MASOMO YA MISA, JUNI 23, 2019: SHEREHE YA MWILI NA DAMU YA BWANA WETU YESU KRISTU

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUNI 23, 2019: SHEREHE YA MWILI NA DAMU YA BWANA WETU YESU KRISTU

Somo la Kwanza

Mwa 14:18-20

Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye juu sana. Akambariki, akasema, Abramu na abarikiwe na Mungu Aliye juu sana, Muumba mbingu na nchi. Ahimidiwe Mungu Aliye juu sana, aliyewatia adui zako mikononi mwako. Abramu akampa fungu la kumi la vitu vyote.

Wimbo wa katikati

Zab 110:1-4

Neno la Bwana kwa Bwana wangu,
Uketi mkono wangu wa kuume,
Hata niwafanyapo adui zako
Kuwa chini ya miguu yako.

(K) Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki

Bwana atainyosha toka Sayuni
Fimbo ya nguvu zako.
Uwe na enzi kati ya adui zako;

(K) Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki

Watu wako wanajitoa kwa hiari,
Siku ya uwezo wako; Kwa uzuri wa utakatifu, Tokea tumbo la asubuhi, Unao umande wa ujana wako.

(K) Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki

Bwana ameapa,
Wala hataghairi,
Ndiwe kuhani hata milele,
Kwa mfano wa Melkizedeki.

(K) Ndiwe kuhani hata milele, Kwa mfano wa Melkizedeki

Somo la Pili

1Kor 11:23-26

Mimi nalipokea kwa Bwana niliyowapa nanyi, ya kuwa Bwana Yesu usiku ule aliotolewa alitwaa mkate, naye akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu. Na vivi hivi baada ya kula akakitwaa kikombe, akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu; fanyeni hivi kila mnywapo, kwa ukumbusho wangu. Maana kila mwulapo mkate huu na kukinywea kikombe hiki, mwaitangaza mauti ya Bwana hata ajapo.

Shangilio

Yn 6:51

Aleluya, aleluya
Mimi ndimi chakula chenye uzima kilichoshuka kutoka mbinguni, asema Bwana; mtu akila chakula hiki, ataishi milele
Aleluya

Somo la Injili

Lk 9:11-17

Makutano walimfuata Yesu; akawakaribisha, akawa akisema nao habari za ufalme wa Mungu, akawaponya wale wenye haja ya kuponywa. Na jua likaanza kushuka; wakamwendea wale Thenashara, wakamwambia, Uage mkutano, ili waende katika vijiji na mashamba ya kandokando wapate mahali pa kulala na vyakula, maana hapa tulipo ni nyika tupu. Akawaambia, Wapeni ninyi chakula. Wakasema, Hatuna kitu zaidi ya mikate mitano na samaki wawili, tusipokwenda tukawanunulie watu hawa wote vyakula. Kwa kuwa wanaume waliokuwako walipata kama elfu tano. Akawaambia wanafunzi wake, Waketisheni watu kwa safu, kila safu watu hamsini. Wakafanya hivyo, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi wake ili wawaandikie mkutano. Wakala, wakashiba wote; na katika vile vipande vilivyowabakia walikusanya vikapu kumi na viwili.


a.gif Katika Amri ya Nne ya Mungu tumekatazwa nini?

Tumekatazwa haya;.. soma zaidi

a.gif Tujifunze kitu hapa

Siku moja mwanamke alitoka nje ya nyumba na kuwaona wazee watatu wenye mvi kichwani wakiwa wamekaa nje ya nyumba yake.
Hakuwatambua na wala hakuwa anawafahamu… soma zaidi

a.gif Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi… soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 23, 2019: SHEREHE YA MWILI NA DAMU YA BWANA WETU YESU KRISTU

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 23, 2019: SHEREHE YA MWILI NA DAMU YA BWANA WETU YESU KRISTU

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Kanuni ya imani

[Wimbo Mzuri PA.gif] Ndiwe stara yangu Bwana

[Tafakari ya Sasa] 👉Maana ya kubarikiwa

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Klara wa Asizi

[Jarida La Bure] 👉NOVENA YA ROHO MTAKATIFU

baada-ya-kufa.JPG

a.gif Nani ni shahidi wa kwanza katika Agano Jipya?

Shahidi wa Kwanza ni Mt Stefano.. soma zaidi

a.gif Baba Mlishi wa Yesu Kristu ni nani?

Baba mlishi wa Yesu Kristo ni Yosefu Mtakatifu (Mt 1:18-20).. soma zaidi

a.gif Yuda Iskarioti

Yuda Iskarioti (kwa Kiebrania יהודה איש־קריות), Myahudi wa karne ya 1, alikuwa mmojawapo wa Mitume wa Yesu, maarufu kwa kuwa alimsaliti mwalimu wake apate vipande thelathini vya fedha (Injili ya Mathayo 26:14-16)… soma zaidi

a.gif Je, wanawake wanaweza kupewa daraja?, Mwanamke anaweza kuwa padri?

Hapana, wanawake hawawezi kupewa daraja, kwa sababu kwa karibu miaka elfu mbili mfululizo Kanisa limejiona halina mamlaka ya kufanya tofauti na Yesu. Yeye alichagua wanaume tu kuwa Mitume wake, ingawa walikuwepo wanawake waaminifu kuliko wengi wao, hasa Maria, mtakatifu kuliko wote… soma zaidi

a.gif Ni nani wahudumu wa Sakramenti ya ndoa?

Wahiudumu rasmi wa Sakramenti ya ndoa ni wachumba wenyewe, Padri kama shahidi rasmi wa kanisa. Tena ni lazima ifungwe mbele ya mashahidi wengine wawili… soma zaidi

a.gif Matumizi ya Neno 'Ameen'

Napenda kuchukua fursa hii kutoa mchango wangu juu ya matumizi mabaya ya neno "Ameen. " Hili neno linatokana na neno la Kiebrania "Amina" likiwa na maana ya "Na iwe hivyo." Neno hilo lilitumika mwishoni mwa maombi kila wakati Wayahudi walipomwomba Mungu wao… soma zaidi

a.gif Tumejuaje kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu?

Tumejua kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu kwa sababu Baba aliwatuma kwetu Mwanae na Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu siku ya mwisho

Kundi la watu lilikwenda mahala wakakuta mawe yamezagaa. Ghafla wakasikia sauti ikisema: "Atakaeokota atajuta na asiyeokota atajuta," baadhi yao wakaokota na wengine hawakuokota. Wakarudi nyumbani… soma zaidi

a.gif Vizuizi vya ndoa ni kitu gani?

Vizuizi vya ndoa ni vile vinavyofanya ndoa isiwe halali tangu mwanzo.. soma zaidi

a.gif Mababu watatu wa Imani Katika Biblia ni wakina nani?

Mababu wa Imani ni Ibrahimu, Isaka na Yakobo.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.