MASOMO YA MISA, JUNI 18, 2019: JUMANNE, JUMA LA 11 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

2 Kor. 8:1 – 9

Ndugu zetu, twaarifu habari ya neema ya Mungu, waliyopewa makanisa ya Makedonia; maana walipokuwa wakijaribiwa kwa dhiki nyingi, wingi wa furaha yao na umaskini wao uliokuwa mwingi uliwaongezea utajiri wa ukarimu wao. Maana nawashuhudia kwamba, kwa uwezo wao, na zaidi ya uwezo wao, kwa hiari yao wenyewe walitoa vitu vyao; wakituomba sana pamoja na kutusihi kwa habari ya neema hii, na shirika hili la kuwahudumia watakatifu. Tena walitenda hivi si kama tulivyotumaini tu, bali kwanza walijitoa nafsi zao kwa Bwana; na kwetu pia, kwa mapenzi ya Mungu.
Hata tukamwonya Tito kuwatimilizia neema hii kwenu kama vile yeye alivyotangulia kuianzisha. Lakini kama mlivyo na wingi wa mambo yote; imani, na usemi, na elimu, na bidii yote, na upendo wenu kwetu sisi; basi vivyo hivyo mpate wingi wa neema hii pia. Sineni ili kuwaamuru, bali kwa bidii ya watu wengine nijaribu unyofu wa upendo wenu. Maana mmejua neema ya Bwana wetu Yesu Kristo, jinsi alivyokuwa maskini kwa ajili yenu, ingawa alikuwa tajiri, ili kwamba ninyi mpate kuwa matajiri kwa umaskini wake.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 146:2, 5 – 9 (K) 2

(K) Ee nafsi yuangu, umsifu Bwana.

Ee nafsi yangu umsifu Bwana
Nitamsifu Bwana muda ninaoishi,
Nitamwimbia Mungu wangu ningali hai. (K)

Heri ambaye Mungu wa Yakobo ni msaada wake,
Na tumaini lake ni kwa Bwana, Mungu wake,
Aliyezifanya mbingu na nchi,
Bahari na vitu vyote vilivyomo. (K)

Huishika kweli milele,
Huwafanyia hukumu walioonewa,
Huwapa wenye njaa chakula,
Bwana hufungua waliofungwa. (K)

Bwana huwafumbua macho waliopofuka,
Bwana huwainua walioinama,
Bwana huwapenda wenye haki
Bwana huwahifadhi wageni,
Huwategemeza yatima na mjane. (K)

SHANGILIO

Ebr. 4:12

Aleluya, aleluya.
Neno la Mungu li hai tena li na nguvu, li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
Aleluya.

INJILI

Mt. 5:43 – 48

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, pendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi; ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyk, mwapata thawabu gani? Hata watoza ushuru; je! Nao hawafanyi yayo hayo? Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi kama hayo? Basi ninyi mtakuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa sababu gani?

Mungu ametuagiza matendo maalumu ya ibada kwa kuzingatia umbile letu, kwamba binadamu ni umoja wa roho na mwili, hivyo anahitaji mwili na hisi zake ili kuingiza chochote rohoni na kutokeza yaliyomo katika roho yake isiyoonekana… soma zaidi

a.gif Matokeo ya hukumu hiyo ni nini?

Matokeo ya Hukumu hiyo ni roho kwenda Mbinguni, Toharani au Motoni. (Mt 25:34-46).. soma zaidi

a.gif Neno hili kuwa nafsi tatu kwa Mungu mmoja laitwaje?

Laitwa fumbo la Utatu Mtakatifu. (Lk, 3:21-22).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 18, 2019: JUMANNE, JUMA LA 11 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 18, 2019: JUMANNE, JUMA LA 11 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Nakupenda Maria

[Jarida La Bure] 👉NOVENA YA ROHO MTAKATIFU

mwili-utakaofufuliwa-ni-huu.JPG

a.gif Mipango ya Mungu

Mipango ya Mungu daima ni myema, Mungu anapanga Mema katika maisha ya mtu kama akifuata mapenzi yake. Tatizo ni kwamba watu wanafuata mapenzi yao wenyewe na kisha kukosa yale mema Mungu aliyopanga kwao… soma zaidi

a.gif Mazinguo ndiyo nini?

Mazinguo ni sala za kupungia mashetani ili kuepusha watu na balaa au madhara, hasa kama wamepagawa nao… soma zaidi

a.gif Kristo maana yake nini?

Kristo maana yake ni “Aliyepakwa mafuta” awe kiongozi wa taifa lake walivyotabiri manabii wa kale… soma zaidi

a.gif Ufanyialo wengine ndilo utakalofanyiwa

Siku niliposoma hili andiko kwa mara ya kwanza nakumbuka, kwanza nilipata mshtuko flani baada ya kulisoma, halafu nikajikuta nikitafakari vitu vingi sana… soma zaidi

a.gif Kwa nini tujute dhambi zetu?

Tunajuta dhambi zetu kwa sababu tumeukosea Utatu Mtakatifu na tunastahili adhabu yake, na pia bila majuto hatuwezi kupata maondoleo ya dhambi… soma zaidi

a.gif Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa nini?

Mtu akitaka kupata Rehema za Kanisa Katoliki yampasa;
1. Kujua na kufuata utaratibu unaotolewa na Kanisa Katoliki wa kupata Rehema
2. Awe katika hali ya neema ya Utakaso
3. Kufanya matendo yote yanayotakiwa kwa kupata rehema hiyo, kwa mfano;.. soma zaidi

a.gif Ni zipi Sakramenti za Huduma ya ushirika na utume?

Ni Sakramenti mbili ambazo ni Sakramenti ya Daraja na Sakramenti ya Ndoa.. soma zaidi

a.gif Upendo, Huruma, Rehema na Neema za Mungu

Mungu ni Mwingi wa Rehema, Huruma, Upendo na Neema… soma zaidi

a.gif Je, vitabu vya Biblia vinatofautiana?

Ndiyo, vitabu vya Biblia vinatofautiana kwa kuwa Mungu alijifunua hatua kwa hatua; hivyo vitabu 46 vilivyoandikwa kabla ya Yesu vinaitwa Agano la Kale na 27 vilivyomfuata vinaitwa Agano Jipya… soma zaidi

a.gif Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi wapi?

Roho Mtakatifu anaweza kutufikisha hadi muungano wa dhati na Mungu… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.