MASOMO YA MISA, JUMATTU JULAI 29, 2019 JUMA LA 17 LA MWAKA

By, Melkisedeck Shine.

Kumbukumbu ya Mtakatifu Martha

SOMO 1

Kut. 24:3-8

Musa aliwaambia watu maneno yote ya Bwana, na hukumu zake zote; watu wote wakajibu kwa sauti moja, wakasema, Maneno yote aliyoyanena Bwana tutayatenda. Basi Musa akayaandika maneno yote ya Bwana, akaondoka asubuhi na mapema, akajenga madhabahu chini ya mlima, na nguzo kumi na mbili, kwa hesabu ya kabila kumi na mbili za Israeli, akapeleka vijana wa wana wa Israeli, waliotoa sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za kuteketezwa, wakamchinjia Bwana sadaka za amani za ng’ombe.

Musa akatwaa nusu ya ile damu, akaitia katika mabakuli; na nusu ya ile damu akainyunyiza juu ya madhabahu. Kisha akakitwaa kitabu cha agano akakisoma masikioni mwa watu; wakasema, hayo yote aliyoyanena Bwana tutayatenda, nasi tutatii. Musa akaitwaa ile damu, akawanyunyizia watu, akasema, hii ndiyo damu ya agano alilolifanya Bwana pamoja nanyi katika maneno haya yote.

Neno la Bwana… Tumshukuru Mungu.

WIMBO WA KATIKATI

Zab. 50:1-2, 5-6, 14-15 (K) 14

(K) Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru.
Mungu, Mungu Bwana, amenena, ameiita nchi,
Toka maawio ya jua hata machweo yake.
Tokea Sayuni, ukamilifu wa uzuri,
Mungu amemulika. (K)

Nikusanyieni wacha Mungu wangu,
Waliofanya agano nami kwa dhabihu.
Na mbingu zitatangaza haki yake,
Kwa maana Mungu ndiye aliye hakimu. (K)

Mtolee Mungu dhabihu za kushukuru;
Mtimizie Aliye juu nadhiri zako.
Ukaniite siku ya mateso;
Nitakuokoa, na wewe utanitukuza. (K)

SHANGILIO

Lk. 8:15

Aleluya, aleluya,
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao, hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.

INJILI

Yn. 11:19-27

Watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao. Basi Martha aliposikia kwamba Yesu anakuja, alikwenda kumlaki; na Mariamu alikuwa akikaa nyumbani. Basi Martha akamwambia Yesu, Bwana, kama ungalikuwapo hapa, ndugu yangu hangalikufa. Lakini hata sasa najua ya kuwa yo yote utakayomwomba Mungu, Mungu atakupa. Yesu akamwambia, Ndugu yako atafufuka. Martha akamwambia, Najua ya kuwa atafufuka katika ufufuo siku ya mwisho.

Yesu akamwambia, Mimi ndimi huo ufufuo, na uzima. Yeye aniaminiye mimi, ajapokufa, atakuwa anaishi; nave kila aishiye na kuniamini hatakufa kabisa hata milele. Je! unayasadiki hayo?

Akamwambia, Naam, Bwana, mimi nimesadiki ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajaye ulimwenguni.

Neno la Bwana…Sifa kwako, ee Kristo

Au (2)

INJILI

Lk. 10 : 38-42

Ikawa katika kuenenda kwao aliingia katika kijiji kimoja; mwanamkw mmoja jina lake Martha akamkaribisha nyumbani kwake. Naye alikuwa na umbu lake aitwaye Mariamu, aliyeketi miguuni pake Yesu, akasikiliza maneno yake. Lakini Martha alikuwa akihangaika kwa utumishi mwingi; akamwendea, akasema, Bwana, huoni vibaya hivyo ndugu yangu alivyoniacha nitumike peke yangu? Basi mwambie anisaidie. Bwana akajibu akamwambia, Martha, Martha, unasumbuka na kufadhaika kwa ajili ya vitu vingi; lakini kinatakiwa kitu kimoja tu; na Mariamu amelichagua fungu lililo jema, ambalo hataondolewa.

Neno la Bwana… Sifa kwako Ee Kristo.


a.gif Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie nini?

Katika kutumia sanaa kwa ibada tuzingatie utakatifu na ukweli, si uzuri tu. Zisiigeuze kamwe kuwa igizo wala tamasha, kwa kuwa lengo si kuchangamsha watu bali kumtukuza Mungu… soma zaidi

a.gif Yakobo Mdogo

Yakobo Mdogo ni jina la mmojawapo kati ya Mitume wa Yesu. Anaitwa hivyo ili kumtofautisha na mtume mwenzake, Yakobo wa Zebedayo… soma zaidi

a.gif Je, karama ni zile za kushangaza tu?

