MASOMO YA MISA, JUNI 10, 2019: JUMATATU JUMA LA 10 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUNI 10, 2019: JUMATATU JUMA LA 10 LA MWAKA

SOMO 1

2 Wakorintho 1: 1-7

1 Paulo, mtume wa Kristo Yesu kwa mapenzi ya Mungu, na Timotheo ndugu yetu; kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, pamoja na watakatifu wote walioko katika nchi yote ya Akaya.
2 Neema na iwe kwenu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
3 Na ahimidiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa rehema, Mungu wa faraja yote;
4 atufarijiye katika dhiki zetu zote ili nasi tupate kuwafariji wale walio katika dhiki za namna zote, kwa faraja hizo, tunazofarijiwa na Mungu.
5 Kwa kuwa kama vile mateso ya Kristo yanavyozidi kwetu, vivyo hivyo faraja yetu inazidi kwa njia ya Kristo.
6 Lakini ikiwa sisi tu katika dhiki, ni kwa ajili ya faraja yenu na wokovu wenu; au ikiwa twafarijiwa, ni kwa ajili ya faraja yenu; ambayo hutenda kazi yake kwa kustahimili mateso yale yale tuteswayo na sisi.
7 Na tumaini letu kwa ajili yenu ni imara, tukijua ya kuwa kama vile mlivyo washiriki wa yale mateso, vivyo hivyo mmekuwa washiriki wa zile faraja.

WIMBO WA KATIKATI

Zaburi 34: 2-3, 4-5, 6-7, 8-9

2 Katika Bwana nafsi yangu itajisifu, Wanyenyekevu wasikie wakafurahi.
3 Mtukuzeni Bwana pamoja nami, Na tuliadhimishe jina lake pamoja.
4 Nalimtafuta Bwana akanijibu, Akaniponya na hofu zangu zote.
5 Wakamwelekea macho wakatiwa nuru, Wala nyuso zao hazitaona haya.
6 Maskini huyu aliita, Bwana akasikia, Akamwokoa na taabu zake zote.
7 Malaika wa Bwana hufanya kituo, Akiwazungukia wamchao na kuwaokoa.
8 Onjeni mwone ya kuwa Bwana yu mwema; Heri mtu yule anayemtumaini.
9 Mcheni Bwana, enyi watakatifu wake, Yaani, wamchao hawahitaji kitu.

INJILI

Mathayo 5: 1-12

1 Naye alipowaona makutano, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;
2 akafumbua kinywa chake, akawafundisha, akisema,
3 Heri walio maskini wa roho; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 Heri wenye huzuni; Maana hao watafarijika.
5 Heri wenye upole; Maana hao watairithi nchi.
6 Heri wenye njaa na kiu ya haki; Maana hao watashibishwa.
7 Heri wenye rehema; Maana hao watapata rehema.
8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
9 Heri wapatanishi; Maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10 Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki; Maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu.
12 Furahini, na kushangilia; kwa kuwa thawabu yenu ni kubwa mbinguni; kwa maana ndivyo walivyowaudhi manabii waliokuwa kabla yenu.


a.gif Je, Biblia zote ni sawa?

Hapana, Biblia zote si sawa. Tujihadhari na matoleo mapungufu ambamo vimenyofolewa vitabu 7 vizima na sehemu kadhaa za vitabu vingine vilivyotumiwa na Wakristo wa kwanza… soma zaidi

a.gif Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo gani?

Ibada ya kutolea Daraja ya uaskofu ina matokeo yafuatayo;.. soma zaidi

a.gif Kabla ya Kupokea Ekaristi Takatifu Tunasali sala gani?

Tunasali "Ee Bwana sistahili uingie kwangu lakini sema neno tu na roho yangu itapona".. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 10, 2019: JUMATATU JUMA LA 10 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 10, 2019: JUMATATU JUMA LA 10 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉LITANIA YA MAMA WA MATESO

[Wimbo Mzuri PA.gif] Ewe Mama Uliyeumbwa

[Tafakari ya Sasa] 👉Mungu ni mwenye haki

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu John Bosco

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano Jipya

BIKIRA-MARIA-KUITWA-MAMA-WA-MUNGU-KWA-NINI.JPG

a.gif Mungu ni mwema maana yake ni nini?

Mungu ni mwema maana yake apenda na kuvitunza viumbe vyake vyote hasa wanadamu na anawatakia mema tu. (Zab, 25:8-10).. soma zaidi

a.gif Tofauti kati ya Ibada, Sadaka na Sala/maombi

Tofauti kati ya Ibada, Sadaka na Sala/maombi ni kama Ifuatavyo;.. soma zaidi

a.gif Zifahamu dhambi ambazo huondolewa na PAPA pekee au Padre kwa ruhusa maalumu kutoka kwa Baba Mtakatifu

ZIFAHAMU DHAMBI AMBAZO HUONDOLEWA NA PAPA PEKEE AU PADRE KWA MAMLAKA MAALUMU KUTOKA KWA PAPA :.. soma zaidi

a.gif Baada ya kifo cha mtu nini hutokea?

Baada ya kifo roho yake inafika mbele ya Mungu kwa hukumu ya mtu binafsi… soma zaidi

a.gif Uzima wa milele ni nini?

Uzima wa milele ni maisha ya kukaa mbinguni na Mungu yasiyokua na mwisho… soma zaidi

a.gif Je, sala inategemea maneno?

Hapana, sala haitegemei maneno mengi mazuri, bali kujijenga.. soma zaidi

a.gif Uzima wa milele

Maswali na majibu kuhusu uzima wa milele;.. soma zaidi

a.gif Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya nani?

Ndoa ya Wakristo ni sakramenti ya Yesu na Kanisa lake… soma zaidi

a.gif Ibada ya Daraja inachapa alama gani nafsini mwa aliyepewa?

1. Ibada ya Daraja inatia rohoni alama isiyofutika.. soma zaidi

a.gif Ni nani wahudumu wa Sakramenti ya ndoa?

Wahiudumu rasmi wa Sakramenti ya ndoa ni wachumba wenyewe, Padri kama shahidi rasmi wa kanisa. Tena ni lazima ifungwe mbele ya mashahidi wengine wawili… soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.