama zinazowakilisha Roho Mtakatifu ni hizi; Maji, Mpako wa mafuta, Moto, wingu, tendo la kuweka mikono, njiwa.. soma zaidi

a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Upendo Mkuu wa Mungu

Mungu alimpenda sana binadamu hata akauvaa Mwili wa Binadamu akashuka duniani na kuishi kama Binadamu ili amkomboe Mwanadamu na hata akaamua kufa kwa ajili ya Binadamu kwa malipizi ya dhambi za Binadamu na kwa maondoleo ya dhambi… soma zaidi

a.gif Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa sababu gani?

Mungu aliwapa watu amri ya kusamehe dhambi kwa sababu amependa washiriki katika kazi zake. Ametuumba kwa njia ya wazazi na kutulea na kutusaidia kwa njia ya wengine pia. Hasa ametuokoa kwa njia ya Yesu, ambaye yupo nasi sikuzote katika Mwili wake, yaani Kanisa, na katika wale walioshirikishwa mamlaka ya Mitume… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.