MASOMO YA MISA, JUNI 17, 2019: JUMATATU, JUMA LA 11 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

2 Kor. 6:1 – 10

Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi, msiipokee neema ya Mungu bure. Kwa maana asema, Wakati uliokubalika nalikusikia, Siku ya wokovu nalikusaidia; tazama, wakati uliokubalika ndio sasa.
Tusiwe kwazo la namna yoyote katika jambo lolote, ili utumishi wetu usilaumiwe; bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika saburi nyingi, katika dhiki, katika misiba, katika shida; katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, ktika kufunga; katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki; katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; kwa utukufu na aisbu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; kama wenye huzuni, bali sikuzote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 98:1-4 (K) 2

(K) Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,
Kwa maana ametenda mambo ya ajabu.
Mkono wa kuume wake mwenyewe,
Mkono wake mtakatifu umemtendea wokovu. (K)

Machoni pa mataifa ameidhihirisha haki yake.
Amezikumbuka rehema zake,
Na uaminifu wake kwa nyumba ya Israeli. (K)

Miisho yote ya dunia imeuona
Wokovu wa Mungu wetu.
Mshangilieni Bwana, nchi yote,
Inueni sauti, imbeni kwa furaha, imbeni zaburi. (K)

SHANGILIO

Efe. 1:17,18

Aleluya, aleluya,
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristu, awape roho ya hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.

INJILI

Mt. 5:38 – 42

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Mmesikia kwamba imenenwa Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kuume, mgeuzie na la pili. Na mtu atakaye kukushitaki na kuitwaa kanzu yako, mwachie na joho pia. Na mtu atakayekulazimisha mwendo wa maili moja, nenda naye mbili. Akuombaye, mpe; naye atakaye kukopa kwako, usimpe kisogo.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Matokeo ya hukumu hiyo ni nini?

Matokeo ya Hukumu hiyo ni roho kwenda Mbinguni, Toharani au Motoni. (Mt 25:34-46).. soma zaidi

a.gif Mtume Simoni Mkananayo

Simoni Mkananayo alikuwa mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu… soma zaidi

a.gif Utafuteje dhambi wakati wa kujiandaa kuungama?

Tafuta dhambi kwa njia hizi.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 17, 2019: JUMATATU, JUMA LA 11 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 17, 2019: JUMATATU, JUMA LA 11 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Majitoleo

[Tafakari ya Sasa] 👉Toba, msamaha na Baraka

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Karoli Lwanga

ufufuo-wa-wafu-upooo.JPG

a.gif Mbona watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika wakati wa ubatizo halafu wanabatizwa?

Ingawa watoto wachanga hawawezi kuelewa kinachofanyika, Mungu anaweza kuwamiminia rohoni mwanga wa imani… soma zaidi

a.gif Swala la Mapadri kutooa limeandikwa wapi katika Biblia?

Pengine umewahi kuulizwa swali hili wakati fulani.Na jibu lake ni kama ifuayavyo:.. soma zaidi

a.gif Je Sakramenti ya Ekaristi hujulikana kwa majina yapi?

Majina haya;.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu dhambi

Fahamu kuhusu Dhambi kwa Kusoma maswali haya;.. soma zaidi

a.gif Ni kwa nini ni Kweli Yesu Kristo yuko chini ya maumbo ya Mkate na Divai?

Nikweli Yesu Kristo yuko chini ya maumbo ya Mkate na Divai kwa sababu.. soma zaidi

a.gif Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake nini?

Yesu kuwa Mwana pekee wa Mungu maana yake ni kwamba, kabla hajazaliwa kama mtu duniani ni Mungu, sawa na Baba anayemzaa yeye tu tangu milele… soma zaidi

a.gif Kutokumuabudu Mungu ni kwa namna gani?

Ni kuruhusu kitu chochote kimtawale mtu badala ya Mungu, mfano cheo, pombe, mali, shetani, tuisheni, kazi, na kutoadhimisha Jumapili au kutoshiriki… soma zaidi

a.gif Agano la Kale lina vitabu vingapi?

Agano la Kale lina vitabu 46.. soma zaidi

a.gif Mvuto wa Maisha ya Kikristo nyumbani

Mvuto wa Maisha ya Kikristo Nyumbani.. soma zaidi

a.gif Maswali na majibu kuhusu Sakramenti ya Daraja Takatifu na Kuhusu Utawa

Fahamu kuhusu Sakramenti ya Daraja kupitia maswali haya;.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.