MASOMO YA MISA, JUNI 1, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 6 LA PASAKA

By, Melkisedeck Shine.

MWEZI%20WA%20ROZARI%20YA%20BIKIRA%20MARIA.png

MASOMO YA MISA, JUNI 1, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 6 LA PASAKA

SOMO 1

Mdo. 18:23-28

Paulo, akiisha kukaa Antiokia siku kadha wa kadha aliondoka, akapita kati ya nchi ya Galatia na Frigia, mji kwa mji, akiwathibitisha wanafunzi. Basi Myahudi mmoja, jina lake Apolo, mzaliwa wa Iskanderia, mtu wa elimu, akafika Efeso; naye alikuwa hodari katika maandiko. Mtu huyo alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikimwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi habari za Yesu; naye alijua ubatizo wa Yohane tu. Akaanza kunena kwa ujasiri katika sinagogi; hata Prisila na Akila walipomsikia wakamchukua kwao, wakamweleza njia ya Bwana kwa usahihi zaidi.

Na alipotaka kuvuka bahari aende mpaka Akaya, ndugu wakamhimiza, wakawaandikia wale wanafunzi wamkaribishe; naye alipofika akawasaidia sana wale waliokwisha kuamini kwa neema ya Mungu. Kwa maana aliwashinda Wayahudi kabisa kabisa mbele ya watu wote, akionyesha kwa maneno ya maandiko ya kuwa Yesu ni Kristo.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 47: 1-2, 7-9 (K) 7

(K) Mungu ndiye mfalme wa dunia yote.

Au: Aleluya.

Enyi watu wote, pigeni makofi,

Mpigieni Mungu kelele kwa sauti ya shangwe,

Kwa kuwa Bwana Aliye juu, mwenye kuogofya,

Ndiye mfalme mkuu juu ya dunia yote. (K)

Maana Mungu ndiye mfalme wa dunia yote,

Imbeni kwa akili.

Mungu awamiliki mataifa,

Mungu ameketi katika kiti chake kitakatifu. (K)

Wakuu wa watu wamekusanyika,

Wawe watu wa Mungu wa Ibrahimu.

Maana ngao za dunia zina Mungu,

Ametukuka sana. (K)

SHANGILIO

Yn. 10:27

Aleluya, aleluya,

Kondoo wangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata.

Aleluya.

INJILI

Yn. 16:23-28

Siku ile, Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Amin, amin, nawaambia, Mkimwomba Baba neno lo lote atawapa kwa jina langu. Hata sasa hamkuomba neno kwa jina langu; ombeni, nanyi mtapata; furaha yenu iwe timilifu. Hayo nimesema nanyi kwa mithali; saa yaja ambayo sitasema nanyi tena kwa mithali; lakini nitawapa waziwazi habari ya Baba. Na siku ile mtaomba kwa jina langu; wala siwaambii ya kwamba mimi nitawaombea kwa Baba; kwa maana Baba mwenyewe awapenda kwa kuwa ninyi mmenipenda mimi, na kusadiki ya kwamba mimi nalitoka kwa Baba. Nalitoka kwa Baba, nami nimekuja hapa ulimwenguni; tena nauacha ulimwengu; na kwenda kwa Baba.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu gani?

Tumuadhimishe Mungu hasa kwa maajabu aliyoyatenda katika Yesu, lakini pia katika Maria na wengine ambao wamefanana naye na kutuonyesha uwezo wa neema yake kwetu… soma zaidi

a.gif Nani Mkombozi wa watu wote?

Mkombozi wa watu wote ni Yesu Kristo, Mwana pekee wa Mungu, Bwana wetu… soma zaidi

a.gif Baada ya kufufuka Yesu alifanya nini?

Alikaa siku 40 katika nchi akaonekana na watu wengi akawatimizia Mitume mafundisho na kuweka Kanisa lake (Mt 28:16-20).. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUNI 1, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 6 LA PASAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUNI 1, 2019: JUMAMOSI, JUMA LA 6 LA PASAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉SALA YA KUTUBU

[Wimbo Mzuri PA.gif] Ewe Mama wa Mwokozi

[Tafakari ya Sasa] 👉Sala sio maneno tuu

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Brigita wa Sweeden

[Jarida La Bure] 👉Biblia Takatifu: Agano la Kale

mtu-akifa-nini-hutokea.JPG

a.gif Je, kati ya viumbe mbalimbali Mungu ameweka mpango wowote?

Ndiyo, kati ya viumbe mbalimbali Mungu ameweka mpango: alitaka malaika wasioonekana wamtumikie kwa kutusaidia sisi watu, na vile vinavyoonekana tuvitumie kwa uadilifu ili kwa njia yetu vimtukuze yeye… soma zaidi

a.gif Karama za kushangaza zina hatari gani?

Karama za kushangaza zina hatari mbalimbali, hasa zikitiwa maanani mno. Hapo ni rahisi zilete majivuno, kijicho na mafarakano… soma zaidi

a.gif Ajabu la ukombozi wa Yesu ni nini?

Ajabu la ukombozi wa namna hiyo ni kwamba, “tulipokuwa adui tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake” (Rom 5:10)… soma zaidi

a.gif Mungu aliumbaje vyote?

Mungu aliumba vyote kwa kutaka tu, bila ya kutumia chochote… soma zaidi

a.gif Tumejuaje kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu?

Tumejua kuwa Mungu ni Umoja wa nafsi tatu kwa sababu Baba aliwatuma kwetu Mwanae na Roho Mtakatifu… soma zaidi

a.gif Malaika na watu wanaweza kuchagua hata nini?

Malaika na watu wanaweza kuchagua hata wawe wema au wabaya milele… soma zaidi

a.gif Siku ya tatu baada ya Yesu kufa ilitokea nini?

Siku ya tatu roho ya Yesu ilirudi mwilini mwake na kudhihirisha utukufu wa ufufuko… soma zaidi

a.gif Watawa wanashika mashauri gani ya Kiinjili?

Watawa wanashika hasa mashauri ya useja mtakatifu, ufukara na utiifu ambayo msingi wake ni maisha na mafundisho ya Yesu kadiri ya Injili… soma zaidi

a.gif Fadhila inayoondoa uvivu ni ipi?

Fadhila inayoondoa uvivu ni utendaji.. soma zaidi

a.gif Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa sababu gani

Sakramenti ya Ekaristi Takatifu hukaa Tabernakulo kwa ajili ya watu wote hasa wagonjwa.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.