Hapana, karama si zile za kushangaza tu, tena zile muhimu zaidi si hizo, bali zile zinazojenga zaidi Kanisa, kama zile za uongozi:.. soma zaidiFwatilia Website hii kupokea Makala Kama hii ya MASOMO YA MISA, JUMATTU JULAI 29, 2019 JUMA LA 17 LA MWAKA

Endelea kusoma makala hizi za kufanana na hii ya; MASOMO YA MISA, JUMATTU JULAI 29, 2019 JUMA LA 17 LA MWAKA

a.gif Mungu Anatuita Na Kutupa Nafasi Ya Kutubu Na Kumrudia Yeye Ili Atusamehe na Kutubariki

Tunaalikwa kutubu na kumrudia Mungu kwa Mioyo yetu yote na kwa nia dhabiti. Mungu ni mwaminifu, atatusamehe dhambi zetu na kutufanya kuwa wapya… soma zaidi

a.gif Tafakari Kuhusu Matumizi Ya Mali

Usiwe Bahili wa kutumia Mali ulizojaliwa na Mungu. Mungu amekupa Mali hizo ili ufurahie maisha uliyonayo ambayo siku moja yana mwisho… soma zaidi

a.gif Ahadi 15 za Rozari Takatifu

Mama Bikira Maria alitoa ahadi 15 kwa yule au wale watakaosali Rozari takatifu kila siku. Ahadi hizi aliwapa Mtakatifu Dominic na mwenye heri Alan de la Roche.
.. soma zaidi

[Sala Ya Sasa] 👉Sala ya Asubuhi ya kila siku

[Wimbo Mzuri PA.gif] Siku ile ya kufa kwangu

[Tafakari ya Sasa] 👉Upendo na ubinafsi

[Mtakatifu wa Sasa] 👉Mtakatifu Ambrosi

KADI-SALAMU-MCHANA-JION.JPG

a.gif Dhamiri inatakiwa kufuata daima masharti gani?

Dhamira inatakiwa kufuata daima masharti yafuatayo.. soma zaidi

a.gif Je, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu peke yetu?

Hapana, toka mwanzo sisi watu tunaasi mpango wa Mungu kwa kuvutwa na mashetani, yaani malaika waliokataa moja kwa moja kumtumikia; baada ya dhambi ya asili hao wanatutumia sisi pia tuangushane na wenzetu… soma zaidi

a.gif Liturujia Ifanyike mahali pa namna gani?

Liturujia ifanyike mahali palipoandaliwa vizuri iwezekanavyo kwa kuwa katika tendo la Ibada tunakutana na Mungu.. soma zaidi

a.gif Ni nini maana ya kuabudu sanamu?

Kuabudu sanamu ni kukipa kiumbe chochote heshima au upendo anaostahili Mungu peke yake… soma zaidi

a.gif Kwa nini Yesu aligeuka sura?

Yesu aligeika sura ili;.. soma zaidi

a.gif Vichwa au Mizizi ya dhambi ni ipi?

1. Majivuno
2. Uchoyo
3. Wivu
4. Hasira
5. Tamaa mbaya
6. Ulafi
7. Uvivu au uzembe.. soma zaidi

a.gif Lengo la mali ya binafsi ni lipi?

Kutosheleza mahitaji yake mtu binafsi, ya familia, ya wenye shida na ya kanisa… soma zaidi

a.gif Ina maana gani kupaka mafuta ya Krisma katika panda la uso wakati wa Kipaimara?

Inamaana kuwekwa wakfu (Yh 17:16-17)… soma zaidi

a.gif Je ni dhambi kukosa Misa Jumapili?

NDIYO. Ni dhambi kubwa kukosa Misa kwa Makusudi siku ya Jumapili/Dominika na Sikukuu zilizoamriwa… soma zaidi

a.gif Kwa namna gani Mungu Baba ndiye asili na lengo la Liturujia?

Mungu Baba ndiye asili na lengo la Liturujia kwa sababu katika liturujia anatujaza Baraka zake katika Mwanae Yesu Kristo, naye anatumiminia Roho Mtakatifu mioyoni mwetu.. soma zaidi

Fwatilia Website hii kwenye Email yako. Ingiza Email yako hapa kisha Bofya SUBSCRIBE na ufuate maelekezo

.

.

.

.

Website na, Melkisedeck Leon Shine | Tembelea website nyingine Hapa>>.