MASOMO YA MISA, JUNI 12, 2019: JUMATANO, JUMA LA 10 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

SOMO 1

2Kor. 3:4 – 11

Tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lolote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko bali war oho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. Basi, ikiwa huduma ya mauti iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika; je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu? Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi. Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana. Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 99:5 – 9 (K) 9

(K) Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.

Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu;
Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
Ndiye mtakatifu. (K)

Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake,
Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake,
Walipomwita Bwana aliwaitikia. (K)

Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao.
Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa. (K)

Ee Bwana, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;
Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe
Ingawa uliwapatiliza matendo yao. (K)

Mtukuzeni Bwana, Mungu wetu;
Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;
Maana Bwana, Mungu wetu, ndiye mtakatifu. (K)

SHANGILIO

Zab. 119:135

Aleluya, aleluya,
Umwangazie mtumishi wako uso wako, na kunifundisha amri zako.
Aleluya.

INJILI

Mt. 5:17-19

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. Kwa maana, amin, nawaambia, mpaka mbingu nan chi zitakapoondoka, yodi moja wala nukata moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. Basi mtu yeyote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Maswali na majibu kuhusu Liturujia

Kuhusu Liturujia soma Makala hizi zifuatazo;.. soma zaidi

a.gif Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni nini?

Alama wazi ya Sakramenti ya Ubatizo ni kumwagia maji katika panda la uso na kutamka maneno "Fulani (jina lake linatajwa) nakubatiza kwa Jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu" (Mt 28:19).. soma zaidi

a.gif Mambo makuu manne ya mwisho ni yapi?

Mambo hayo ni;.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 12, 2019: JUMATANO, JUMA LA 10 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 12, 2019: JUMATANO, JUMA LA 10 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Wimbo Mzuri PA.gif] Maombezi yako Maria

[Tafakari ya Sasa] 👉Uhuru na Amani ya Moyoni

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Juan Diego

KADI-MMISI-MZAZI.JPG

a.gif Neno "BIBLIA" maana yake ni nini?

Neno "BIBLIA" ni neno linalotokana na neno la Kigiriki "Biblion" lenye maana ya vitabu… soma zaidi

a.gif Sala ni nini?

Sala ni kuinua mioyo yetu kwa Mungu na kuongea nae. Kuongea maana yake ni kusema na Kusikiliza. Sala sio kuongea tuu, sala ni kuongea na kusikiliza. Mungu anatualika tuongee nae kwa kusema na kusikiliza. Kwenye Biblia tunasoma Hivi;

“Niite, nami nitakujibu na kukuambia mambo makubwa yaliyofichika ambayo hujapata kuyajua".(Yeremia 33:3).. soma zaidi

a.gif Kabla ya Kupokea Ekaristi Takatifu Tunasali sala gani?

Tunasali "Ee Bwana sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona".. soma zaidi

a.gif Katika unyonge wetu tutumainie nini?

Katika unyonge wetu tutumainie huruma ya Mungu aliyetutumia Mkombozi hata “dhambi ilipozidi, neema ikawa kubwa zaidi” (Rom 5:20)… soma zaidi

a.gif Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya nani?

Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya Yesu na Kanisa lake… soma zaidi

a.gif Katika amri ya kwanza ya Mungu tumeamriwa nini?

Tumeamriwa tusadiki kuwa Mungu ni mmoja, ndiye Baba yetu na Mkubwa wetu: tumpende, tumwabudu yeye peke yake. (Mt 10:33, Kumb 6:4-9).. soma zaidi

a.gif Agano Jipya lina vitabu vingapi?

Agano Jipya lina vitabu 27.. soma zaidi

a.gif Twaharibu heshima ya wengine kwa namna gani?

Twaharibu Kwa.. soma zaidi

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Maneno na ishara kwenye ibada vinaweza kubadilishwa na nani?

Maneno na ishara vinaweza kubadilishwa na waandamizi wa Mitume, waliokabidhiwa na Yesu mamlaka ya kuendeleza kazi yake katika mazingira mbalimbali hata mwisho wa dunia… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.