MASOMO YA MISA, JUNI 13, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 10 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUNI 13, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 10 LA MWAKA

KUMBUKUMBU YA MT. ANTONI WA PADUA

SOMO 1

2Kor. 3:15 – 4:1, 3 – 6

Hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. Lakini wakati wowote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. Basi ‘Bwana’ ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho.
Kwa sababu hiyo, kwa kuwa tuna huduma hii, kwa jinsi tulivyopata rehema, hatulegei. Lakini ikiwa injili yetu imesitirika, imesitirika kwa hao wanaopotea; ambao ndani yao mungu wa dunia hii amepofusha fikira zao wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu. Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana; na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Kwa kuwa Mungu, aliyesema, Nuru itang’aa toka gizani, ndiye aliyeng’aa mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 85:8 – 13 (K) 9

(K) Utukufu wake ukae katika nchi yetu.

Nisikie atakavyosema Mungu Bwana,
Maana atawaambia watu wake Amani,
Naam, na watauwa wake pia,
Bali wasiurudie upumbavu tena.
Hakika wokovu wake u karibu na wamchao,
Utukufu ukae katika nchi yetu. (K)

Fadhili na kweli zimekutana,
Haki na Amani zimebusiana.
Kweli imechipuka katika nchi,
Haki imechungulia kutoka mbinguni. (K)

Naam, Bwana atatoa kilicho chema,
Na nchi yetu itatoa mazao yake.
Haki itakwenda mbele zake,
Nayo itazifanya hatua zetu kuwa njia. (K)

SHANGILIO

Efe. 1:17, 18

Aleluya, aleluya.
Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, awape roho wa hekima mjue tumaini la mwito wake.
Aleluya.

INJILI

Mt. 5:20-26

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Haki yenu isipozidi hiyo haki ya waandishi na Mafarisayo, hamtaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni.
Mmesikia watu wa kale walivyoambiwa, Usiue; na mtu akiua, itampasa hukumu. Bali mimi nawaambieni, Kila amwoneaye ndugu yake hasira itampasa hukumu; na mtu akimfyolea ndugu yake, itampasa baraza; na mtu akimwapiza, itampasa jehanum ya moto. Basi ukileta sadaka yako madhabahuni, na huku ukikumbuka ya kuwa ndugu yako ana neno juu yako, iache sadaka yako mbele ya madhabahu, uende zako, upatane kwanza na ndugu yako, kasha urudi uitoe sadaka yako. Patina na mshitaki wako upesi, wakati uwapo pamoja naye njiani; yule mshitaki asije akakupeleka kwa kadhi, na kadhi akakupeleka kwa askari, ukatupwa gerezani. Amin, nakuambia, Hutoki humo kamwe hata uishe kulipa senti ya mwisho.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Wakati wa ibada tuvae vipi?

Wakati wa ibada tuvae namna inayodhihirisha malengo ya moyo wetu, hasa usafi na heshima, unyenyekevu na udugu… soma zaidi

a.gif Je, Yesu alirudia maisha ya duniani?

Hapana, Yesu hakurudia maisha ya duniani: tofauti na watu aliowafufua warudie maisha haya, Yesu mfufuka ameshaingia utukufu wa milele:.. soma zaidi

a.gif Rehema ni nini?

Rehema ni msamaha au ondoleo la adhabu ya dhambi tulizostahili sababu ya dhambi zilizokwisha ondolewa.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 13, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 10 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 13, 2019: ALHAMISI, JUMA LA 10 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Tafakari ya Sasa] 👉Tumaini kwa Mungu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Brigita wa Sweeden

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

UJUMBE-WA-ZA-JIONI-KWA-NDUGU.JPG

a.gif Kwa njia ya watawa Kanisa linaonyesha nini mbele ya watu wote?

Kanisa linaonyesha jinsi Yesu alivyotenda mahali popote pale alipopita kwa mfano wagonjwa, maskini, wakosefu, watoto, vilema, wenye njaa na wasiojua habari njema.. soma zaidi

a.gif Nani ni shahidi wa kwanza katika Agano Jipya?

Shahidi wa Kwanza ni Mt Stefano.. soma zaidi

a.gif Je, Mkristo akipokea kipande cha Hostia amempokea Yesu Mzima?

Ndiyo, Amempokea Yesu Mzima kabisa, Hata akipewa zaidi ya hostia moja amempokea Yesu Mzima.. soma zaidi

a.gif Ibada ni nini?

Ni roho ya kupenda utumishi wa Mungu na yote yale yenye kumpa Mungu sifa na Heshima.. soma zaidi

a.gif Baada ya kujua maisha ya Yesu tunapaswa kufanya nini?

Baada ya kujua maisha ya Yesu tunapaswa kujilinganisha naye hadi aundwe na kuishi ndani mwetu akitushirikisha uhai, kifo na ufufuko wake… soma zaidi

a.gif Neema ya Utakaso yapoteaje?

Neema ya Utakaso yapotea kwa kutenda dhambi kubwa (dhambi ya mauti).. soma zaidi

a.gif Je, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi?

Ndiyo, tumuendee padri ili kuondolewa dhambi tulizotenda baada ya ubatizo, kwa kuwa hatuwezi kupokea msamaha tukikataa masharti yake, na Mungu ametupangia watu ambao watuondolee kwa niaba yake… soma zaidi

a.gif Siku arubaini baada ya kufufuka, Yesu alifanya nini?

Siku arubaini baada ya kufufuka, Yesu alipaa mbinguni mbele ya wanafunzi wake. Hataonekana tena rasmi mpaka arudi siku ya mwisho… soma zaidi

a.gif Ni ipi sala kubwa ya Kanisa?

Sala kubwa ya Kanisa ni Misa Takatifu.. soma zaidi

a.gif Ni kwa nini Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu? Na kwa nini aheshimiwe?

Bikira Maria anaitwa Mama wa Mungu kwa sababu amemzaa Yesu na Yesu ni Mungusoma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.