MASOMO YA MISA, JUNI 20, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 11 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

USIKOSE HII👉 Vyanzo vya sala za Kikristo

SOMO 1

2 Kor. 11:1 - 11

Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami. Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi. Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nancho mitume walio wakuu. Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu.

Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira? Naliwanyang’anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi. Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote nalijilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena nitajilinda. Kama vile vile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya. Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 111: 1-4, 7-8 (K) 7

(K) Matendo yako Bwana ni kweli na hukumu.

Aleluya.
Nitamshukuru Bwana kwa moyo wangu wote,
Barazani pa wanyofu wa moyo na katika mkutano. (K)

Matendo ya Bwana ni makuu,
Na haki yake yakaa milele.
Amefanya ukumbusho wa matendo yake ya ajabu;
Bwana ni mwenye fadhili na rehema. (K)

Matendo ya mikono yake ni kweli na hukumu,
Maagizo yake yote ni amini,
Yamethibitika milele na milele,
Yamefanywa katika kweli na adili. (K)

SHANGILIO

1The. 2:13

Aleluya, aleluya,
Lipokeeni neno la Mungu, siyo kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu.
Aleluya.

INJILI

Mt. 6:7-15

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Mkiwa katika kusali, msipayuke-payuke, kama watu wa mataifa; maana wao hudhani ya kuwa watasikiwa kwa sababu ya maneno yao kuwa mengi. Basi msifanane na hao; maana Baba yenu anajua mnayohitaji kabla ninyi hamjamwomba.
Basi ninyi salini hivi; Baba yetu uliyembinguni, jina lako litukuzwe, ufalme wako uje, mapenzi yako yatimizwe, hapa duniani kama huko mbinguni. Utupe leo riziki yetu. Utusamehe deni zetu, kama sisi nasi tuwasamehevyo wadeni wetu. Na usitutie majaribuni, lakini utuokoe na yule mwovu.
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Tafakari ya leo ya Katoliki kuhusu Kusali na Kuomba

Rafiki yangu, Omba utafute uso wa Mungu, Aonaye kwa Siri atakujibu kwa wazi… soma zaidi

a.gif Kuna Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso?

Faida ya kuwa na Neema ya Utakaso ni;-.. soma zaidi

a.gif Bikira Maria alimzaa Yesu Kristo kwa uwezo gani?

Bikira Maria alimzaa Yesu Kristo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu. (Lk 1:35).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 20, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 11 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 20, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 11 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Majitoleo

[Wimbo Mzuri PA.gif] Ee Mungu kwa wema wako

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Jorome

[Jarida La Bure] 👉ROZARI YA MAMA BIKIRA MARIA

KADI-SALAMU-JIONI-MZAZI.JPG

a.gif Mkristo Mkatoliki awezaje kufunga ndoa mchanganyiko au utofauti wa dini kwa uhalali?

Aweza kufunga ndoa hiyo kwa uhalali baada ya kupata ruhusa maalumu ya Askofu kwa Barua… soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Malaika

Mambo ya Msingi kujua kuhusu Malaika;.. soma zaidi

a.gif Dhambi zinatofautianaje katika uzito?

Kuna:
1. Dhambi ya Mauti (Dhambi kubwa) na
2. Dhambi nyepesi (Dhambi ndogo).. soma zaidi

a.gif Ni lini Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake?

Yesu Kristo aliwapa Maaskofu na Mapadri Uwezo wa kugeuza mkate na divai kuwa Mwili na Damu yake alipowafanya Mitume kuwa Mapadri katika karamu ya mwisho aliposema "FANYENI HIVI KWA UKUMBUSHO WANGU" (Lk 22:14-20).. soma zaidi

a.gif Mungu aliumbaje ulimwengu?

Mungu aliumba ulimwengu kwa uwezo wake kwa kusema na bila kutumia kitu chochote. (Mwa 1:1).. soma zaidi

a.gif Ni vitu gani vya msingi na vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu?

Vitu vya lazima katika kuadhimisha Ekaristi Takatifu ni.. soma zaidi

a.gif Mafundisho ya dini kuhusu Binadamu na Ubinadamu

Kuhusu ubinadamu na Binadamu haya ndiyo maswali ya muongozo;.. soma zaidi

a.gif Mungu alisema nini alipotaka kumuumba mtu?

Mungu alipotaka kumwumba mtu alisema;.. soma zaidi

a.gif Kilichowapata Watu 8 waliowahi kumdhihaki Mungu

HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA MAJANGA… soma zaidi

a.gif Je, Ni lazima kila Mkristo kupokea Sakramenti ya Kipaimara?

Ni lazima kila Mkristo kupokea Sakramenti ya Kipaimara kwa sababu ni Ukamilisho wa Sakramenti ya Ubatizo. (Mdo 8:14-17).. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.